Jabali la Siasa
JF-Expert Member
- Jul 10, 2020
- 2,823
- 2,466
Shaka: Kibali Rais Samia kusafiri nje amepewa na CCM
MONDAY DECEMBER 06 2021
Summary
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Shaka Hamdu Shaka amesema kibali cha kusafiri nje ya nchi, Rais Samia Suluhu Hassan amepewa na Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho.Dar es Salaam. Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Shaka Hamdu Shaka amesema kibali cha kusafiri nje ya nchi, Rais Samia Suluhu Hassan amepewa na Ilani ya Uchaguzi ya chama hicho.
Shaka ameeleza hayo leo Jumatatu Desemba 6, 2021 mbele ya Rais Samia, kwenye hafla ya kuzindua kiwanda cha Elsewedy Electronic East Africa Ltd cha kuzalisha vifaa vya umeme (Electronic Products ) kilichopo Kisarawe II, Wilaya ya Kigamboni Dar es Salaam.
Shaka amesema kumekuwa na maswali mengi kwa watu kuhoji kwanini Rais huyo amekuwa akisafiri nje ya nchi mara kwa mara na kwamba ilani ya chama hicho imempa njia na nguvu namna ya kusimamia diplomasia ya uchumi wa ndani ya nchi.
“Kumekuwa na maswali kwanini Rais anasafiri sana nchi za nje. Amepewa baraka na kibali cha kusafiri nje ya nchi na ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ibara ya 132 kifungu kidogo cha 18, kifungu kidogo cha 22 kifungu kidogo cha 32 kifungu kidogo cha 46imemuonesha namna ya kusimamia diplomasia ya uchumi wan chi.,”amesema Shaka
Amesema Uongozi ni kitu cha ajabu sana na uhalisia wa uongozi utangulizwa na uzalendo na kwamba Rais huyo ameshaonesha asilimia 100 kutokana na ujasiri,utayari,karama ya udhubutu wa kutekeleza ilani kwa Weledi na kwa mafanikio makubwa.
Amesema hadi sasa Rais huyo muelekeo wake ni mzuri na alipeleka taifa kule ambako walio wengi wanatarajia kuwa na uchumi unaokuwa kila siku ndani ya Afrika na kuwafanya watanzania kujivunia nafasi yao ya kijiografia.