Rais kuhutubia wazee wa Dodoma

Mutensa

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2009
Posts
421
Reaction score
92
Wanajamvi,
Heshima mbele. Naomba niulize na ninaomba majibu maridhawa ili mimi na watanzania wengine tujifunze kupitia JF. Swali langu ni "nini hasa maana ya rais kuhutumia/kuongea na wazee wa Dodoma?"
Nimekuwa nikijiuliza hili bila majibu, kwa mfano kwa nini asiongee na wazee wa singida au rukwa au dar es salaam au mkoa mwingine. Nitafurahi zaidi kama nitapata majibu ya kuelimisha na si kubadili mjadala huu kuwa chanzo cha marumbano au sehemu ya chokochoko.samahani kama kuna mtu alishauliza swali hili, naomba link ya kufika kwenye swali hilo na majibu yake.
Nawasilisha.
 
Rais anapozungumza na kundi fulani la jamii, ndio anafikisha ujumbe kwa Taifa zima. Mara nyingi maRais wa Tanzania wamekuwa wakizungumza na Wazee wa Dar es Salaam manake Serikali iko Dar, japo wanadai Makao Makuu yako Dom. Hivyo kwa kuwa Makao Makuu ya Serikali yako Dom, na Rais alitaka kulihutubia Taifa kuhusu mtikisiko wa Uchumi, alichagua Wazee wa Dom na Wabunge kulifikishia ujumbe Taifa. Anaweza pia kuamua kuhutubia Wazee wa Singida, Ruvuma ama Mjini Magharibi. Kama alivyolihutubia Taifa Mwanza alipozungumzia pamoja na mambo mengine Sangara (mapanki). Hivyo aweza kuhutubia mkoa wowote na kuwaita Wazee. Wazee ni hazina.
 
Rais anapoamua kuzungumza na Wazee wa mkoa fulani, anakuwa amekusudia kuongelea jambo muhimu ambalo kwa kiasi kikubwa linahusu mkoa huo. Vile vile, hutumia mwanya huo kuwaomba wazee hao kumsaidia, kuelezea umaa ama tu kushirikiana na serikali yake katika yale anayotaka kuwaeleza.

Katika kikao alichokutana na Wazee Dodoma mwanzoni mwa mwezi huu, nia yake kuu ilikuwa ni kuomba Wabunge kuielewa Bajeti ya Serikali iliyokuwa inakusudiwa kupelekwa Bungeni siku inayofuata na kusaidia kuikubali ili itumike kwa mwaka unaofuata wa fedha. Alizungumza na wabunge pamoja na wazee wa mkoa wa Dodoma ili kufikisha ujumbe huo bila ya kuonekana moja kwa moja kushinikiza wabunge kukubali Bajeti hiyo. Hii ilisababishwa na uwepo wa wabunge wote Dodoma.

Alishasikia tetesi za kukataliwa kwa Bajeti, labda ndio sababu za kufanya hivyo. Anaweza kukutana nao tena katika kutaka kusawazisha haya mapya yanayotokea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…