Uchaguzi 2020 Rais Magufuli huoni kama jitihada zako za kuimarisha miundo mbinu jijini Dar es Salaam inafeli?

Uchaguzi 2020 Rais Magufuli huoni kama jitihada zako za kuimarisha miundo mbinu jijini Dar es Salaam inafeli?

Maneno Meier

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2013
Posts
2,467
Reaction score
1,697
Ni kitu cha kufurahia na kushukuru sana kuona jinsi gani Rais unavyo jitahidi kuliweka jiji letu kuwa mobile kwa jitihada zako kubwa za kimkakati unazozifanya za kudumisha na kuimarisha miundombinu ya usafiri jijini Dar es Salaam kwa kujenga mbarabara, madaraja na Flyovers. Imekuwa ni faraja kubwa sana kwetu.

Lakini katika dhamira hiyo pana na muhimu kwa mobility ya wakazi wa Dar es salaam inaonekana kuwa watendaji wako bado hawana uelewa mpana wa jinsi gani hali hiyo inayo onekana ngumu, inavyo weza kukabiliwa kiufasaha na kirahisi zaidi.

Watu ambao wana maarifa mapana wamesha shauri mara nyingi sana kuwa uenezaji wa miundombinu yetu ya usafiri unatakiwa uende sambamba na miundo mbinu ya sewage systems.

Ni ujinga wa hali ya juu kudhani kuwa utengenezaji wa barabara nzuri za lami ambazo magari yanaweza kupita ndiyo kutoa jawabu sahii la kuondoa matatizo ya usafiri jijini, bila kuweka miundo mbinu thabiti ya kukabiliana na swala la maji taka, huko ni kujidanganya sisi wenyewe.

Mimi mda wote najiulizwa sana, hivi Rais wetu unazungukwa na watu wa aina gani haswa ambao hawana hata chembe za kuwaza mambo yanayoweza solve problems zetu za miundo mbinu ya maji taka?

Rais Magufuli nasikitika kukuambia kuwa Waziri wetu wa wizara nyeti ya Ujenzi Mh. Waziri Engineer Kamwelwe na maengineer wanzake wengine kwenye hiyo wizara hawawezi kazi. Na ninakuomba kama utapata tena ridhaa ya kuongoza hii nchi, basi hawa watu kusema kweli waondoe mara moja kwenye nafasi zao ili wawaachie kazi vijana wengine ambao wako serious na kazi zao za kutatua matatizo haya ambayo jiji letu la Dar es salaam linakabiliana nayo ya mafuriko yanayo tokea mara kwa mara jijini.

Haiwezekani nchi yenye watu wenye degree ya civil Engineering kem kem kama Tanzania kuwa na matatizo ya mafuriko kama haya ya juzi tarehe 13 jijini kila mara na hakuna engineer hata mmoja ambaye yuko tayari kutoa mchango wake kwenye kutatua hilo tatizo. Kuna nini kwani kwenye hii sector?

Rais Magufuli najua unapenda sana kuona vitu vizuri vinavyo pendeza machoni, lakini ukweli wa mambo unashindwa kuwaweka watu ambao wana uwezo mkubwa wa kufikiri na kutatua matatizo ya vitu muhimu ambavyo vitasababisha hivyo vitu vizuri unavyo penda kuviona kwa macho, viendelee kudumu.

Haingii akilini kuona serikali inatumia mabilioni na mabilioni ya fedha za walipa kodi kila mwaka kugharimia unjenzi wa barabara na madaraja ambayo hayadumu na hivyo hivyo kuitia hasara kubwa nchi yetu, alafu hao watu wanao sababisha hayo matatizo waendee tu kula hela za bure za walipa kodi, hiki ni kitu ambacho hakiwezi kukubalika.

Hapa Rais Magufuli lazima hiyo wizara uifanyie reformation, ukiingia tena madarakani. Hatuwezi tukaendelea kuwa na wizara yenye watu hopeless namna hiyo kama hawa maengineer wetu huko wizarani. Huko ni ku-jeopardize sisi wenyewe, wakati jawabu la kutatua tatizo hilo linajulikana, nalo ni Sewage system.

Rais Magufuli kama wananchi watakupa tena ridhaa ya kuongoza nchi nakuomba uwe serious na jambo hili la sewage system jijini, vinginevyo utakuwa unapoteza hela za bure kila mwaka, hela ambazo zingeweza fanya mambo mengine mengi muhimu ya maendeleo nchini.

Wengi walio chukua masomo ya sayansi hasa somo la Geography kinadharia inaeleweka kuwa maeneo yenye maporomoko makali ya kimazingira kuna hathari kubwa za kutokea mmomonyoko wa ardhi pindi mvua zinapo nyesha na jawabu la kutatua tatizo hilo linaeleweka ni kupanda nyasi na miti ambayo itasaidia kwa kiasi fulani kuzuia mmomonyoko huo wa ardhi usitokee. Na sehemu zenye majengo mengi ni kujaribu kwa kadri itakavyo wezekana kuifunika ardhi kwa njia nyingine ambazo zitazuia mmomonyoko huo wa ardhi usitokee na pia kujenga; barabara za lami, mitaro au Drainage systems, pavements na kadhalika.

Rais Magufuli kuwa na seriousness kwenye maswala haya yanayo husu maji taka na maji ya mvua jijini. Dar es salaam inahitaji sewage systems za uhakika kama za wenzetu kwenye nchi zilizo piga hatua za kimaendeleo na sio hivi vijimitalo tunavyo vijenga kando kando ya barabara zetu. Havitasaidia kitu chochote.

Kwa jinsi nilivyo kusikia jana ukiwa njiani ukielekea kwenye mkutano wako Kawe, nilipata shock kubwa sana kusikia eti umetenga shilingi bilioni 32, pesa ambazo zitatumika kwa ajili ya kutengeneza mitalo jijini Dsr es salaam na kutegemea kuondoa hili tatizo la mafuriko jijini. Hiyo wajerumani wanasema, "Es ist lächerlich!" Na ni "lächerlich" kweli kweli.

Hiyo inaonyesha Rais wetu jinsi gani ulivyokuwa hujajua nini maana na umuhimu wa kuwa na sewage system ya uhakika mijini. Sewage system kwenye nchi za wenzetu ni moja wapo ya nguzo inayo determine uchumi na maendeleo ya nchi. Na pia ni mojawapo ya Study ya chuo kikuu na ina institutes zinazofanya research kuhusu maswala haya na kwa nchi kama ujerumani hiki kitengo kiko chini ya wizara maaluma ya mazingira.

Mbali na hilo sewage system ni source kubwa ya ajira kwa vijana wetu na vile vile sio jambo la kulitengea shilingi bilion 32. Hiki ni kichekesho! Hili swala kwa jiji la Dar es salaam linahitji pesa nyingi sana na utaalam mkubwa na pia usimamizi wa hali ya juu. Bila hilo tutakwama tu. Hatutakuwa na maendeleo ya kweli.

Nafikiri sasa nimepata jawabu kwanini Rais Magufuli ulimteua Mh. Zungu kuwa waziri wa mazingira. Hiyo kwangu ni dalili ya kutambua jinsi gani wewe hili swala la sewage system umelielewa na kutambua umuhimu wake. Hili swala liko katika sekta nyeti sana kisasi kwamba ina impact kubwa kwenye maisha yetu ya kila siku, lakini wewe naona bado unalichukulia kimazaa mzaa.

Sewage system ina umuhimu mkubwa sana katika maisha ya jamii kama ambavyo mabomba ya maji safi na umeme mijini ulivyo. Kuendelea kulichukulia hili swala kimzaa mzaa kwenye jiji ambalo function curve ya ongezeko la wakazi wake linakua exponentially mwaka hadi mwaka, ni sawasawa na kujitia kitanzi shingoni, tukisubiri kamba hiyo ivutwe na maisha yateketee.

Ujenzi wa mkondo wa mto Msimbazi peke yake kutoka kwenye source yake huko milima ya Kwembe mpaka Jangwani inaweza ku-cost shilingi bilioni 100. Alafu wewe unawatangazia wana Dar es salaam kuwa umetenga shilingi bilion 32 kwa ajili ya kujenga mitalo Dar es salaam? Aisee! Kweli tunahitaji PHD kujua jinsi gani hiyo mitaro kwa kiasi hicho cha fedha kinaweza kutatua matatizo ya mafuriko jijini.

Ukweli ninaouona mimi hapa ni kwamba sio kweli kuwa huwezi kugharamia miradi hio ya sewage system bali naona unashindwa kwa sababu ya kuchukua maamuzi mazito ya kuvunja baadhi ya nyumba za watu na kulipa compensation. Kwa utafiti wangu nilio ufanya kwa mikondo ya mto msimbazi sidhani kama kutakuwa na haja ya kutoa compensation kubwa sana, kwani nyumba nyingi zinaonekana kuwa mbali na mikondo hiyo.

Huwezi tatua swala hili ambalo jiji letu la Dar es salaam linakabiliana nalo kwa kuliona kama ni kitu kidogo. Nguvu na skill kubwa inatakiwa itumike. Hapa Rais Magufuli unahitaji mtu ambaye atakuongoza kwenye kutafuta ufumbuzi wa tatizo hili.

Nakuomba achana na hao makandarasi na wahandisi wa kutoka India au Pakistan. Hawana maarifa yoyote ya kutatua matatizo kama haya. Kwanza wao ndiyo watu wanaoleta matatizo mengi ya ujenzi kwenye hii nchi. Huko kwao wanakotoka wameshindwa kutatua matatizo ya namna hii sembuse ndiyo waweze kwetu? Tunahitaji wataalam wenye upeo wa hali juu kuhusiana na matatzo haya ya mafuriko.

Mwisho naomba nikutakie mafanikio mema katika kampeni zako za uchaguzi tarehe 28.
 
Back
Top Bottom