Rais Kikwete: Nabii asiyekubalika nyumbani kwake?


Obi,
Hizo degree nilitolea kama mfano tu wa jinsi watu wa nje ya Tz wanavyomtizama JK.

Kuna wakati anasifiwa na watu wa nje (mf Bush, Obama) mpaka unajiuliza kama kweli wanamaanisha au ni sisi ndo hatuoni mazuri yake.

Lakini kama watu mbalimbali walivyochangia mada, ni wazi kuna mazuri amefanya hata kama hayawezi ku outweigh mabaya yake.
 
umejitaidi kumtafutia vya kumsifia lakini jambo moja tu hujalitaja na ndio la msingi, hakuna nchi yoyote duniani iliyoendelea bila strong MANUFACTURING INDUSTRY, tiger ecenomies, china zote zimeendelea kwa strong manufacturing industry, na hapo ndio capitalist powers wame hold their advantage na hawatakubali waingilie, tunataka rais wa kuendeleza manufacturing industry badala ya kua taifa la wachuuzi, dream ya kila kijana nchi hii nowdays ni kupata frem pale kariakoo akalete makorokoro kule dubai aje auze, hatutaendelea milele, wala sio average, this guy is the worst of all kwani anayoyafanya ndio yanaumiza majority ya watanzania, kwa mfano he couldnt find new source of revenue instead when the budget reach deficit he rush to print more money( you need know someone in the inner circle to know this) as a result wananchi suffer from inflation of basic need e.g food prices are almost three times that when at the time he took office! democracy, freedom of press, road construction etc are vocabulalry not familiar to majority of tanzanian as they do not touch their daily lives, foods touch people daily lives!
 
Just a question for the JK apologists, Hivi JK alichaguliwa kuwa raisi ili afanye nini? Na so far aliyotakiwa kuyafanya yametekelezeka kwa % ngapi??

Usihangaike na kuwauliza wanaomtetea hata ukimuuliza yeye mwenyewe hajui alichaguliwa afanye nini alifikiri ni sifa kuwa rais aliona kama Mwanyi kawa rais basi na yeye naweza hakuwa na vision yeyote mbali ya kuuza sura angekuwa na busara angepumzika lakini asivyo atataka tena kipindi kingine na mambo ndiyo yata develop from bad to worse.
 
hana ajipya huyu bwana,
hana narudia tena hana
mbabaishaji tu.
 

aliyevaa kiatu ndiye anajuwa kinapombana!
 
sio kwamba jamii haioni jambo zuri lililofanywa na kikwete mfano uhuru wa habari lakini tunategemea kiongozi au rais ambae atafanya mazuri zaidi ya yaliyofanyika kwa mfano azuie wazungu wasiibe rasilimali zetu, asiuze ardhi yetu kwa mwarabu(loliondo) , asicheke na mafisadi na pia awe mkweli pindi makosa yanapofanyika, si kwamba yeye asifanye kosa lolote,
 

Kwa hali ilivyo ni ngumu sana kuwakandamiza watu wasitoe maoni na dukuduku zao kwa faida ya ujenzi wa nchi yao.
 
Amefanya na kuanzisha UDOM na kufanya watu wake wame na cha kusemea na kupiga kelele nyingi sana juu ya hilo
 
Kwa mtazamo wako hapa ume credit kama 20%
Kwa mtazamo wako hapa ume mcredit kama 40%

Kwa mtazamo wako hapa ume mcredit kama 50%

Kwa mtazamo wako hapa umem credit kama 60%

Kwa vile point zingine hujakubaliana nazo kwa mtazamo wako hapa ume mcredit kama 20%

Kwa mtazamo wako hapa ume mcredit kama 15%

Kwa mtazamo wako hapa ume mcredit kama 10%

Kwa mtazamo wako hapa ume mcredit kama 5%

Asante Kasheshe umetusaidia ku focus zaidi:
16. International Affairs: We have no "bifu" with anybody. he has done his part but Ni kweli amejitahidi.
Kwa mtazamo wako hapa ume mcredit kama 50%


Nimejiweka kama External Exam moderator nimejaribu kuzangalia point zako na kuzigrade kwa ujumla na hii naichukulia ni grade uliyompa JK kwa masuala uliyoyataja

Ukitafuta average ni sawa na kumpa JK 30% katika utendaji wake yaani

20%+40%+50%+60%+20%+15%+10%+5%+50%= 30%
 
Kwa hali ilivyo ni ngumu sana kuwakandamiza watu wasitoe maoni na dukuduku zao kwa faida ya ujenzi wa nchi yao.

kama rais akipenda anaweza kuwa mkandamizaji lakini utakuwa mwamzo wa mwisho wa mafanikio yake, kwa mfano tazama urusi kipindi cha putin
 
Ukitafuta average ni sawa na kumpa JK 30% katika utendaji wake yaani. 20%+40%+50%+60%+20%+15%+10%+5%+50%= 30%

Luteni,

Wewe unaionaje hiyo 30%? Inamtosha? Au ameonewa na 'perfomance appraisal' inabidi irudiwe🙂?

Lakini, on a serious note tunavyoelekea October kama wapiga kura na pengine watu ambao tunaweza/wanaweza kuwa mbadala wa utawala uliopo ni vema kuanza kuyatizama mambo haya kwa karibu zaidi. Si ajabu kusikia ameshinda kwa kishindo kuliko ilivyokuwa 2005.
 

Strong points.
 

Hiyo 30% nimei grade kutokana na mtazamo wako ila kwa mtazamo wangu nafikiri hata hiyo 30% asingefikisha lakini sina shaka pamoja na kuonyesha poor performance kama zilivyo shule zetu nyingi baada ya uchaguzi utasikia ka pass mtihani kwa flying colours
 
Mambo makubwa yaliyotokea wakati wa awamu ya kwanza ya JK yameimpact mfumo mzima wa kijamii na hivyo inakuwa vigumu kuona wapi tumegain kwasababu ofcourse Socially politically na pia economically,we have been loosers na sijui lini we have turned to be the gainers,coz sioni how wakati bajeti yetu ni tegemezi kwa asilimia kubwa na Taifa linaendeshwa "Kimatonya matonya" huku umasikini ukikithiri!

Kama tunakubali kuwa Taifa letu ni masikini,then cha kupima ni kwa kiasi gani tumepiga hatua tukiongozwa na mh rais kwenye kuutokomeza umasikini ambao unapelekea matatizo mengi kama magonjwa,ujinga nk.

Nimegunduwa kuwa viongozi wetu wakuu hususan mh rais mwenyewe huwa kimawazo wanaishi tofauti na matarajio na matakwa ya wananchi.....Hivyo basi Rais apimwe rather for how he has fought to eradicate poverty na si kwa jinsi gani jiji linafanana na majuu ama arabuni nk kwa majengo,fly overs ect....Viongozi wameloose touch na hivyo kutoka kwenye basics za kutuongoza ili tuweze kutoka kwenye dimbwi la umasikini....Badala yake wanatumia udhaifu uliopo ku implement siasa za danganya toto huku Taifa likiangamia.

Kuna namna siasa zinachezewa vibaya na wanasiasa wetu,namna ambayo inajeorpodize well being na stability ya taifa letu kwa kizazi kilichopo na hata kijacho kwasababu hakuna dalili kuwa mabadiliko ya kweli yatatoka from within.
 
Amemleta Drogba..
Amemleta Etoo...
Amemleta Bush...
Amemleta Maximo...
Ameleta kombe la dunia na tukapiga nalo picha..
Rais wa kwanza toka Africa kumtembelea Obama
Amewakaribisha wasanii wa bongo flava ikulu kupiga nao stori
Ameendesha mahojiano ya ana kwa ana live kupitia luninga....
Mhudhuriaji mzuri kwenye misiba,graduations na birthdays..(hata walalahoi tulipata nafasi ya kumshika mkono).
Kuna mwaka Miss Utalii ilitaka kushindikana kufanyika kwa kukosekana fedha ,akaiokoa na ikafanyika
Sasa watz wenzangu hapo nyumbani mngeyaona wapi yote hayo ???asili ya binadamu ..akiondoka ndiyo mtamkumbuka kwa 'mema'...
 

jmushi
Mimi naona the opposite is true kwamba mambo makubwa ambayo hayajafanyika ndiyo inatufanya tusione kama tume gain au tume lose sijaona jambo kubwa lolote la maendeleo limefanyika katika awamu hii kwa hiyo hatuwezi kupima kitu kama hatuna cha kupima

well wakati wa awamu ya pili liona mambo makubwa yalifanyika kama kuruhusu mfumo huria wa biashara kuruhusu mfumo wa vyama vingi hayo ndiyo tunaweza kusema ni mambo makubwa hata hivyo huwezi kuyapima kwa muda mfupi

naweza kusema katika awamu ya tatu pia kuna mambo makubwa talitokea mfano kukua kwa ukusanyaji wa kodi kuliosababisha kukua kwa pato la taifa vile vile kuingia mikataba mingi fake ambayo JK amekuja kuirithi

Jambo kubwa ambalo JK angeweka historia ni kuivunjilia mbali hiyo mikataba fake in contrary yeye ndiyo anaendelea kuikumbatia labda naweza kusema jambo kubwa ambalo JK amefanikiwa ni kutokuchukua maamuzi magumu yanayoweza kusambaratisha wanamtandao
 

Hizi ni kama decorations tu katika nyumba mtu atakayekuja ku evaluate thamani ya nyumba huwa haviangalii na sisi hapa sidhani kama hivyo vitatusaidia kum evaluate JK hata nyumba za makuti ndani huwa na mapambo lakini hayawezi kuongeza thamani ya nyumba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…