Rais Magufuli aubadilisha jina uwanja wa Taifa, Rasmi kuitwa "Mkapa stadium"

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
21,711
Reaction score
35,644
Rais Magufuli amesema "Mzee Mkapa aliujenga uwanja mkubwa wa michezo. Wengi wanataka uitwe Mkapa Stadium. Alikuwa hapendi vitu viitwe kwa jina lake, lakini hawezi kuniadhibu amelala. Natamka rasmi uitwe Mkapa Stadium'

 
Huu uwanja mpya tangu zamani ulikuwa ukifahamika kwa jina la Benjamin Mkapa Stadium, kwa wale watu wanaotumia DSTV watakuwa wanafahamu nazungumza nini.

Mechi zote zilizokuwa zikichezwa hapo zilikuwa zikiandikwa LIVE from Benjamin Mkapa Stadium, Dar es Salaam, Tanzania.

Tusitafute sifa ktk msiba wa mtu.

Sent from my SM-G930F using JamiiForums mobile app
 
Rip mzee Mkapa hakupenda vitu viitwe kwa jina na hata mapenzi yake kwa timu ya wananchi ya Yanga hakuyaweka hadharani.

Ombi la muda mrefu tangu pale uwanja ulipokamilika la kutaka uwanja huo mpya "kwa mchina" uitwe Mkapa National Stadium, limekubaliwa na Rais Magufuli.

Yanga hoyeeee..........Simba hoyeeee....... Azam hoyeeee......!

Maendeleo hayana vyama!
 
Halikuwa rasmi..lakini kwa sasa hata hati take itabadilishwa na kuwa ya "Mkapa National Stadium" badala ya "Tanzania National main Stadium".
 
Halikuwa rasmi lakini kwa sasa hata hati take itabadilishwa na kuwa ya "Mkapa National Stadium" badala ya "Tanzania national main stadium".
 
Toka long watu walisema kwa mkapa utoki maana utafungwa ukienda huko
 
Hivi nani aliondoa neno MTUKUFU kwenye kumtaja rais..!?
 
Ila jina "Kwa mchina" limekaa poa sana!
 
Sasa badala ya kuuita "Uwanja wa Mkapa" nyie mnaleta uzungu tena wa "Mkapa stadium"!

Ivi waafrika tutaendelea kuwa watumwa wa fikra Hadi lini?.
Na wewe kwaNini unakuwa mtumwa wa majina ya kizungu? Kwanini usijiite Mwakifumu au Bashite?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…