johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Mwalimu Nyerere kama kiongozi alikuwa na ndoto zake na miongoni mwa ndoto hizo ni pamoja na Kuhamishia makao makuu ya serikali Dodoma, pili kumiliki njia kuu za uchumi na tatu kuwa na bwawa kubwa la kuzalisha umeme Stieglers Gorge.
Katika uongozi wake kama Rais, Dr Magufuli ameweza kuhamishia makao makuu ya serikali kwenda Dodoma.
Pili amefanikisha ujenzi wa bwawa la Stieglers Gorge ambapo mkandarasi ameshapatikana na mkataba umesainiwa.
Tatu, Rais Magufuli ameshaanza kuhakikisha serikali inakuwa na umiliki katika njia kuu za uchumi, amefufua ATCL, TRC inaimarishwa na taasisi nyingine za miundombinu zinaimarishwa na hii ndio ndoto ambayo Nyerere aliifanikisha lakini mabeberu wakaitibua kwa kugawana mashirika yetu karibia yote.
Nina imani Rais Magufuli ataikamilisha ndoto hii ya mwalimu Nyerere.
Naomba niishie hapo!