Rais Magufuli aongoza kikao cha kwanza cha Baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dodoma, Rais Mwinyi aapishwa kuwa Mjumbe wa Baraza

Rais Magufuli aongoza kikao cha kwanza cha Baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dodoma, Rais Mwinyi aapishwa kuwa Mjumbe wa Baraza

mwanamwana

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
1,309
Reaction score
4,798
Rais wa Tanzania, John Magufuli leo Jumatano ataongoza kikao cha kwanza cha Baraza la Mawaziri jijini Dodoma. Matangazo ya moja kwa moja ya kikao hicho yatarushwa kuanzia saa 4:00 asubuhi.

Historia itawekwa leo ikiwa ni mara ya kwanza kikao cha Baraza la Mawaziri kurushwa mbashara kwenye TV na Redio mbalimbali nchini.

=========

Kikao cha baraza kinaanza kwa kiapo cha Dkt. Mwinyi kama Mjumbe wa Baraza la Mawaziri mbele ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa. Ibrahim Juma na kuwa mjumbe Rasmi wa Baraza la Mawaziri.

Mwinyi.jpg

Jaji Mkuu Profesa Juma akimwapisha Dkt. Mwinyi kuwa Mjumbe wa Baraza la Mawaziri

Rais Magufuli anampongeza kwa kuapa na kumkaribisha kwenye kikao, Rais Magufuli anawakaribisha wajumbe wote na kuwapongeza kuwa wajumbe wa Baraza la Mawaziri.
1.jpg


 
Rais Magufuli leo anaongoza kikao cha kwanza cha Baraza la Mawaziri baada ya uchaguzi mkuu wa 2020.

Tukio liko mubashara TBC, Channel ten na ITV

Updates;

Viongozi wote wameshaketi ukumbini akiwemo makamu wa Rais mama Samia, Rais wa Zanzibar, Dkt. Mwinyi na Waziri mkuu mh Majaliwa.
 
Mazungumzo ya vikao vya Baraza la Mawaziri hupaswa kuwa siri.
Kwa mujibu wa kiapo cha mawaziri kinasema "Sitotoa siri za baraza la mawaziri isipokuwa kwa idhini ya Mh Rais" Hivo basi, endapo Mh Rais atalidhia lolote katika kikao cha baraza liwe wazi bas litatolewa public.
 
Vipi Mwinyi akishindwa kubugia kiapo kama yule N/W wa madini
 
Rais Magufuli leo ameshuhudia Rais wa Zanzibar Dr Hussein Mwinyi akila kiapo kuwa mjumbe wa Baraza la mawaziri mbele ya Jaji mkuu Prof Juma.

Hili ni takwa la kikatiba linalomtaka Rais wa Zanzibar kula kiapo kabla ya kuanza kuhudhuria vikao vya baraza.

Source ITV.
 
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania
Anatufanyizia Kazi
Nasema Uongo Ndugu Zangu
 
Seif ni Makamo wa SMZ Watanganyika mnaumia sana WAZANZIBAR wakiungana hivi shida yenu ni nini??
Nani ana shida mkoa ukiungana? Tatizo ni pale unapopata mimba ya kubakwa kisha ukimzaa mtoto useme watu wanakuonea wivu kwa mwanaume uliyeridhika naye!
 
Back
Top Bottom