Rais Magufuli awashangaa Wazaramo Jokate kutokuolewa

Rais Magufuli awashangaa Wazaramo Jokate kutokuolewa

Mzukulu

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2020
Posts
1,401
Reaction score
2,641
Je, huu ni Utani wa kweli wa Kimakabila yetu nchini Tanzania au ni Utani wa Kutamani kweli huku Ukitega kuangalia anayetaka Kukuzidi Kete kwa Mrembo?

" Hata Mkuu wa Wilaya wa hapa amefanya kazi nzuri katika kuondoa Zero, ninachowashangaa watani zangu Wazaramo hajaolewa, lakini mnashindwa kumuoa mnamuangalia tu, ndiyo shida ya Wazaramo saa zingine mnashindwa mambo " -Rais @MagufuliJP

Mzukulu nasema ogopa sana Mwanamke wako akimpata anayemkuna zaidi yako lazima ataanza Kukudharau na Utawachukia Watu wote tu jirani.

====

Magufuli awashangaa Wazaramo Jokate kutokuolewa

JUMAPILI , 28TH JUN , 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, amewashangaa watani zake Wazaramo kwa kushindwa kumuoa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo ili hali hana Mume.

WEB%20MAGU%20NA%20JOKATE.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo.
Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Juni 28, 2020, alipokuwa akiwahutubiwa wananchi wa Kisarawe mara baada ya kuzinfua mradi wa maji wa Kibamba hadi Kisarawe uliogharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 10.6.

"Hata mkuu wa Wilaya wa hapa amefanya kazi nzuri katika kuondoa Zero , hapa kulikuwa na Zero nyingi sana, ninachowashangaa watani zangu Wazaramo hajaolewa, lakini mmeshindwa kumuoa mnamuangalia tu, ndiyo shida ya wazaramo saa zingine mnashindwa mambo" amesema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli amempongeza Waziri wa TAMISEMI Selemani Jafo kwa utendaji wake wa kazi, "Nimpongeze Jafo kwa kunisaidia kazi, kijana huyu anajituma sana, mwembamba kwa umbo lakini mambo yake makubwa anazunguka kila mahali, sijasema Mawaziri wengine hawafanyi kazi lakini nipo kwenye jimbo la Kisarawe".
 
Mpaka juzi Kati ilibidi mheshimiwa rais ampe jokate shout out, kwa kuuliza wananchi wake, mbona wanaume wa kisarawe hawamuoi jokate?

Jokate ni mrembo, ni maarufu, halafu ana class flani hivi..au wanaume anaokutana nao wanamuogopa? Ina maana Tanzania nzima, kweli..hakuna mwanaume wa kumuoa jokate, nahisi jokate sahiv ana miaka 30 (though sina uhakika)
 
Naona DAS mtumbuliwa umekuja kwa gia ya reverse...
 
Wengine hatujavutiwa naye bado kila mtu anachakuvutiwa na mwanamke anayempenda sio wote wanavutiwa naye.
 
32
Mpaka juzi Kati ilibidi mheshimiwa rais ampe jokate shout out, kwa kuuliza wananchi wake, mbona wanaume wa kisarawe hawamuoi jokate?

Jokate ni mrembo, ni maarufu, halafu ana class flani hivi..au wanaume anaokutana nao wanamuogopa? Ina maana Tanzania nzima, kweli..hakuna mwanaume wa kumuoa jokate, nahisi jokate sahiv ana miaka 30 (though sina uhakika)
Nadhani kafikisha au 33
 
Jojo high maintenance...level yake kwa sasa labda mabachelor wabunge
 
Tembo wanavutia mno wakiwa porini, sasa wafuge uone!
 
Hizi post nazo Mh. Rais akiziona atashangaa jinsi gani mambo ya kawaida yanawachanganya wananchi wake.
Kwa kifupi Wazaramo wajipange wakatoe posa..ngoja wachelewe waone..
 
Back
Top Bottom