Rais Magufuli hasemi ukweli kuhusu wazee Tanzania

Rais Magufuli hasemi ukweli kuhusu wazee Tanzania

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2012
Posts
6,710
Reaction score
9,063
Jana tarehe 01 Oktoba ilikuwa ni Siku ya Wazee duniani. Tumemsikia Magufuli kwenye Kampeni akiwalaghai Wazee na watanzania kwa ujumla wao ati Serikali yake ya CCM inawajali Wazee na inawalinda kwa nguvu zote!

Huo ni urongo na Unafiki mkubwa na pengine ni lugha tu ya kuombea kura!

Kuna matatizo lukuki ya Wazee wa nchi hii na hayajapatiwa ufumbuzi na yameongezeka sana katika kipindi cha utawala wa Magufuli:
  1. Wazee wanastaafu KULIPWA pensheni inachukua mwaka mpaka miaka 3 na kuna wengine wamepoteza maisha kwa kucheleweshewa mafao yao.
  2. Bado wazee wananyanyaswa kupatiwa matibabu ya bure mpaka wawe na Bima ya Afya.
  3. Bado Wazee wanalazimishwa na TRA kulipa kodi za majengo na Viwanja ilhali kuna msamaha hewa.
  4. Wazee wasio na makazi rasmi wanatangatanga mitaani na kuwa ombaomba ilhali kuna Sera ya kutunza Wazee kwenye makazi maalumu.
Kwa ujumla wazee wa nchi hii wanaonekana hawana thamani baada ya kulitumikia Taifa kwa weledi mkubwa. CCM ni adui nambari moja wa Wazee wa nji hii.

Ufumbuzi wa hili ni kumwambia Magufuli apishe Ikulu waingie wengine wenye Utashi wa kuwalinda, kuwatetea na kuwapigania wazee wa nji.

Hivi Kama Makundi ya vijana, Wanawake na Walemavu Wana UWAKILISHI BUNGENI Kwanini kundi la Wazee halina uwakilishi Bungeni? Huu ni ubaguzi wa hovyo kabisa.
 
Back
Top Bottom