Rais Magufuli aamrisha wananchi kwenda kujisaidia nyumbani kwa mkurugenzi na DC Kibiti

Rais Magufuli aamrisha wananchi kwenda kujisaidia nyumbani kwa mkurugenzi na DC Kibiti

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887

Rais Magufuli leo akiwa njiani kutoka msibani, amesimama mara kadhaa kuwasalimu wananchi na kuwasikiliza. Ameshangazwa na watu walio chini yake kushindwa kujenga choo cha soko ilihali mapato ya halmashauri yao ni zaidi ya bilioni 1.8

Rais Magufuli ametoa agizo la choo husika kukamilika ndani ya siku saba la sivyo mkurugenzi aandike barua ya kuacha kazi. Pia ameagiza siku saba wakati choo kinajengwa wananchi waende kujisaidia nyumbani kwa DC pamoja na mkurugenzi ambae nyumba yake iko mtaa wa pili kutoka soko lilipo kwani nchi haiwezi kukosa choo wakati wanakusanya bilioni 1.8.

Amesema yuko 'very serious' na suala hilo hivyo mwananchi akibanwa afunguliwe. Amewaamirisha wawatayarishie maji ya kutosha lakini kama wana akili watajenga usiku na mchana.

Rais Magufuli amesema haiwezekani wakusanye bilioni moja kutoka kwa wananchi alafu washindwe kuwajengea choo hivyo amewataka wafanyibiashara sokoni hapo kutolipa ushuru kuanzia leo mpaka siku kitapojengwa choo.
 
Hah Hah siasa haihitaji hasira, ndiyo tatizo la kukosa mfumo kila kitu wateuliwa kama ma-RC, DC, DED hawajiamini kutoa maamuzi wanasubiri Mh. Rais atatue. Hili pia lipo ktk mhimili wa Bunge ambapo wabunge wa CCM wanashindwa kuiwajibisha serikali wanawaachia mawaziri watoe maswali na majibu kwa niaba ya wabunge wa CCM.

Uchaguzi wa Oktoba 28 , 2020 wagombea wa CCM watakuwa wapweke hakuna wa kuwabeba kutoka mhimili wa serikali kuu (dola) wala spika kuwalinda dhidi ya maamuzi magumu ya wananchi kuchagua wabunge kutoka upinzani wenye uwezo wa kusema kwa niaba ya wananchi na kuibana serikali ili iweze kuamka toka usingizini ipate kuwajibika.
 
Hah Hah siasa haihitaji hasira, ndiyo tatizo la kukosa mfumo kila kitu wateuliwa kama ma-RC, DC, DED hawajiamini kutoa maamuzi wanasubiri Mh. Rais atatue. Hili pia lipo ktk mhimili wa Bunge ambapo wabunge wa CCM wanashindwa kuiwajibisha serikali wanawaachia mawaziri watoe maswali na majibu kwa niaba ya wabunge wa CCM.

Uchaguzi wa Oktoba 28 , 2020 wagombea wa CCM watakuwa wapweke hakuna wa kuwabeba kutoka mhimili wa serikali kuu (dola) wala spika kuwalinda dhidi ya maamuzi magumu ya wananchi kuchagua wabunge kutoka upinzani wenye uwezo wa kusema kwa niaba ya wananchi na kuibna serikali kuwajibika.
Usimsingizie rais eti mfumo,choo?,acha masihara wamechemka tu,na kawaumbua
 
Back
Top Bottom