kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Tanzania ilipata Uhuru kutoka kwa mkoloni miaka karibu miaka 60 iliyopita. Miaka 60 Ni mingi sana, inatosha kwa wananchi wote kupatiwa maji, umeme, viwanda, hospitali, shule, mabwawa ya umeme na umwagiliaji, reli, barabara kutokana na wingi wa rasilimali zilizoko nchini.
Kwa miaka 60 CCM haikuwapa wananchi maji na sasa wanataka wasifiwe kwa kuwapelekea wananchi maji leo, hawakupeleka umeme na sasa wanataka wasifiwe kwa kupeleka umeme, waliua viwanda sasa wanataka wasifiwe kwa kufufua viwanda, waliua reli sasa wanataka tuwasifu kwa kufufua reli, kwa miaka 60 hawakujenga shule za kutosha sasa wanataka tuwasifu kwa kujenga shule, walianzisha ulaji rushwa sasa wanataka sisi tuwasifu kwa kuuondia rushwa. Hivi ni vitu ambavyo vilikuwa vifanywe na CCM miaka 60 iliyopita ya Uhuru.
Jitihada anazozionyesha leo mh. Rais ni namna tu ya kujaribu kuifutia dhambi CCM. Wana CCM ndio wanaopaswa kumsifu sana kwa kuwafutia dhambi zao kwa wananchi kuliko wananchi wa kawaida.
Natamani mh. Rais angekuwa mgombea kupitia vyama vya upinzani kuliko CCM kwasababu wananchi wanaiona CCM kama chanzo cha shida zote zinazowakabili ambazo Rais JPM anakabiliana nazo leo. Hata angefanya Nini wapinzani wa CCM watakuwepo tu palepale. Ni Heri angetumia chama kingine.