Rais Magufuli, Dangote, Obama kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Kenyatta

Rais Magufuli, Dangote, Obama kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Kenyatta

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
Magufuli.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt John Magufuli na Rais mstaafu wa Marekani, Barack Obama ni miongoni mwa viongozi wanaotarajiwa kuhudhuria katika sherehe za uapisho wa Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta.

Kamati ya maandalizi ya sherehe hizo inayoongozwa na Katibu Kiongozi, Joseph Kinyua imebainisha kuwa imeandaa orodha ya majina ya viongozi wa kimataifa kwa ajili ya kushuhudia tukio hilo la kihistoria la uapisho wa Kenyatta endapo ushindi wa Kenyatta hautopingwa mahakamani.

Kwa mujibu wa Katiba ya nchi hiyo, sherehe za uapisho hufanyika siku 14, baada ya mshindi wa uchaguzi kutangazwa ili kutoa fursa kwa chama chochote kinachotaka kupinga matokeo kufanya hivyo.

Viongozi wengine wanaotarajiwa kualikwa katika sherehe hizo wakiwemo wakuu wa nchi ni pamoja na Rais wa Rwanda Paul Kagame, Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma na Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari. Wengine ni Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May.

Aidha, katika orodha hiyo pia yupo Rais wa Liberia, Ellen Johnson Sirleaf, mfanyabiashara tajiri namba moja Afrika Aliko Dangote, Kiongozi wa Jumuiya ya Ismailia, Aga Khan, Waziri Mkuu mstaafu wa Italia, Matteo Renzi na Rais Xi Jinping wa China.

“Tupo kwenye maandalizi ya sherehe za uapisho wa Rais wakati tukisubiria hatua za kikatiba kukamilika. Orodha hii ni ya marafiki wa Kenyatta, viongozi wa Afrika na viongozi wengine wa kimataifa, tunaotarajia kuwaalika”, amesema mmoja wa wanakamati hiyo ya maandalizi.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Mipaka na Uchaguzi Kenya, Wafula Chebukati mwishoni mwa wiki alimtangaza rasmi Rais Kenyatta na Naibu wake, William Ruto kuwa washindi katika uchaguzi uliofanyika wiki iliyopita nchini humo

Chanzo: Mpekuzi
 
Sasa mbona nimesikia Odinga hatahudhuria?
Itakuwaje sasa au tutapitia kisumu?
Mimi nipo najitayarisha kwa safari....hureee!!
 
lol! is this a joke? sidhani kama hao marais watahudhuria....Xi Jinping alikosa kuhudhuria uzinduzi wa reli sasa atakuja kuhudhuria hii? Merkel wa Ujerumani, Matteo wa Italia, Obama na Theresa May hawana muda wa kuhudhuria upuuzi...

naiita upuuzi kwani nchi zile ukitazama wanavofanya uchaguzi, utatambua kuwa bado tuko mbali sana...kisha kuna security threats nyingi mno hapa Kenya.

they would have to bring secret service na afisa wengi..that would cost their countries a lot of money and cost Kenya too alot of money to host the ppl..sioni hata mmoja akikubali mwaliko huu....pengine Kagame, Magufuli, Farmajo na Museveni.

Buhari kumbuka ni mgonjwa...Zuma naye ana changamoto tele zamkabili kule chini...that list is crazy! finally, Kenya is not a global power...not even close
 
lol! is this a joke? sidhani kama hao marais watahudhuria....Xi Jinping alikosa kuhudhuria uzinduzi wa reli sasa atakuja kuhudhuria hii? Merkel wa Ujerumani, Matteo wa Italia, Obama na Theresa May hawana muda wa kuhudhuria upuuzi...naiita upuuzi kwani nchi zile ukitazama wanavofanya uchaguzi, utatambua kuwa bado tuko mbali sana...kisha kuna security threats nyingi mno hapa Kenya...they would have to bring secret service na afisa wengi..that would cost their countries a lot of money and cost Kenya too alot of money to host the ppl..sioni hata mmoja akikubali mwaliko huu....pengine Kagame, Magufuli, Farmajo na Museveni.....Buhari kumbuka ni mgonjwa...Zuma naye ana changamoto tele zamkabili kule chini...that list is crazy! finally, Kenya is not a global power...not even close
Yup ,you're right hii list inasoma kama "fake news" kabisa.Niliona Angela Merkel,Xi Jinping na Theresa May kwa hio list na hapo ndio my doubts machine went beyond gauge.Tuko na slums aplenty,hawkers ndio tele na watu wengi bila maji safi lets focus on that before even dreamin of unfounded global influence.
 
Mleta mada jaribu kuwa Mkweli..

Hiyo ni list ya waalikwa..

Na ukialikwa sio lazima uhudhurie, unaweza hata kutuma mwakilishi

Wapi wametoa udhibitisho kwamba JPM, Obama, Dangote na hao wengine kwamba watahudhuria..??!

Akili nyingine bwana.
 
lol! is this a joke? sidhani kama hao marais watahudhuria....Xi Jinping alikosa kuhudhuria uzinduzi wa reli sasa atakuja kuhudhuria hii? Merkel wa Ujerumani, Matteo wa Italia, Obama na Theresa May hawana muda wa kuhudhuria upuuzi...

naiita upuuzi kwani nchi zile ukitazama wanavofanya uchaguzi, utatambua kuwa bado tuko mbali sana...kisha kuna security threats nyingi mno hapa Kenya.

they would have to bring secret service na afisa wengi..that would cost their countries a lot of money and cost Kenya too alot of money to host the ppl..sioni hata mmoja akikubali mwaliko huu....pengine Kagame, Magufuli, Farmajo na Museveni.

Buhari kumbuka ni mgonjwa...Zuma naye ana changamoto tele zamkabili kule chini...that list is crazy! finally, Kenya is not a global power...not even close
Jay siku hizi unaona mbali! Kudoz to your lecturers! They're doing quite a nice job to shape u!

btw, kumwalika mtu na kuhudhuria ni vitu viwili tofauti!, wanaweza wasihudhulie ila wakawatuma mabalozi wao hapo Kenya! Naamini wengi watafanya hivyo ukiondoa Obama ambaye hana hyo mandate tena!
 
Back
Top Bottom