jd41
JF-Expert Member
- Aug 23, 2015
- 3,756
- 4,847
Ikiwa kila unapohudhuria mechi ya Simba SC pale uwanja wa Taifa lazima tupoteze, na wewe ukiwa ni mpenzi namba moja wa michezo nchini, hasa mpira wa miguu, nakuomba kwa heahima na taadhima siku nyingine Simba ikicheza tazama hiyo mevhi ikulu.
Ulianza kutazama mechi ya Simba dhidi ya Kagera Sugar tukapoteza, licha ya kuwa hatukuwahi kufungwa toka ligi ianze hapo kabla, ila siku uliyofika pale uwanjani tukapokea kipigo cha kwanza.
Leo tena tumefungwa na timu inayoongoza kwa kutoa sare, hii hali haieleweki. Nakuomba tu uwe unawasha TV hapo ikulu, ukae na familia yako, mfurahie mpira kuliko kwenda uwanjani kwenye makelele mengi, yanayoweza kukusababishia maumivu ya kichwa.
Na ukiwa na majukumu mazito ya kusogeza gurudumu la maendeleo ya nchi yetu mbele, nisingependa upate maumivu ya kichwa, kwasababu kichwa ndio halmashauri ya kila kiungo mwilini.
N.B: Leo ikiwa ni siku ya wanawake duniani, basi tuwaache wanawake washerehekee siku yao.
Sent using Jamii Forums mobile app