Rais kutwaa ardhi kwa manufaa ya umma mita za mraba 233,000 Manispaa za Ubungo na Kinondoni

Insidious

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2020
Posts
654
Reaction score
895
Tangazo linatolewa kwamba Mheshimiwa Rais anakusudia kutwaa kwa manufaa ya umma ardhi ya ukubwa wa mita za mraba 233,000 zilizopo Manispaa ya Kinondoni na Ubungo Mkoa wa Dar es Salaam na inayohusisha makazi ya watu katika makutano ya Barabara ya Bagamoyo na Kunduchi (Mbuyuni), Sam Nujoma na Chuo Kikuu cha Ardhi Mkabala na Mlimani City na eneo linalomilikiwa na Manispaa ya Ubungo lililopo Simu 2000 na Boko Basiaya.

Mtu yeyote anayedai kuwa na haki yoyote katika ardhi hiyo anatakiwa kutoa maelezo na uthibitisho wa haki hiyo kwa Mheshimiwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Mendeleo ya Makazi ndani ya majuma sita (6) kutoka tarehe ya tangazo hili kutolewa katika Gazeti la Serikali.

Source: Rais kutwaa ardhi

Rais Kutwaa 00.PNG
Rais Kutwaa 2.PNG
Rais Kutwaa 3.PNG
 
Right, inakubalika hasa pale serekali inapohitaji eneo kwa maendeleo ya umma.
 
Mh Rais Acha kusumbua watu, njoo utwae huku mkoa wa Pwani maeneo bado ni mapori tu
 
Hivi wakuu gazeti la serikali naweza kulisomaje online? Kuna tangazo nimeliona Rais wa jamuhuri kwa mujibu wa sheria na wizara ya ardhi wanataka kutwaa eneo lenye Square mtr 233,000, kuanzia mawasiliano,mbuyuni njia panda ya kunduchi,na boko basihaya,kwajili ya mradi wa maendeleo.

Sasa ningependa kujua hivi huwa serikali ikitaka eneo kwani lazima itoe tangazo, si wanawapa tu taarifa raia na kulitwaa kwajili ya mradi wa maendeleo.

----
Taarifa ya Kawaida Na.14607

WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
SHERIA YA UTWAAJI ARDHI (SURA 118)
(Chini ya Fungu la 6)​

Tangazo linatolewa kwamba Mheshimiwa Rais anakusudia kutwaa kwa manufaa ya umma ardhi ya ukubwa wa mita za mraba 233,000 zilizopo Manispaa ya Kinondoni na Ubungo Mkoa wa Dar es Salaam na inayohusisha makazi ya watu katika makutano ya Barabara ya Bagamoyo na Kunduchi (Mbuyuni), Sam Nujoma na Chuo Kikuu cha Ardhi Mkabala na Mlimani City na eneo linalomilikiwa na Manispaa ya Ubungo lililopo Simu 2000 na Boko Basiaya.

Mtu yeyote anayedai kuwa na haki yoyote katika ardhi hiyo anatakiwa kutoa maelezo na uthibitisho wa haki hiyo kwa Mheshimiwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ndani ya majuma sita (6) kutoka tarehe ya tangazo hili kutolewa katika Gazeti la Serikali.

Inatangazwa pia kwamba kama Mheshimiwa Rais hakuagiza vinginevyo kuhusu siku ya kuingia katika ardhi hiyo, ananuia kuingia katika ardhi hiyo yatakapoisha majuma sita (6) toka tarehe ya kutolewa kwa tangazo hili katika Gazeti la Serikali.

Mtu yeyote ambaye kwa hila au makusudi atamzuia mtu yeyote ambaye amepewa madaraka ipasavyo kisheria kuingia katika ardhi hiyo atakuwa na makosa chini ya Sheria iliyotajwa hapo juu na atalazimika kulipa faini isiyozidi shilingi elfu tano (Shs. 5,000/=) au kufungwa kwa muda usiozidi miaka miwili au vyote faini na kifungo.

Limetolewa Dodoma siku hii ya tarehe 06 Mwezi Novemba, 2024.
...........................................
Deogratius J. Ndejembi (Mb)
WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
 
Mi nataka kujua tu, hao wakazi wa eneo hilo watahamishwa kupisha eneo hilo na je watalipwa fidia? Maana ni eneo kubwa, ni kama mji kuwahamisha wakazi wake itabidi mabilioni ya pesa yatumike kwa zoezi hilo la kuhamisha wananchi wa eneo hilo
 
Ingia website ya wizara ya ardhi, au pia ingia google tafuta tanzlii ni website ya hukumu za mahakama ila pia huwa kuna sehemu ya G.N nenda sehemu ya government gazette utafutie hapo.

Ila kwa aina ya taarifa unayoitafuta ni rahisi kuipatia wizara ya ardhi na kwenye tovuti ya halmashauri husika.
 
Kama ni kweli basi hii serikali ya Samia inaukatili sana dhidi ya wananchi wake.kila sehemu inawafukuza ili kuwauzia wawekezaji.wamasai walifukuzwa na Hawa Tena anataka kuwaondoa kwenye maeneo Yao ya asili. Hatari sana Huyu mama.
 
Jambo la maendeleo ni la wote mkuu, serikali inataka kuweka mradi mkubwa maeneo hayo, nadhani wananchi watalipwa vizuri bila mgogoro.
 
Kama ni kweli basi hii serikali ya Samia inaukatili sana dhidi ya wananchi wake.kila sehemu inawafukuza ili kuwauzia wawekezaji.wamasai walifukuzwa na Hawa Tena anataka kuwaondoa kwenye maeneo Yao ya asili. Hatari sana Huyu mama.
Taarifa ya Kawaida Na.14607

WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
SHERIA YA UTWAAJI ARDHI (SURA 118)
(Chini ya Fungu la 6)

Tangazo linatolewa kwamba Mheshimiwa Rais anakusudia kutwaa kwa manufaa ya umma ardhi ya ukubwa wa mita za mraba 233,000 zilizopo Manispaa ya Kinondoni na Ubungo Mkoa wa Dar es Salaam
na inayohusisha makazi ya watu katika makutano ya Barabara ya Bagamoyo na Kunduchi (Mbuyuni), Sam Nujoma na Chuo Kikuu cha
Ardhi Mkabala na Mlimani City na eneo linalomilikiwa na Manispaa
ya Ubungo lililopo Simu 2000 na Boko Basiaya.

Mtu yeyote anayedai kuwa na haki yoyote katika ardhi hiyo anatakiwa kutoa maelezo na uthibitisho wa haki hiyo kwa Mheshimiwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ndani ya majuma sita (6) kutoka tarehe ya tangazo hili kutolewa katika Gazeti la Serikali.

Inatangazwa pia kwamba kama Mheshimiwa Rais hakuagiza vinginevyo kuhusu siku ya kuingia katika ardhi hiyo, ananuia kuingia
katika ardhi hiyo yatakapoisha majuma sita (6) toka tarehe ya kutolewa kwa tangazo hili katika Gazeti la Serikali.

Mtu yeyote ambaye kwa hila au makusudi atamzuia mtu yeyote
ambaye amepewa madaraka ipasavyo kisheria kuingia katika ardhi hiyo atakuwa na makosa chini ya Sheria iliyotajwa hapo juu na atalazimika kulipa faini isiyozidi shilingi elfu tano (Shs. 5,000/=) au kufungwa kwa
muda usiozidi miaka miwili au vyote faini na kifungo.

Limetolewa Dodoma siku hii ya tarehe 06 Mwezi Novemba, 2024.

...........................................
Deogratius J. Ndejembi (Mb)
WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
 
Taarifa ya Kawaida Na.14607

WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
SHERIA YA UTWAAJI ARDHI (SURA 118)
(Chini ya Fungu la 6)

Tangazo linatolewa kwamba Mheshimiwa Rais anakusudia kutwaa kwa manufaa ya umma ardhi ya ukubwa wa mita za mraba 233,000 zilizopo Manispaa ya Kinondoni na Ubungo Mkoa wa Dar es Salaam
na inayohusisha makazi ya watu katika makutano ya Barabara ya Bagamoyo na Kunduchi (Mbuyuni), Sam Nujoma na Chuo Kikuu cha
Ardhi Mkabala na Mlimani City na eneo linalomilikiwa na Manispaa
ya Ubungo lililopo Simu 2000 na Boko Basiaya.

Mtu yeyote anayedai kuwa na haki yoyote katika ardhi hiyo anatakiwa kutoa maelezo na uthibitisho wa haki hiyo kwa Mheshimiwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ndani ya majuma sita (6) kutoka tarehe ya tangazo hili kutolewa katika Gazeti la Serikali.

Inatangazwa pia kwamba kama Mheshimiwa Rais hakuagiza vinginevyo kuhusu siku ya kuingia katika ardhi hiyo, ananuia kuingia
katika ardhi hiyo yatakapoisha majuma sita (6) toka tarehe ya kutolewa kwa tangazo hili katika Gazeti la Serikali.

Mtu yeyote ambaye kwa hila au makusudi atamzuia mtu yeyote
ambaye amepewa madaraka ipasavyo kisheria kuingia katika ardhi hiyo atakuwa na makosa chini ya Sheria iliyotajwa hapo juu na atalazimika kulipa faini isiyozidi shilingi elfu tano (Shs. 5,000/=) au kufungwa kwa
muda usiozidi miaka miwili au vyote faini na kifungo.

Limetolewa Dodoma siku hii ya tarehe 06 Mwezi Novemba, 2024.

...........................................
Deogratius J. Ndejembi (Mb)
WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
Yakiisha hayo majuma sita ndio huwa inakuaje wanawavunjia baada ya Tasmini au, Nadhani ni mradi ule wa mwendokasi kwajili ya stendi na karakana
 
Kwan akichukua ana mipango gan? Si raia wanaishi tayari.
 
Back
Top Bottom