Elections 2010 Rais Kikwete kama unaipenda Tanzania achia demokrasia ifanye kazi yake

Elections 2010 Rais Kikwete kama unaipenda Tanzania achia demokrasia ifanye kazi yake

Pax

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2009
Posts
268
Reaction score
87
Siku zimekwenda sana lakini hii haiwezi kuwa sababu ya wapenda amani kuendelea kutoa nasaha zetu. Mengi yamesemwa na mengine tumeshuhudia wenyewe, lakini mwisho wa yote tunamsihi amiri jeshi mkuu aachie demokrasia iamue hatima ya nchi yetu. Awaase wote aliowapa dhamana ya uchaguzi huu kwa moyomweupe waache haki itendeke. Nchi yetu imeshafikia kwenye hali ya kuwa delicate sio kama kipindi cha nyuma ambacho CCM walikuwa wanashinda kirahisi. Mahudhurio ya mikutano ya wagombea inatoa taswira fulani japokuwa tunahitaji maamuzi rasmi hapo jumapili 31 October.

Chondechonde muheshimiwa tuachie tuamue wenyewe.

The only thing necessary for the triumph of evil is for the good people to remain silent





ChondechondeC
 
Hakika akiacha demokrasia ikachukua mkondo wake atakuwa ameonesha ukomavu wa kiwango cha juu kisiasa. Na atakumbukwa daima kama rais aliyekubali kushindwa. Tuombe mambo yaende vizuri.
 
Back
Top Bottom