Uchaguzi 2020 Rais Magufuli fanya yafuatayo uridhishe Watanzania vijana ili kuinusuru CCM

Uchaguzi 2020 Rais Magufuli fanya yafuatayo uridhishe Watanzania vijana ili kuinusuru CCM

Riz king

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2018
Posts
276
Reaction score
549
Ndugu wana jamvi,

Mimi ni mwana CCM tena kindakindaki. Nayaona yafuatayo ndo yatatupa ugumu katika hizi chaguzi na tusipoyaona tutaondolewa madarakani ndani ya chaguzi mbili zjazo.

1. Vijana kukosa Ajira
Hili tatizo vijana vengi wahitimu wamekuwa hawana tumaini tena kwani tangu umeingia madarakani ajira zimekuwa kaa la moto huku mawaziri wako wakikejeli vijana kujiajiri huko majukwaani wakati wao wanahangaika na teuzi kwa vile walishakusoma dira yako kuwa ukisifiwa na ukasapotiwa bila kukosolewa ndo huwa furaha yako.

2. Mikopo vyuoni
Hili nalo limekuwa tatizo maana vijana wengi wamekuwa wakiacha kabisa masomo na wametokea familia masikini kabisa huku vigezo vya kuupata huo mkopo mkizidi kuvibana. Hili mh jaribu kulirekebisha maana nasikia imefikia hatua yanaandikwa majina ya UVCCM vyuoni ili wakapate mkopo. Mimi sidhani kama huwa ndo maelekezo yako ila wateule wako wanafanya mambo ya hovyo bila wewe kujua wakiamini wanakujenga.

3. Huduma za afya
Sawa vimehengwa vituo vingi vya afya ila angalia uongeze watumishi maana hawakidhi kwa namba ya idadi ili watanzania watibiwe kwa weredi na hapo pia rudisha huduma za bure kwa wazee na waathirika wa HIV maana siku hizi wazee kama hawana bima ya CHF analipia matibabu huku wale wenye HIV nae hulipia kama akiugua hata maradhi nyemelezi.

4. Elimu bure lakini bado kuna vitu huvihudumii
Hilo Mh linaleta doa sana maana kiukweli michango haijaisha mashuleni Mara utasikia ya kulipia walimu wa sayansi wanaojitolea Mara vile yaani angalia sana kasoro hizo ili urekebishe kusiwepo na kasoro la sivyo urudishe ushirikishaji wa kuichangia elimu ili serikali itop up pale penye upungufu.

Me yangu ni hayo mh Rais huku wana CCM tushaanza kuzomewa mpaka na bodaboda mitaani na nashauri haya ili tusipate wakati mgumu kama ule 2015. Hao wateule wako waangalie kwa jicho la ukali zile sifa za hovyo wanazokupa ni kutaka teuzi wala hawana upendo na wewe. Mambo ya kukusifia sijui SGR mara Flyover mara bwawa la umeme. we yaangalie pia usijisahau Yale unayoyaona yatawapa watanzania furaha kwa kugusa nyoyo zao.
 
Pesa za mafao hazipo. NSSF Wala PSSF. Watu hawalipwi.

Kuna wasi wasi kuwa Pesa zimechotwa.

Wafanyakazi ndio wanaoumizwa vibaya na hii Serikali
 
So unataka afanye nini labda aendekee tu kutapatapa lakin lazma atambue kuwa hawezi kukuepuka kifo
 
Mmeshachelewa na hata akifanya hayo hiyo itakua rushwa yaani nimesota kitaa mppaka sasa mwaka wa tano hata akitoa ajira bado tutawachinjia shingoni kama mbuzi wa kafara fungeni virago hamuna muda tena kutudanganya saiz majuukwani mtatudanganya lipi tena ?
 
Kimsingi mimi nadiriki kusema awamu ya tano imefanya mambo makubwa mengi kulingana na Ilani ya uchaguzi kwa asilimia 80 ila changamoto zilizopo ni sehemu ya mchakato wa maendeleo. Haikwepeki hata nchi zilizoendelea bado zina changamoto zake ikiwemo ajira as a global challenge. Tumpe mitano tena ayashughulikie kuliko kuanza na mtu mpya. Waswahili husema bora shetani unayemfahamu kuliko....
 
Back
Top Bottom