Rais kumlaumu Mkuu wa Mhimili wa Bunge, hatua mujarabu ni avunje Bunge

Rais kumlaumu Mkuu wa Mhimili wa Bunge, hatua mujarabu ni avunje Bunge

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
Rais Samia Suluhu Hassan kusema kiongozi mhimili wa Bunge kuusema mhimili wa serikali kuu yaani taasisi ya Urais ni dalili za kutengeneza mazingira ya kushindana naye katika uchaguzi wa 2025 inaashiria hali ya sintofahamu ndani ya chama tawala.

Huku bunge la Tanzania kuwa la chama kimoja baada ya uchaguzi mkuu kufanyika 28 October 2020, na spika wake pia kutoka chama hicho hicho cha CCM maana yake Spika Job Ndugai kupitia caucus ya wabunge wa CCM ndani ya Bunge wapo upande mmoja na Spika Ndugai kupeleka ujumbe wa kutokuwa na imani na mwenendo wa serikali ya awamu ya sita.

04 January 2022

KWA HASIRA: RAIS SAMIA AMJIBU SPIKA NDUGAI KISOMI - "UNA STRESS za 2025, KELELE HAZINISHUGHULISHI"

Uwezo huo kikatiba wa kulivunja Bunge anao, lakini hofu yake ni kuwa tutalazinika kwenda kwenye uchaguzi mwingine.

Hicho ndiyo kimbembe😁
 
Tulizoe kuona mkuu wa mhimili wa Bunge yaani spika wa Bunge akiwepo kila pahala penye shughuli ya serikali tangu utawala wa John Pombe Magufuli.

Sasa baada ya kauli kinzani kutolewa kwanza na Spika Job Ndugai na leo hii tarehe 04 Januari 2022 mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kumjibu mkuu wa mhimili wa Bunge ni dhahiri mazoea ya mihimili hii inayoongozwa na wanaCCM wavaa sare za kijani kuonekana wamoja mbele ya umma wa waTanzania hatutayaona labda spika ajiuzulu na pia kama spika alitumwa na caucus ya wabunge wa CCM basi hakuna namna zaidi ya Bunge kuvunjwa uchaguzi ufanyike.

TOKA MAKTABA:

MAHUSIANO 'MAZURI' KATI YA RAIS NA SPIKA
thumb_430_800x420_0_0_auto.jpg
Imewekwa: July 18th, 2019

Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ametembelea Wilaya ya Kongwa na kuongea na wananchi wa Kongwa katika viwanja vya Ofisi ya Mbunge. Rais Magufuli ameongeza na wananchi baada ya kutoka kutembelea kaburi alikozikwa baba yake Mhe Joab Ndugai ambaye ni Spika wa Bunge la Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Kongwa Source : Rais Magufuli Aongea na Wananchi wa Kongwa

1.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana kwa furaha na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai mara baada ya kuwasili nyumbani kwake Sala Sala nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam
source : RAIS DKT. MAGUFULI AMJULIA HALI SPIKA WA BUNGE JOB NDUGAI PAMOJA NA WAZIRI MKUU MSTAAFU JOHN SAMUEL MALECELA JIJINI DAR ES SALAAM AGOSTI 16,2016 | Blogu Rasmi ya Ofisi ya Rais
 
Rais Samia Suluhu Hassan kusema kiongozi mhimili wa Bunge kuusema mhimili wa serikali kuu yaani taasisi ya Urais ni dalili za kutengeneza mazingira ya kushindana naye katika uchaguzi wa 2025 inaashiria hali ya sintofahamu ndani ya chama tawala.

Huku bunge la Tanzania kuwa la chama kimoja baada ya uchaguzi mkuu kufanyika 28 October 2020, na spika wake pia kutoka chama hicho hicho cha CCM maana yake Spika Job Ndugai kupitia caucus ya wabunge wa CCM ndani ya Bunge wapo upande mmoja na Spika Ndugai kupeleka ujumbe wa kutokuwa na imani na mwenendo wa serikali ya awamu ya sita.

04 January 2022

KWA HASIRA: RAIS SAMIA AMJIBU SPIKA NDUGAI KISOMI - "UNA STRESS za 2025, KELELE HAZINISHUGHULISHI"

Job aliongea kama Job sio kama mhimili ,Bungeni wanaongea Sana tuu lakini hakuna mwenye shida.

Ikumbukwe pia mwendazake aliwahi waandikia barua za kujieleza wabunge walioharibu kupinga bajeti yake.
 
Kukivunja
Uwezo huo kikatiba wa kulivunja Bunge anao, lakini hofu yake ni kuwa tutalazinika kwenda kwenye uchaguzi mwingine.

Hicho ndiyo kimbembe😁
Na am sure hofu ingine kwenye uchaguzi uwezekano wa kutoboa mdogo na matozo aya
 
Samia mwenyewe ndie anaeiwaza 2025 ajabu anawasema wengine, kilichompeleka kuwaambia wanawake wenzake 2025 ni zamu yao kilikuwa kitu gani?

Vita aliyoianzisha mwenyewe sasa hivi anatafuta mlango wa kutokea, apambane kama wengine asitumie nafasi yake kama mkuu wa nchi kujiona ana haki zaidi ya wengine wakati nae amekuwa akitoa kauli za ubinafsi, ikulu sio mahali pa mipasho.
 
Tulizoe kuona mkuu wa mhimili wa Bunge yaani spika wa Bunge akiwepo kila pahala penye shughuli ya serikali tangu utawala wa John Pombe Magufuli.

Sasa baada ya kauli kinzani kutolewa kwanza na Spika Job Ndugai na leo 04 Januari 2022 mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kumjibu mkuu wa mhimili wa Bunge
Haikuwa hivyo kabla ya utawala huo
 
Samia mwenyewe ndie anaeiwaza 2025 ajabu anawasema wengine, kilichompeleka kuwaambia wanawake wenzake 2025 ni zamu yao kilikuwa kitu gani?

Vita aliyoianzisha mwenyewe sasa hivi anatafuta mlango wa kutokea, apambane kama wengine asitumie nafasi yake kama mkuu wa nchi kujiona ana haki zaidi ya wengine wakati nae amekuwa akitoa kauli za ubinafsi, ikulu sio mahali pa mipasho.
Hii yote ni baada ya gazeti la uhuru kurusha jiwe gizani.....
 
Nguvu ya causus ya wabunge wa CCM inayoongozwa na Spika:

https://www.mwananchi.co.tz › kitaifa
CCM yafanyia kazi pendekezo la Ndugai - Mwananchi

22 Apr 2021 — Hata hivyo, baada ya kauli hiyo Spika wa Bunge, Job Ndugai aliushauri uongozi wa Kamati ya wabunge wa CCM, (party caucus) uitishe kikao .....

Taarifa Ya Caucus Ya Wabunge Wa CCM | PDF - Scribd

19 Jan 2019 — Wabunge wa Chama cha Mapinduzi wampongeza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG

Wabunge Wa Ccm | Facebook

Ukurasa rasmi ya 'Party Caucus' ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), CCM ina Jumla ya Wabunge
 
03 January 2022
Dodoma, Tanzania

NDUGAI AITISHA MAOMBI, RAIS SAMIA SULUHU HASSAN MGENI RASMI DODOMA 29 JANUARY 2022

Spika wa Bunge la Muuungano wa Tanzania Mh.Job Ndugai alifanya mkutano na waandishi wa habari Januari 3 , 2022 katika Ofisi za Bunge Jijini Dodoma na kuwaalika pia waandishi wa habari wahudhurie siku hiyo maalum ya maombi 29 January 2022
 
Picha ya jinsi caucus ya wabunge CCM inavyojiendesha bungeni pembezoni mwa kumbi rasmi ya Bunge ili waweze kuwa wamoja ktk hoja zinazoendelea au zitakazowakikishwa mbele ya Bunge

Monday, January 18, 2016​

Party Caucus ya Wabunge wa CCM inaendelea Mjini Dodoma​

Wabunge wa chama Tawala CCM wako Dodoma kwa kikao cha Kikao cha Party Caucus.

Source : peterdafi.blogspot.com
 
Uwezo huo kikatiba wa kulivunja Bunge anao, lakini hofu yake ni kuwa tutalazinika kwenda kwenye uchaguzi mwingine.

Hicho ndiyo kimbembe[emoji16]
Hawezi kuvunja bunge, akivunja bunge amevijua urais automatic. Labda ashughulike na ndugai kama ndugai
 
04 January 2022

Dr. Azavery Lwaitama - Rais ana kura ya turufu katika sakata hili la mihimili ya Bunge na Serikali Kuu

Kofia ya pili ya Rais kama mwenyekiti wa CCM ina mpa uwezo wa kushawishi chama kuwa Spika Ndugai afukuzwe uanachama na hivyo kupoteza ubunge na nafasi ya uspika

Source : Mubashara studio
 
Toka maktaba

07 May 2021
Dodoma, Tanzania

SPIKA NDUGAI ATOA MASHARTI KWA VYAMA VYA SIASA VINAVYOTAKA KUFUKUZA WABUNGE

Spika wa Bunge , Job Ndugai amevitaka vyama vya siasa vinavyotaka kufukuza wanachama wao ambao ni wabunge kufuata sheria na taratibu zote kwani lazima mchakato huo utendeke kwa haki.

Aidha, ameendelea kusisitiza kuhusu wabunge 19 waliofukuzwa uanachama Chadema, akitaka kupatiwa vielelezo kuhusu kufukuzwa kwao na kwamba huo ni msimamo wa kiti.

Wabunge hao 19 akiwemo Halima Mdee walifukuzwa Chadema Novemba mwaka 2020 baada ya kuapishwa kuwa wabunge bila ridhaa ya chama hicho lakini wameendelea kuwa wabunge jambo ambalo kwa nyakati tofauti Chadema wamelipinga huku Ndugai akidai hana vielelezo.

“Maamuzi ninayotoa hapa, ni maamuzi ambayo yatatumika nami na hata watakaofuata baada yangu… Kwa vyama vyovyote vyenye kufukuza wabunge…. wanapaswa wanapomwandikia barua spika… lazima barua hiyo iambatane na katiba yao, iambatane na muhtasari au mihtasari ya vikao vilivyohusika kuwafukuza wabunge hao,” Spika Ndugai ameeleza hayo leo bungeni mjini Dodoma na kusistiza kuwa anaposema kitu isichukuliwe kama ni Job Ndugai ndiye amesema, bali kiti cha Spika wa Bunge.

Pika Ndugai amesema maamuzi hayo hayawalengi wabunge wa upande mmoja tu bali kwa chama chochote cha siasa ambacho kitakuwa na nia ya kuwatimua wabunge.

Amesema kwa kufanya hivyo inarahisisha kazi yake ya kutenda haki
 
Haikuwa hivyo kabla ya utawala huo

Jamaa mwendazake alijichimbia mhimili wake kiasi katika demokrasia ya si coca cola kwa Tanzania tukashindwa kutofautisha mihimili ya serikali kuu (taasisu ya urais) executive, Bunge na Mahakama.

El poder ejecutivo está separado del legislativo y el judicial en una democracia
 
06 January 2022

Albert Chalamila - Nashauri Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mh. Ndugai ajiuzulu

Chalamila azungumzia hali ya kisiasa ndani ya CCM kufuatia mtifuano baina ya mihimili miwili ya nchi / dola inayoongozwa na wanaCCM waandamizi

Source : wasafi media
 
Back
Top Bottom