Rais Kikwete, hatima ya Tanzania 2015 iko mikononi mwako, tuepushe na machufuko yasiyo ya lazima

Rais Kikwete, hatima ya Tanzania 2015 iko mikononi mwako, tuepushe na machufuko yasiyo ya lazima

Wimana

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2012
Posts
2,449
Reaction score
718
Kwako Rais wetu mpendwa Jakaya M. K. Kikwete,

Kwanza nakupongeza kwa nia yako ya dhati ya kutupatia Katiba Mpya ya miaka 50 ijayo. Naamini ni nia yako ya dhati baada ya kugundua umuhimu wa suala hilo kwa mustakabali ufaao wa nchi yetu.

Pamoja na nia hiyo njema uliyonayo, nathubutu kusema kuwa wenzako wengi katika Chama chako cha CCM, hawakukubaliana, na inaonekana hawako tayari kuona tunapata "Katiba ya Watanzania wote" bali wangependa tuwe na Katiba "mpya" ambayo itatoa fursa zaidi kwa CCM kuendelea kutawala. Nasema hivyo kwa sababu, hakuna Mtanzania mwenye upeo au Elimu ya Sekondari ambaye haoni bidii ya Wahafidhina wa CCM kujaribu kuiteka Katiba Mpya na hili liko wazi kwa kuwa CCM (kwa maagizo ya Vikao vyake) walikuja na maelekezo kwa Wanachama wake waliochaguliwa kwenye Mabaraza ya Katiba ili kuhakikisha matakwa na Sera za CCM zinazingatiwa katika Katiba Mpya. Tumeona hayo pia hata kwa baadhi ya Makada wa CCM waliobahatika kuwa na nyadhifa kubwa Serikalini kama vile Kingunge Ngombae-Mwiru. Hawa wako tayari kuona maoni ya Watanzania juu ya Katiba mpya yanapuuzwa, ati kwa sababu tu ni kinyume cha Sera za CCM! Najiuliza, hivi hii Katiba mpya tunaounda sasa ni kwa ajili ya CCM au Tanzania? Yaani maoni ya Watanzania wote yapuuzwe ati kwa kuwa 'CCM' haikubali mambo kadhaa kwenye KAtiba mpya!

Rais wetu Kikwete, najua unayo nia ya dhati kutupatia Katiba Mpya, ila wenzako wengi hawako tayari kuona tunapata Katiba ambayo inatishia nafasi zao za kuendelea kutawala.

Mh. Rais, wewe ulikuwa kinara wa kusuluhisha mgogoro uliotokea Kenya mara baada ya Uchaguzi wa 2008 ambao ulisababisha Wakenya wengi kupoteza maisha, na wengine kuwa wakimbizi wa ndani hadi leo hii! Katiba yao mpya, imechangia sana wenzetu wa Kenya kufanya uchaguzi wa amani ambapo kila mtu na Wakenya wenyewe, wamekubaliana na MAtokeo ya uchaguzi wa mwaka 2013 na amani imetawala hadi leo.

Iwapo CCM watafanikiwa kupenyeza mambo yao katika KAtiba hii, ninayo hofu kubwa kuwa huenda maka 2015, uchaguzi mkuu usiwe wa amani kama tulivyozoea, na ktk uchaguzi wa mwaka 2010, kama sio busara/ hofu (na mgawanyiko) za wapinzani wa CCM walioshindwa ingawa hadi sasa baadhi hawakubali kuwa walishindwa (mimi naamini walishindwa ila si kwa kiwango kilichotangazwa na Tume).

Nini kifanyike?
1. Vyama vya Siasa, (na hasa CCM), vijiweke mbali na kupenyeza maslahi yao kwenye KAtiba mpya. Naamini Wapinzani nao wanajiingiza kwenye kujaribu kuchakachua Katiba mpya kwa kuwa tu CCM hawataki kuwaachia Watanzania wapate Katiba wanayoitaka.

2. Tupate Tume mpya ya Uchaguzi iliyo huru na ielezwe hivyo kwneye KAtiba.

3. Tupate daftari jipya la Wapiga kura, hili lililopo lina kasoro nyingi sana kulirekebisha maana nathubutu kusema kuwa wapiga kura wengi ni feki (hawezekani zaidi ya nusu ya waliojiandikisha wasipige kurakwenye kila uchaguzi).

Ninayo mengi,ila ikiwa utatoa fursa ili tupate Katiba ya Watanzania badala ya Katiba ya Wanasiasa, utakuwa na nafasi kubwa ya kuiacha nchi yetu ikiwa imetulia na kuziba loopholes zinazoweza kututumbukiza kwenye ghasia. Mpendwa, Rais, hatima ya nchi hii iko mikononi mwako.
 
Back
Top Bottom