MaxShimba
JF-Expert Member
- Apr 11, 2008
- 35,771
- 4,065
Rais Kikwete kufungua benki ya wanawake Ijumaa Dar
Na Sadick Mtulya
RAIS Jakaya Kikwete atazindua rasmi huduma za Benki ya Wanawake nchini (TWB) Ijumaa.
Pamoja na mambo mengine, Rais Kikwete atafungua rasmi huduma maalumu ya akaunti ya wajasiriamali wa aina zote.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Tamasha la Wanawake Wajasiriamali Tanzania (TWWT), mkurugenzi mtendaji wa TWB, Margareth Mattaba Chacha alisema Rais Kikwete atafanya uzinduzi huo saa 3:00 asubuhi.
Pamoja na kuwa shughuli za kibenki kuanza mwezi mmoja uliopita, Ijumaa Rais Kikwete atafungua rasmi huduma hizo ikiwa ni pamoja na uzinduzi wa akaunti ya maalumu ya wajasiriamali wa aina zote, alisema Mattaba
Mattaba alisema TWB inatarajia kufikisha mtaji wa Sh6 bilioni mara tu baada ya akaunti ya huduma ya wajasariamali kuanza.
TWB ilianza na mtaji wa Sh2.5 bilioni lakini mara baada ya akaunti maalumu ya wajasiriamali kuanza tunatarajia mtaji wetu kukua hadi Sh6 bilioni, alisema Mattaba.
Mkurugenzi huyo alisema hadi kufikia juzi wateja walishafungua akaunti 1645 za aina mbalimbali katika benki hiyo na kwamba asilimia 75 ya waliofungua akaunti hizo ni wanawake.
Awali, Mattaba alisema TWB inajiandaa kutoa mafunzo mbalimbali ya matumizi ya kibenki kwa wanawake ili wapate changamoto ya kutumia huduma zitolewazo na mabenki nchini.
Alisema ukosefu wa elimu pamoja na kutojitambua ni miongoni mwa matatizo yanayowakumba wanawake wengi nchini.

Tuma maoni kwa Mhariri