Rais Magufuli apiga marufuku wapiga debe kwenye stendi ya Dodoma. Ataka wafanyabiashara wasisumbuliwe

Rais Magufuli apiga marufuku wapiga debe kwenye stendi ya Dodoma. Ataka wafanyabiashara wasisumbuliwe

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
RAIS Dk. John Magufuli, ametoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi, kuhusu stendi kuu ya mabasi iliyopo jijini humo ikiwemo kuhakikisha wajasiriamali wadogo, waendesha bodaboda na daladala kutosumbuliwa.
magu%20simm.jpg

Rais Dk. John Magufuli.
Magufuli ametoa maagizo hayo leo kwa njia ya simu baada ya kuona na kusikia malalamiko ya wafanyabiashara waliopo katika stendi hiyo na kumtaka Mkurugenzi wa Jiji hilo kwenda kuwasikiliza na kutatua malalamiko hayo, huku akiwataka Askari wa Suma JKT kuacha tabia ya kurukisha watu vichura kwani hayupo tayari kuona wananchi wake wanateseka

Hata hivyo Magufuli ametoa pongezi kwa wadau wa stendi hiyo kwa kuzungumza mambo ya msingi ambayo na yeye amekubaliana nayo ikiwa ni pamoja na kuruhusu watu kufanya biashara katika stendi hiyo, huku akiongeza kuwa stendi hiyo haikujengwa kwa ajili ya matajiri bali ni kwa ajili ya watu wote.

"Mtu anatoka kijijini kule, watani zangu Wagogo ametoka kule amekuja kwenye basi halafu anateremka pale unamlazimisha akale chakula cha shilingi 5000 , kwa hiyo mama lishe lazima wawepo kwa ajili ya kuuza chakula cha shilingi 500 badala ya shilingi 5000, haya ndio maisha yetu watanzania lakini ieleweke hiyo stendi haikujengwa kwa ajili ya watu matajiri, stendi nimeijenga kwa ajili ya watu wote wakiwemo masikini"

"Watanzania wote wa maisha yote wa viwango vyote washiriki kujitafutia riziki katika maeneo hayo , kwa hiyo nitafurahi siku moja mtu anayeuza juisi, karanga, anampa mtu aliyekuwa kwenye basi lakini kuteremka kila mmoja utaenda kuzinunua zabibu za kwenye mahoteli ya shilingi 6000" amesema Rais Magufuli.

Pamoja na hayo, Rais Mgufuli hakuweza kukubaliana na suala la uwepo kwa wapiga debe katika stendi hiyo kwa madai ya kuwa hao wapiga debe wakati mwingine wanageuka na kuwa wezi.

“Wapiga debe ndio wakati mwingine wanageuka kuwa majizi na kurubuni watu, wale hapana, kwenda pale na kuanza kupiga debe sio kitu kizuri ,kwanini mtu apige debe,akapige debe la nyumbani kwake. Kupiga debe pale hiyo sio njia ajira nzuri,ajira nzuri ni watu kwenda kufanyabiashara kwa kuuza zabibu, karanga huo ndio ujasiriamali.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji hilo, Godwin Kunambi amesema amepokea maelekezo yote ya Rais Magufuli na anakwenda kuyafanyia kazi kwa haraka sana.
 
Ni sawa,watu wote wanatakiwa kufaidika na hiyo fursa...
 
Wapiga debe hawatakiwi stendi zote au Dodoma tu?

Kama hii ni kwa Dodoma peke yake hadi rais atoe maagizo kwa stendi zote nchini mbona hiyo itakuwa ni kwa awamu 20?
 
Hahah lkn maisha ya wafanyakazi wa umma na wastaafu wala hana habari nayo.

Mama ntilie,Bodaboda,Machinga huu ndio muda wenu(Kampeni) wa kula maisha then baada ya uchaguzi mjiandae kwa mtiti mzito kama kawa.
 
Visawe vya maneno
Wapigadebe, Masarange, nyoka, wavunja mabawa = wana nguvu kuliko Wamiliki wa magari
Matajiri, mabeberu, makaburu, wahisani = hawawezi kuiona pepo
Wanyonge, masikini, wachumia tumbo, wavuja jasho, macomrade = wapiga kura
 
Miaka mitano umefanya kampeni ,bungeni kampeni,ikulu kampeni yaani
 
Back
Top Bottom