Rais Kikwete- mambo ya kuzingatia kuelekea uzinduzi wa bunge maalumu

Rais Kikwete- mambo ya kuzingatia kuelekea uzinduzi wa bunge maalumu

mshumbue-soi

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2013
Posts
1,842
Reaction score
1,148
Mhe. Rais

Pole na majukumu
Naomba uzingatie ushauri wangu na watakaopenda kutumia njia hii kukushauri.

1.Jaza nafasi zilizowazi mpaka sasa za wajumbe ambao hawaripoti.

ZINGATIA.

a.Makundi yaliyokosa uwakilishi pamoja na kutuma maombi. Kama vile Wapentekoste PCT na wengineo kama baadhi ya madhehebu ya waislamu.

b.Makundi wanayotoka waliosalia kwenye orodha kama uliowateua hawajaripoti.

2.Hotuba ya kuzindua bunge izingatie muundo uliotokana na maoni ya wananchi kwa tume Jaji Warioba au hata ukirejea Nyalali na Kisanga.

Muundo unaokubalika ni Serikali 3 WANAOSEMA 2 Maoni yao yamefuata mchakato gani wa kitume?

Haiwezekani rasimu ya muundo wa Serikali 3 upige kura kuamua 3 au 2 wakati tume haijaandaa rasimu mbili za muundo wa Serikali 2 na 3 hivyo Bunge liamue kati ya 2au3 au kuingiza muundo wa serikali 2 kwenye 3.

3.Kama watataka serikali 2 wakujulishe uvunje bunge ukaunde tume nyingine ikusanye maoni ya serikali 1 au 2 na rasimu ya muundo 1au2 ndipo uliitishe upya
4.Zingatia pia yafuatayo ya Wana JF
 
Je sheria ya mabadiliko ya katiba inaruhusu hayo? Mfano kufidia wajumbe wasioripoti? Pia nashauri rais aache kutoa misimamo yake kuhusu katiba mpya kupitia chama chake, atauvuruga mchakato wa kupata katiba mpya..
 
Sijakuelewa vizuri,Je,ulichotoa ni ushauri,maoni,au mtazamo wa msimamo wako??
 
pamoja na yote atakayoyasema awaombe wajumbe waanze na muundo wa muungano ikipidi kwa maoni yake apendekeze serikali moja ndio itatuunganisha zaidi.
 
Back
Top Bottom