Rais Magufuli akifanya mambo haya, Watanzania watamlilia wenyewe aongezewe muda wa kutawala

Mh Rais yeye mwenyewe kasema hataki kuongezewa muda na mbona twamlazimisha etii hata afanye nini muda wake ukiisha asepe
 
Iv president uwa anapitia hizi nyuzi kweli..... au anatakiwa kuzipata vipi?? Kuna nondo za kutosha sana humu
 
Kuna mtu juzi alianzisha uzi unaosema kuwa watanzania wanatamani magari ambayo hayapo duniani; lisinywe mafuta, likimbie, vipuri viwe vya bure etc wewe sasa unatamani kodi zipunguzwe ila wanaotafuta ajira wote waajiriwe! Unataka nyongeza ya mshahara wakati kodi zimefutwa! It’s impossible my friend
 
Umeandika Mambo mazuri Sana,lakini ukidhubutu kuivunja katiba ,utakuwa umeingiza ugonjwa mbaya,na wangine hata Kama watabolonga ,wataivunja ili waendelee kubaki on power.
 
A
Hayo yote uloyoyataja yanahitaji pesa. Sasa kwa kodi anazotegemea hizi hawezi kuyafanya.

Anachojua ni kukamua ngombe maziwa ila malishoni hawezi mpeleka.
 
Maajabu hayaishi. Yaani kwa uovu wote aliowafanyia watanzania, halafu eti waandamane kumtaka aendelee?

1) Kuua demokrasia ya uchaguzi, uhuru wa maoni na uhuru wa vyombo vya habari
2) Upendeleo wa wazi kwa kijiji chake. Kutumia rasilimali za nchi nzima kujengea miradi isiyo na tija kijijini kwake
3) Kufanya teuzi za upendeleo kwa kuteua watu wengi wa kanda yake kuongoza taasisi mbalimbali za serikali
4) Kuwatesa watu kwa kuwafunga kwa muda mrefu kisha kuwalazimisha wakubali kuwa wamehujumu uchumi
5) Kuua biashara kwa kuwabambikia kodi zisizolipika wafanyabiashara
6) Kuangusha ukuaji wa uwekezaji toka 28% mpaka 4%
7) Kuangusha ukuaji wa sekta ya utalii toka 15% mpaka 3.6%
8) Kuangusha thamani ya mauzo ya mazao ya kilimo kwa 50%
9) Kuharibu mazingira ya uwekezaji kiasi cha wawekezaji wengi kuhama nchi na kwenda mataifa jirani
10) Kuharibu mazingira ya uwekezaji sekta ya madini, mpaka kuifikisha Tanzania kwenye nafasi ya kwanza kuwa na mazingira mabaya Duniani
11) Kuendesha uongozi wa kilaghai na udanganyifu kama vile kuwadanganya wananchi kuwa Tanzania hakuna corona kumbe dhamira yake ni kutokuwa tayari kutumia rasilimali za Taifa kunusuru maisha ya wananchi
12) Kushindwa kufanya maandalizi ya mazingira ya kuwahudumia waathirika wa corona, na badala yake kupora pesa iliyotolewa na jamii ya kimataifa kwaajili ya kupambana na corona, na kupeleka kwenye maigizo ya uchaguzi , kisha kuwadanganya wananchi kuwa tumetumia pesa ya ndani kugharamia uchaguzi
13) Kuua ajira
14) Kutopandisha mishahara kwa wafanyakazi kwa miaka 6
15) Kutunga sheria gandamizi ili kuua uhuru wa watu wa kupashana habari
16) Kuanzisha kodi mbalimbali kuwakamua wananchi wa hali ya chini kama vile kodi za vocha, kodi za ufugaji kuku, kodi za visima vya maji, kodi za mashamba, kodi za mazao ya miti ya kupanda, kodi ya nyumba za vijijini, n.k.

Mimi naamini, kila mtanzania, hata yule mwenye akili ndogo kabisa, ukiwaacha wanafiki, huyu mtu hata aseme leo hii kuwa anaondoka, itakuwa ni sherehe kubwa kila kona ya nchi. Ameleta madhara zaidi kuliko faida.

Kitu kimoja kikubwa asichokijua, hakuna hata nchi moja iliyokuwa maskini halafu ilipata maendeleo kwa haraka kwa kuongeza uwingi na ukubwa wa kodi. Kadiri kodi zinavyokuwa nyingi na kubwa, ndivyo unavyoua uwekezaji, ndivyo unavyoua ajira, ndivyo unavyoua soko la bidhaa, ndivyo unavyoua teknolojia, na ndivyo unavyoua mwingiliano wa kisekta ambao husaidia sekta kuinuana.
 

Haya uliyoandika ni wajibu kwa rais yoyote, na sio majukumu ya ziada mpaka useme akifanya anastahili kuongezewa muda wa kukaa madarakani. Tunapaswa kila rais anayeingia madarakani atekeleze mambo haya maana sio hisani.
 
Mh Raisi akiyafanya hayo bila chuki wala roho mbaya Watanzania wenyewe wataamua na kumshinikiza kwa maandamano atawale ata milele hadi afie ikulu.
Haya ndiyo matatizo ya waTanzania hawa.

Unaacha mambo ya msingi unarukia peremende? Utamu wa peremende utakufikisha wapi?

Hayo yoooote uliyoyaorodhesha hapo kuwa ndio yatakayomfanya akubalike ni mambo ya kitaratibu, yasiyohusu uamzi wa mtu mmoja.

Mwambie aruhusu taratibu zilizopo zifanye kazi, mengi ya hayo utayapata; huhitaji kwenda kupiga magoti kwa yeyote.

Afuate katiba na sheria zake,...HAKI itapatikana kwa kila mmoja.

Angefanya hivyo toka mwanzo, hata sehemu ambazo zingekuwa ngumu kuzitekeleza kwa kukosa uwezo, watu wangeelewa na wasingemlaumu yeye binafsi.

Mada yako ni ya kulambisha watu sukari. Utamu unakwisha, unarudi palepale pa mwanzo.
 
11) Kuendesha uongozi wa kilaghai na udanganyifu kama vile kuwadanganya wananchi kuwa Tanzania hakuna corona kumbe dhamira yake ni kutokuwa tayari kutumia rasilimali za Taifa kunusuru maisha ya wananchi
Umeandika mambo mazito sana.

Na sasa maono yenye umuhimu kwake ni kufundisha historia, wala hawazii sayansi na teknologia! Tunarudi nyuma huku wenzetu wakienda mbio mbele. Tumepoteza sana, na tutajutia.

Great Thinker.
 
Hakika
 
Wapi nmesema kod zfutwe?? Kodi za sasa n kandamizi mpk biashara znafungwa. La ajabu n lipi wakt mara kibao anatwambia nchii hii ni tajiir, tuutumie utajiri wetu kufanya hayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…