Uchaguzi 2020 Rais Kuamuru watendaji wa wilaya kutoa fedha ili mradi fulani ukamilike wakati wa kampeni za uchaguzi ni halali?

Uchaguzi 2020 Rais Kuamuru watendaji wa wilaya kutoa fedha ili mradi fulani ukamilike wakati wa kampeni za uchaguzi ni halali?

tathmini

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2011
Posts
318
Reaction score
250
Ni kawaida kwa mgombea wa urais John Pombe Magufuli kutoa maelezo katika sentensi zinazopingana. Amefanya hivyo tena Musoma. Amesema kuwa amekataa kupeleka maendeleo kwenye maeneo yanayoongizwa kibunge na watu wanaomtukana, lakini muda mfupi baadaye akasema kuwa maendeleo hayana chama. Huo ni udhaifu wake.

Hapo havunji sheria. Lakini mwishoni akawa si tu anajipinga bali kama vile anavunja sheria za uchaguzi kwa kutoa amri kwa viongozi mbalimbali wa serikali kutoa fedha kwa ajili ya miradi, tena kwa kupinga maamuzi halali ya usimamizi wa fedha wa wilaya. Ni kama rushwa fulani hivi ya uchaguzi.

Wengine mnasemaje?
 
Ni ukakasi wa Hali ya juu... Kuongea mwenyewe na kujipinga mwenyewe...
 
Ni kawaida kwa mgombea wa urais John Pombe Magufuli kutoa maelezo katika sentensi zinazopingana. Amefanya hivyo tena Musoma. Amesema kuwa amekataa kupeleka maendeleo kwenye maeneo yanayoongizwa kibunge na watu wanaomtukana, lakini muda mfupi baadaye akasema kuwa maendeleo hayana chama. Huo ni udhaifu wake. Hapo havunji sheria. Lakini mwishoni akawa si tu anajipinga bali kama vile anavunja sheria za
uchaguzi kwa kutoa amri kwa viongozi mbalimbali wa serikali kutoa fedha kwa ajili ya miradi, tena kwa kupinga maamuzi halali ya usimamizi wa fedha wa wilaya. Ni kama rushwa fulani hivi ya uchaguzi. Wengine mnasemaje?
Maji ya shingo mkuu!!! Hali si hali Lumumba alafu ata ushindi wa mezani kuupata ni mbinde!! Anachofanya sasa ni kujitoa tu ufahamu na kuvunja sheria za gharama za uchaguzi
 
Ajira zinatolewa wakati wa kampeni, maagizo yanaendelea ili tu kutufurahisha wapiga kura kwa muda...

HATUDANGANYIKI. Siku zote walikuwa wapi?
 
Acha watoe ni pesa zetu hizo na huu ndio msimu wetu kuvuna.
 
Back
Top Bottom