Rais Magufuli akamilisha uteuzi wa Baraza la Mawaziri, Makame Mbarawa abadilishiwa Wizara

BARAZA la Waislamu Tanzania (Bakwata) limemtaka Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (Necta), Dk Joyce Ndalichako kujiuzulu wadhifa huo akimtuhumu kuwafelisha mitihani ya dini ya Kiislamu wanafunzi wa kidato cha sita wa dini hiyo. Kauli hiyo ya Bakwata imetolewa na Mufti wa Tanzania, Sheikh Issa Bin Shaaban Simba katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Tanga jana kuelezea msimamo wa Waislamu nchini kuhusu matokeo ya kidato cha sita, hujuma inayoandaliwa kufanyika katika zoezi la sensa pamoja na vurugu zilizotokea Zanzibar.
Kuhusu hujuma ya mtihani, Mufti Simba alisema kuwa matokeo ya mtihani ya dini hiyo ya Kidato cha Sita yaliyotangazwa Mei Mosi 2012, yaliwashtua wanafunzi Waislamu waliofanya mtihani wa elimu ya dini ya kiislamu (Islamic Knowledge), ambayo yalionyesha kuwa asilimia 70 walifeli kwa kupata daraja F.
Alisema matokeo hayo yalionyesha kuwa ni asilimia 30 ndiyo waliofaulu kwa kupata daraja D, ambapo waliopata alama za juu kabisa nchi nzima ni wanafunzi saba pekee.?Matokeo haya yaliwashtua wanafunzi na wazazi, taasisi mbalimbali za kiislamu zilimua kukata rufaa kuonyesha kutokubaliana na matokeo hayo, hatimaye baraza hilo
likabaini kuwa lilikosea na likaidhinisha kutolewa matokeo
mapya,? alisema Mufti Simba.
Tayari Ndalichako ametoa ufafanuzi kuwa kosa lililotokea akisema si hujuma bali ni la kiufundi lililotokana na kubadili utaratibu wa kufanya mitihani mitatu ya somo hilo kuwa miwili, lakini mfumo wa ujumlishaji maksi ulisahaulika kubadilishwa.
Ndalichako alilieleza gazeti dada la Mwananchi, The Citizen, kuwa awali matokeo ya mitihani mitatu yalikuwa yanajumlishwa na kugawanywa kwa tatu kwa kutumia mfumo wa kompyuta, ili kupata alama rasmi za mtahiniwa, lakini safari hii zilipojumlishwa alama za mitihani miwili ya somo hilo ziliendelea kugawanywa kwa tatu badala ya mbili kimakosa.
Habari zilizopatikana kutoka Necta zimesema kuwa baada ya kupata malalamiko ya wanafunzi hao, uchunguzi ulifanyika na kubaini kasoro hiyo ambapo ilirekebishwa.Mei 30, mwaka huu Necta ilikutana na Baraza la Wakuu wa Shule za Kiisilamu na kufafanua suala hilo, ambapo ilionekana tatizo hilo si hujuma bali kosa la kiufundi.
Mwenyekiti wa Islamic Education Panel, Pilly H.H alimwandikia barua Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na nakala kwa Katibu Mtendaji wa Necta, Amir, Jumuia na Taasisi za Kiislamu Tanzania akishukuru wizara kwa hatua zilizochukuliwa.
?Tunashukuru kwa jinsi Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi ilivyopokea suala hili kwa uzito unaostahiki?Tunatoa shukurani za pekee kwa katibu mtendaji wa baraza la mitihani kwa hatua alizochukua ndani ya muda mfupi sana, nashukuru kwa ushirikiano,? ilisema barua hiyo iliyoandikwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wakuu wa Shule za Kiislamu.
Hata hivyo, akisistiza hoja yake Mufti Simba alisema kuwa matokeo yaliyotolewa upya yalionyesha kwamba wanafunzi zaidi ya asilimia 70 ya wanafunzi walifaulu, jambo ambalo Waislamu wanaamni kwamba ni hujuma inayolenga kupunguza idadi ya wanafunzi wa Kiislamu wa kujiunga na vyuo vikuu.
Mufti huyo alisema jambo lililomshangaza yeye pia pamoja na Waislamu wote nchini ni tamko lililotolewa na Ndalichako kupitia vyombo vya habari Jumanne iliyopita aliposema kuwa Baraza la Mitihani halikukosea kutoa matokeo hayo kwa kuwa waliosahihisha ni walimu wenye sifa.
?Bakwata inamshangaa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani, Ndalichako kwa kauli yake aliyoitoa kupitia vyombo vya habari juzi 5/6/2012 akisema hakuna hujuma na mitihani inasahihishwa na walimu wenye sifa na wanachaguliwa na wakuu wa shule zao,?alisema Mufti Simba.
Alisema hoja iliyotolewa na Ndalichako kwamba wanaosahihisha ni wenye uzoefu haina mashiko kwa sababu Waisalmu wanacholalamikia ni mfumo mzima wa ?Conveyor Belt?, aliodai umewekwa kuwahujumu wanafunzi
Waislamu.
Alisema matokeo hayo ya mtihani wa somo la kiislamu umeonyesha kuwa upo wasiwasi kwamba kilichofanyika huko ndicho wanachofanyiwa wanafunzi wa kiislamu katika masomo mengine kuanzia darasa la saba, kidato cha nne na hata vyuo vikuu kwa lengo la kupunguza idadi ya wasomi waislamu.
?Waislamu tunaamini kwamba hila kama hii inafanyika pia kwenye masomo mengine, kwa maana hiyo tunataka Ndalichako na watendaji wengine wajiuzulu ili kuondoa kashfa hii kwa Serikali, pia kuleta imani ya Waislamu kwa Serikali yao, ?alisema Mufti Simba.
Alifafanua kuwa baada ya kujiuzulu, Serikali iunde tume ya kuchunguza hujuma zilizotendeka katika baraza hilo dhidi ya Waislamu kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita akieleza kuwa Waislamu wanaamini kwamba wanafunzi wengi
wamefelishwa kwa kusudi maalumu la kuzorotesha kizazi chao.
Chanzo: Mwananchi
 
Kulalamika bila vivid evidences za kubaguliwa Kidini Siyo Kistaarabu Ndg zangu...
 
Hivi msahihishaji wa Mtihani wowote atamtambua vipi mtahiniwa anayesahihisha karatasi yake kwamba ni mkiristo ama ni muislam?Hawa akina Mufti hawajui watahiniwa hutumia Namba na wala sio jina? Kweli kuna viongozi hupenda kuleta mtafaruku kwa maksudi.
 
Naona mujahidini mmeanza chokochoko..tena shekhe Ponda kapata agenda ya kuanzia mwaka
 
Hivi huyo ndalichako amefanya nini alipokuwa baraza la mitihani?mitihani kilasiku ilikuwa inavuja na kuwafanya watoto wa wenye noti kupata mtihani kabla ya kuingia ndani ya chumba cha mitihani

Sifa kubwa ya Ndalichako pale Necta ni kudhibiti kuvuja kwa mitihani,hakukuwa na hayo mambo wakati wake
 
walimfojia mama wa watu wakamwondoa, kelele bila akili uwezi kuwezeshwa.
 
Hivi hao ni waislamu wa wapi!! Wanao mshtumu Dr Ndalichako? Wakati waislamu wanao jielewa wapo pamoja na Dr ??
 
Hivi Shekh simba bado yupo au kashapigwa chepe
 
Hawa watu wananiboa Sana. Wana udini mwingi kwenye taifa lenye upana kama Tanzania. Waislamu wamekaa kifujofujo tu. Sisi wakristo tunafundishwa upendo. Hawa sijawaelewa kwa kweli. Ndalichako kichwa kile
 
Tumpe nafasi waziri mpya wa elimu naona mambo yalifanyika kwenye awamu ileeee sasa hapa kazi tu akiboronga tena atapigwa chini tu hamna namna
 
Kulalamika bila vivid evidences za kubaguliwa Kidini Siyo Kistaarabu Ndg zangu...

unataka ushahidi gani zaidi ya huo aliotoa muanzisha mada, hata ukisikia waislamu hawakusoma mufti hawezi akazuka na uzushi wa level hiyo, tutaishi nae kwa mashaka.
 
Hawa watu wananiboa Sana. Wana udini mwingi kwenye taifa lenye upana kama Tanzania. Waislamu wamekaa kifujofujo tu. Sisi wakristo tunafundishwa upendo. Hawa sijawaelewa kwa kweli. Ndalichako kichwa kile
Lazima mseme hivyo maana JK kila alipoteua waislam mlimwita mdini pamoja wakristo kuwa wengi kwenye baraza lake lakini JPM kati ya mawaziri 34 waislmu 7 hiyo mnaona sawa.
 
Hivi Mh. Magufuli ungemteua Kilahama awe Waziri wa Mali asili na utalii usingetosha kusafisha majipu kweli? achana na suala la ukabila, angalia utendaji kazi. Hii namba hamjaitumia ipasavyo.
 
waote karibia poa hila huyu waziri mzigo sijui anaoogopa PHD yake isifie kijijini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…