Rais Maguful na Spika Ndugai kama hamtaki kuahirishwa Bunge tumieni Video Conference!

Rais Maguful na Spika Ndugai kama hamtaki kuahirishwa Bunge tumieni Video Conference!

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2012
Posts
6,710
Reaction score
9,063
Leo Tena Bunge limepata msiba wa 3 ndani ya wiki mbili tu. Hii si hali ya kawaida tangu Tanzania ipate Uhuru kwa Bunge kupoteza Wabunge 3 kwa vifo vya kutatanisha.

Wabunge wa Upinzani CHADEMA na ACT-Wazalendo pamoja na Watanzania wenye busara walishauri Bunge lisifanyike kwasababu ya kuwepo kwa maambukizi ya Ugonjwa wa COVID-19.

Lakini Serikali ya CCM inayo jinasibu kwa kibri, ubabe na kutokuwa sikivu kwa mawazo kinzani ilipuuza ushauri huu.

Kwa vile sasa Spika Ndugai amejionea mwenyewe Wabunge wanavopukutika namshauri aombe msaada wa Tekeknolojia ya Mawasiliano ya Video Conferencing Bungeni kwa muda uliobaki kabla ya kuvunjwa kwa Bunge la Bajeti ifikapo Juni 30, 2020

Kama haiwezekani kwa Bunge kutumia teknolojia ya Video Conferencing basi ni bora Bunge lisitishwe na Wabunge wote wakae Quarantine ya 14 days.

Wasalaam.
 
Jukumu Lao ni kutulinda na wao kujilinda..
Kama vyote wameshindwa why wewe Una jali?
Waache waambukizane wamalizike labda Mungu anataka tupate 'wapya'wengi kabisa ..mambo yabadilike
 
CCM hawawezi kusitisha vibao vya bunge kwasabb wakifanya hivyo itaonekana wameshindwa kuhimili janga la Corona na kupelekea kupata aibu.....wakisitisha vikao Sisi wananchi tutajua moja Kwa moja kuwa vile vifo vya wabunge 3 vimetokana na Coronavirus

Hawa WAJINGA-WAJINGA wa kijani wataendelea kufa na Tai zao shingoni kwasabb ya kuogopa aibu
 
Wenzako wako busy kutafuta mafungu ya uchaguzi

Kwa Hali inavoelekea,mpaka Bunge likamalizike ni wachache sana watakao vuka kuingia kwene kinyang'anyiro Cha GE-2020!!!!Time gonna tell....!
 
CCM hawawezi kusitisha vibao vya bunge kwasabb wakifanya hivyo itaonekana wameshindwa kuhimili janga la Corona na kupelekea kupata aibu.....wakisitisha vikao Sisi wananchi tutajua moja Kwa moja kuwa vile vifo vya wabunge 3 vimetokana na Coronavirus

Hawa WAJINGA-WAJINGA wa kijani wataendelea kufa na Tai zao shingoni kwasabb ya kuogopa aibu

Kweli Hawa NZI WA KIJANI ni hatari sana kwa Afya zao na za WATANZANIA wote.....!
 
Back
Top Bottom