Siasa ziwekwe mbali na maeneo ya kitaaluma. Kwa VC kuteuliwa na Rais, huko ni kuleta siasa vyuoni-kitu ambacho wote (bila kujali itikadi zetu) tutakuja kukijutia. Siku hizi hawa ma-VC hawafanyi tena kazi za taaluma, wao ni siasa mwanzo mwisho. Mfumo wa sasa haufai ktk mazingira haya ya siasa za vyama vingi na ushindani mkali wa sasa.
Kila wanachokiamua, kwanza wanakuwa wamekiangalia kwa lenzi ya siasa. Mfano mzuri ni kufukuzwa wanafunzi UDSM hivi karibuni. Hawakuishia kuwafukuza tu, wameamua wasisome chuo chochote cha Umma na hata kupata mkopo wa bodi. Sasa hapa tujiulize UDSM wamepata wapi mamlaka ya kuzuia wanafunzi waliowafukuza wasidahiliwe vyuo vingine vya umma? Toka lini UDSM ikawa na mamlaka ya kuviamulia vyuo vingine vya umma kama sio siasa hizi?
Mwisho nipendekeze mchakato wa kumpata VC uanzie ngazi za chini kabisa ktk chuo husika. Wahadhiri wapendekeze majina ambayo TCU watachagua mmojawapo. Hii itawafanya ma-VC kuwajibika kwa wanataaluma wenzao, badala ya kuwajibika kwa wanasiasa na chama tawala na kuwadharau wanataaluma wenzao kana kwamba hawajawahi kuwa wanataaluma.