Uchaguzi 2020 Rais Magufuli kama Mbeya na Kanda ya Nyasa na Arusha mjini wanamshabikia Tundu Lissu na CHADEMA kiasi hiki, wapi utakuwa umefanya makosa?

Ni suala la muda tu, huko ulikotaja Magufuli atafunika mbaya kabisa. Mpaka uje ufute bandiko lako na ufanye utafiti upya.
 
Pamoja na limakala lako kuwa reefu! Lakini Lisu havuki 20% ya kura
Sidhani kama umesoma mpaka mwisho, ila kwa nilivyomuelewa mwandishi hana tatizo kabisa na JPM kushinda uchaguzi huu na ndivyo anavyowish ashinde.

Lakini amejaribu kutoa mapendekezo katika dira na mustakabali wa maisha ya watu kutoka 2020-2025,kwangu mimi nampongeza kwa kutumia muda wake kuandika uzi huu na hii inaonesha anaupendo kwa nchi na wananchi wake lakini pia anajali na kuheshimu viongozi wake.

Rai yangu kwake nafikiria Mheshimiwa huwa anapitia hapa ama wasaidizi wake huwa wanasoma, hivyo kwa yale mazuri watayachukua na kwa yale ambayo hayapo sawa ila yenye nia nzuri wanaweza kuyaboresha kwasababu lengo la serikali ni kuhakikisha nchi inasonga mbele.

Mwisho ila kwa umuhimu nawaomba tujitokeze kupiga kura na ikipendezea tumpatie JPM kura za kutosha ili aweze kumalizia kazi yake.

JPM 2020-2025
 
Hili ndilo tatizop la vijana wa Kiafrika, siri ya Maendeleo utayapata kutokana Maandishi hicho ndio chanzo sahihi ya kupanua uelewa wako.Usipende sana vitu vya kusimuliwa tafata maarifa katika vitabu na machapisho ya kitalaamu.Huyu ndugu Mier ameamua kuchukua mda wake kushare nasi kile anachokifahamu.
 
Aliyekwambia huwa sisomi vitabu nini maana nimeanza kusoma maandishi marefu robo tatu nikusifia tu mwanaume mwenzake, sasa hapo aeleweke vipi kutwa kusifia mwanaume mwenzako ni udhaifu, then nikaendelea kusoma nafika mahali anatukana wengine halafu kwenye bandiko lake ana mtaja mtaja Mungu nikaona mnafiki tu na yeye na bandiko lake kwangu likakosa maana
 
Wewe ni mwongo na unatoa uzushi ambao hauna kichwa wala miguu.

Kwenye mada yangu kuna paragraphs kama 94 hivi na kati ya hizo ni pargagraphs 4 tu za mwanzo nimemsifu Rais Magufuli kwa kazi zake na ujasiri alio uonyesha kwetu zidi ya wanyonyaji.

Sasa ungizingatia idadi hiyo ya paragraphs ambazo nimemsifia kwa kazi zake na jumla ya idadi ya paragraphs kwenye mada yangu utaona ni kama 3.8% tu nimezitumia kumsifu yeye. Hizo nyingine zote nimezitumia kama mtazamo wangu juu ya maisha yetu na nini kifanyike ili tuweze songa mbele kimaendeleo kiasi kwamba vijana kama nyie msiwe na frustrations za maisha.

Ninacho kusihii ukitambue ni kwamba kule kuishi kwa janja janja kwa kupiga madeal na kuwa Millionen, Tundu Lissu akiruhusu hii nchi iwe tegemezi kwa wazungu hutaipata tena. Na swala la mzungu kukujali wewe sokwe kama binadam mwenzake hiyo sahau.

Mzungu tajiri anashindwa wasaidia wazungu wenzake kwao na kuhamisha mtaji wake China eti ndiyo aje akusidie wewe sokwe? Endelea tu na chozi zako za mchana.

Nikupe mfano tu ambao labda utauelewa kwa ufasaha jinsi matajiri walivyo. Matajiri wakubwa dunuani kama Warren Buffett, Bill and Melinda Gate, Bezos wa Amazo, Mark Zuckerberg, na wengine kadha wa kadha umeshawasikia kwenye kipindi hiki cha Lockdown kwa ajili ya Covid 19 wakitoa mabilioni yao kuzisaidia serikali zao ili ziwasaidie hata kwa chakula tu wananchi wao? Je umejiuliza hizo hela zote walizo nazo wanazifanyia nini kwa manufaa ya umma?

Ukipata majibu ya maswali yangu haya nafikiri ndiyo utatambua jinsi gani nchi yetu itakuwa pindi Lissu atakaponshika madaraka, kwani inabidi uelewe kuwa Lissu hatakuwa na say kama hivi sasa Magufuli.

Lissu atakuwa amebanwa na hao matajiri na yeye na wenzake wataamua kuchukua chao na kuondoka. Nyie mtajua mtakacho fanya.

Asikudanganye mtu ndugu yangu kwenye Ulimwengu huu wa leo ukimwona mwafrika mwenzako ana anza kupata umaarufu kwa mzungu basi naomba ujiulize mara sita sita kwa nini? Usiwe na mawazo ya kuwa na ulafi wa utajiri wa bila kufanya kazi. Hutaupata kirahisi hivyo kama unavyofikiria.

Magufuli katupa sisi fursa nyingi sana za maisha ambazo sizani kama fursa hizi tutakuwa nazo endapo Lissu atakuwa Rais.

Kwaza naomba ujiulize hivi sasa Lissu hana hela, akiwa madarakani atafanya nini kwanza? Off course atajitajirisha mwenyewe kwanza na pili wasaidizi wake, lakini kwa hela zipi? Hela zetu za kodi na baada ya hapo unafikiri atakuwa tena na mawazo ya kutengenzeza barabara ambazo anazikandia? Off course not. Hii miradi yote wazungu watamqambua asiitekeleze, kwani hawana mpango wa kutuona sisi tunajikwamua wenyewe kimaisha.

Hawapendi kwa sababu wanajua fika kuwa tukiwa na nguvu na uwezo, hawataweza kuto cotral sisi na na uwezo wa kuchota rasilimali zetu kwa jinsi wanavyo taka hawatweza.

Ulimwengu unatawaliwa na watu wachache wenye pesa. Wao ndiyo wana amua nini kifanyike. Angalia hii clip kuhusu Melina Gate mke wa Bill Gate:
 
Uko so biased mno kwa kweli kwanini umsifie hivo mwanaume mwenzako? Yani unamsifu kuliko muumba wako jamani loh.
Halafu kwanini ujiite sokwe Yani unaji undermine kuwa wewe sio chochote Wala huna nafasi yoyote?
Pia most of the time blaming mabeberu tu hata kwa uzembe wetu wenyewe huko ka si kukwepa responsibilities nini, maana mabeberu imekuwa chaka la watawala kuficha udhaifu wao kwa kuchota akili watu wenye uelewa mdogo wa Mambo, hao hao mabeberu mnaowatukana bila wao hamuwezi ishi mnategemea kununua ndege kutoa kwako, madawa mbalimbali ka ARV then mkiwa kwenye siasa mnaongea utopian thought ili iweje? Na huyo lissu Mimi sio shabiki wake napenda kitu kilicho halisi maana wanasiasa wote wanafiki tu ni ndumilakuwili wataka madaraka na wabinafsi so yoyote atakayepata nafasi atatelekeza sera, so kusema lissu Hana hela kwani magufuli anatoa hela yake mfukoni kufanya maendeleo? Maana Mimi ka raia nakatwa Kodi na TRA iweje uje useme flani anatuletea maendeleo as if anatoa mfukoni kwako na hisani kumbe tunakatwa Kodi kubwa bila huruma na return yake kwa raia bado sio kubwa, so kwangu mimi yoyote atakayetelekeza National interest apewe kiupaumbele na sio kusingizia mabeberu kwa udhaifu wetu wenyewe.
 
Mkuu Kilatha nakushukuru kwa mchango wa hoja yako, lakini kulingana na uhalisia wa mada yangu utagundua kuwa haukuwa kutoa lawama bali ni kutoa mapendekezo ya cha nini kifanyike ili tatizo la ajira na pia uenezi wa maarifa kwa vijana wetu uweze kufanyika au kutamalaki.

Kama kwako imeonekana kuwa ni lawama basi ningekuomba kusoma tena kipegele kinacho husu mambo ambayo Rais Magufu angeweza kuyafanya ili kuondoa tatizo hilo ambalo linatukabili.

Kwenye kipengele hiki ninacho kinukuu nimelezea yafuatayo;

"Mimi binafsi ningekuomba sana tena sana kutokuwa na uoga au ukakasi wowote ule wa kuwahakikishia watanzania kuwa wewe katika muhula wako huu wa pili, kama watanzania watakupa ridhaa ya kuunda serikali tena, utatumia nguvu zako zote, maarifa yako yote na rasilimali zetu zote tulizo nazo nchini kuwekeza kwenye miradi mikubwa ya kimkakati ambayo itawawezesha wananchi kwanza kuondokana na tatizo la kuwa na njaa na pili kwa kuweka juhudi kubwa kwenye kuweka mazingira mazuri ya kuzalisha ajira nyingi kwa wananchi kwa kufanya yafuatayo;

1. construction and manufacturing
industries,
2. Aggricaltural revolution,
3. Energy source,
4. Forth Industrial Revolution
Kuongeza juhudi kubwa kwenye IT
(Information Technology),
5. Miundo mbinu zaidi ya puplic transort
kama; High Speed Trains
na Commuter trains au Trams mijini.
6. Tourismus and intertainmemt (Sport na
sanaa)
7. Kuweka mifumo thabiti ya usafishaji wa
maji taka (sewage systems and
wastewater treatment plants)
8. Scientific Research (Utafiti wa kisayansi)"

Kinaonyesha dhahiri mawazo yangu juu ya mada nzima niliyo i-discuss.

Kama kuna kitu ambacho wewe unaweza ukakiona kama ni lawama ni pale nilipo sema kuwa yeye (Rais Magufuli) anazunguka majukwaani nchi nzima akipiga kelele za kwamba nchi hii ni tajiri, kama hii nchi ni tajiri basi autumie huo utajiri tulio nao ambao yeye anauona ili kuleta mandeleo ya nchi yetu na kuondoa tatizo kubwa linalo wakabili vijana la njaa na ajira.

[emoji3][emoji3][emoji3] Nakushuru kwa complement yako ya kunikebei kuhusiana na profession yangu, lakini hata hivyo ningependa kukuambia kitu kimoja "be carefull na propaganda za wazungu kuhusiana na maswala mazima yanayo husu energy.

Wachina kwa mfano wamejenga mzinga wa Dam kwa ajili ya kuzalisha umeme wa karibu Terawatt moja huko kwao kwenye mto Jangtsekiang na Wajerumani bado wanatumia mitambo yao mipya inayofua umeme kwa kutumia coal, njia ambazo zina pollute environment. Sisi huku wanatuzuia kutumia mito yetu na makaa yetu ya mawe ili kuzalisha umeme wa kutosha.

Hivyo wewe ulie karirishwa na kuaminishwa chochote wanachofanya wao ni sawa, huoni kama hiyo ni double standard? Au wewe unaonaje?

Kitu kingine ambacho pia unapaswa kukijua ni kuacha kuimba nyimbo za ngonjera kuhusu Reduction of the Earth temperature through renewable Energy sources kama wazungu wanavyo wakaririsha nyie. Wewe unazungumzia chanzo cha renewable energy kama solar, lakini unasahahu kuwa ili kuweza ku tap hiyo energy kuna vitu vinahitajika vitengenezwe ndiyo tuweze ku tap hiyo energy. Usiangalie aspect moja katika chain nzima ya Energy Generation.

Katika Energy Generation kwa njia ya solar kuna baadhi ya vitu vinahitajika kama facilities mojawapo muhimu sana. Solar Modules ambazo process zake katika manufacturing ni very energy intensive na zenyewe upatikaji wake zinahitaji kuwa analysed.

Kama ambavyo umeshawahi sikia kuwa solar cells zinatokana na SiO2 (sand), kwa hiyo process ya upatikanaji wake unahitaji joto la hali ya juu zaidi kuliko hata joto la ipatikanaji wa chuma. SiO2 inayeyuka kwenye 1710 °C, wakati chuma kwenye 1538 °C.

Kwa hali hii peke yake inatuonyesha kuwa ni uongo wa hali ya juu unatumika ili kutuhadaa sisi kuhusiana na hiyo process ya generation of the renewable energy. Hapa namaanisha kuwa factors zote zinazohitajika ili kufanya mahesabu kamili ya kubalance energy haziwi icluded.

Kitu kingine ambacho hakizingatiwi kwenye Energy Equetion ni efficience ya Solar cell moja ya Silicon. Efficience ya Solar cell moja ni 17% ambayo ukiilinganishwa na production costs utaona kwamba faida ya energy ya Solar cell moja ni ndogo sana.

Tatizo hapa liko kwa watu kama nyie. Afrika tuna wasomi kibao ambao wamesoma madudu ambayo hawayaelewi na hawajui kuyatumia. Ni sawa na wewe unaimba tu Renewable Energy Source lakini hujui jinsi gani solar cell moja inavyopatikana.

Ndiyo maana watu kama nyie mzungu akija kuwaambia kitu basi mnakubali mara moja kuwa ndiyo hivyo. Hamkai mkatumia nafasi zenu na maarifa mliyo yatapata kwenye fani zenu, kujiuliza inakuwaje? Hivi haya mambo ambayo hawa Caucasians wanawaeleza ni kweli au si kweli?

Misomi uchwara ya nadharia kama nyinyi mnatuangusha sana Afrika. Mnajazwa uongo na wazungu na wapiga mahesbu yenu fake ya kibiashara, mnakubali na kuja kwetu sisi kutuambia ni kweli kutengeneza chuma yetu it is not viable. Who says that?

Sikiliza mkuu wewe hujachukua Material science na wala hujui mahesabu ya material science kwa hiyo sio sawa unakuja na aspect moja tu ya kiuchumi ku overrule kila kitu. Hayo ndiyo makosa mbayo mnayafanya.

Kama nyie hamjui properties za material tofauti, wachukueni basi wataalam wa vitu hivyo kwenye makadirio ya miradi ya maendeleo yenu badala ya kuwakatisha tamaa watu wanaotaka kuleta maendeleo ya nchi kwa kutumia rasilimali zetu.

Tanzania tukiamua kuanzisha mtambo wetu wenyewe wa kutengeneza chuma tutafaidika maradufu sio tu kwa faida itakayo patikana na mauzo ya hiyo product, bali pia itakuwa chachu ya kuwa na wataalam na wajasiliamali wengi na hivyo kusababisha kukua kwa uchumi wetu na vilevile maendeleo ya nchi. Hii ndiyo njia mojawapo kubwa ya kupunguza idadi ya watu wasio na ajira.

Tuna advantage moja kubwa ya kubreak even kwa haraka nayo ni kwamba mali zetu ghafi zote ziko nchini. Hatuna haja ya kuagiza Iron ore wala makaa ya mawe wala gesi asilia kutoka nje.

Katika kuzalisha/extract Iron kama raw material kwa ajili ya kutengeneza chuma steel na cast iron hewa (O2), coal kama fuel au gesi asilia inahitajika na sio umeme.
Umeme unahitajika kwenye kutengeneza chuma (steel).

Hakuna nchi wala kampini ambayo inaanza kufanya kitu kwa mara ya kwanza ikawa na maexperts wake yenyewe bali inaanza na baadhi ya maexperts walio watoa sehemu tofauti ikiwemo nje, baadae ndiyo watu wa nyumbani wanafundishwa taratibu.

Mjerumani alipo wekeza kwenye locomotive yake ya kwanza kutoka Nuernmberg kwenda Furth mpaka dreva wa hiyo locomotive alikuwa mwingereza, lakini baada ya miaka 10 ijayo Dailmler akagundua gari lake la kwanza.

Hapa nataka nikuambie kuwa bila technology Transfer hakuna technology Transformation. Wajerumani kwenye hicho kipindi cha miaka kumi waliendelea kueneza njia nyingine za reli na kuongeza treni nyingine. Kwa hiyo wajerumani walipanua professions na hivyo kuajiri watu wengi. Badae wakaanza kutengeza treni zao wenyewe na kuzifanyia Experiments tofaut mpaka wakaja kugundua treni za umeme na ndiyo maana mpaka sasa wajerumani ni namba one katika kutengeza trains. Na panapo majariwa na sisi mwakani tutakuwa na high speed trains zetu za kwanza ambazo imetokana na jasho letu.

Hivi ndivyo maenseleo na ustaarabu unavyo anza. Afrika tunahitaji watu jasiri, wenye kuthubutu na wenye maono kama Rais Magufuli, kwani watu kama hawa ndiyo wanao leta maendeleo ya watu.

Rais Magufuli ana maono kwa sababu ameielewa science na ndiyo maana hababaiki. Anajiamini kwa kile anachokifanya sababu science inampa yeye kujiamini.

Nyie watu msiojua au kuielewa science mnamatatizo makubwa sana kwasabu masomo yenu hayawapi nguvu ya kujiamini kwa kile mnacho kifanya na ndiyo maana mmekuwa mzigo kwa waafrika. Kwa kutokujiamini kwenu mna wa Induce mpaka wananchi wa society yenu. Wanakuwa waoga kwa kila jambo.

Sio kila bishara lazim ianze na faida, kuna biashara nyingine ili uzielewe vizuri lazima uanze na hasara badaadae ukisha ielewa ndiyo utapata maarifa ambayo yatakusaidia kupata faida.

Kama mambo mengine huyajui afadhali ukae kimya kuliko unajifanya unajua kumbe hujui kitu. Naomba nikuulize kitu. Waigereza walianza kutengeza chuma kwanza au loconotives?

Waingereza walisha anza tengeneza meli za chuma kabla hata George na Robert Stephensons kutengeneza locomotive yao ya kwanza.
 
Kitambulisho vyake vya ujasiliamali, kuzuia mikutano ya siasa, ajira hamna, wakati watu wengi wamestaafu ,wengine vifo ndani ya miaka 5 ,lakini huyu baba kaajiri walimu wa sayansi tu na wstumishi wa afya. Kada nyingine zote hazijaguswa kabisa,
 
Kitambulisho vyake vya ujasiliamali, kuzuia mikutano ya siasa, ajira hamna, wakati watu wengi wamestaafu ,wengine vifo ndani ya miaka 5 ,lakini huyu baba kaajiri walimu wa sayansi tu na wstumishi wa afya. Kada nyingine zote hazijaguswa kabisa,
Ni vizuri kama ameajiri walim wengi wa sayansi. Atakuwa yuko right kwa sababu sayansi ni kitu muhimu sana kwenye maisha ya binadam kuliko hata dini au kuabudu mungu wa wazungu alio letwa kwa meli na wakoloni.

Hao wasomi wa mambo mengine kama wasomi wa uchumi, utawala, Theology na mengineyo kwenye kipindi cha miaka karibu 60 toka tupate uhuru wamefanya nini katika kulijenga taifa hili kimaendeleo? Nothing! Absolutelly nothing!

Wame create watu waoga na wasio jiamini, Watu wasiojua maisha ni nini, Watu ambao wanamsujudu mzungu na kumwona yeye ni kama mungu, Ndiyo maana mnawaona watu kama akina Lissu, Zitto Kabwe na Membe ambao hawajiamini wako tayari kutaka sisi tutawaliwe na mkoloni mambo leo eti kwa sababu tu wao wanataka wawe viongozi wa nchi. Thubutuuu!

Japo kuwa naweza sema mawazo ya Lissu ya kutaka kubadili mfumo wa kiutawala, hasa wa kuwataka marais wetu nao wawajibishwe pindi inapo bainika kuwa kuna makosa wame yatenda, sio mbaya passee na mimi kuunga mkono azimio hilo, lakini approach yake ya kufikia lengo hilo kwa kushirikiana na mabeberu na hasa Robert Amsterdam ambaye ni mleta Chaos kwenye nchi masikini na kukandia kila kitu ambacho Rais wetu amejitahidi so far kukifanya kwa maendeleo yetu, hicho kitendo kidogo kinanipa utata.

Wasomi wa masomo ya sayansi duniani kwote ni watu ambao wako very very constructive na contributive kwenye maisha ya binadam, lakiki wengine wote ni destruktive na hasa wasomi wa Theology. Si mnamwona kwa mfano Mbunge AD wa Iringa mjini, Peter Msigwa jinsi alivyo?

Hivyo ndivyo jinsi ya namna ya watu wenye kusoma sana theology walivyo. Wanataka kwenye kila kitu, hata kile wasichokiweza, wawe mstari wa mbele. Wasipofanikiwa kwenye mipango hiyo wanapata frustrations na kuanza kuwa wendawazimu.

Kwa hiyo sioni sababu ya wewe kumlaumu Rais Magufuli kwa vifo vya watu ambao wanaamua kuondoa maisha yao. Katika mabadiliko ya yoyote yale ya kimfumo lazima kuna baadhi ya member wa system, au tuseme society, lazima wawe loser.
Na hiyo sio principle ya Rais Magufuli bali ni principle ya nature.

Hata kama Lissu atashinda uchaguzi na kuwa Rais wetu, kama ata impliment agenda yake ya kurekebisha katiba na mfumo wa kiutawala, kutakuwa na mabadiliko tu ambayo yatasababisha baadhi ya watu kupoteza vitu vyao ambavyo wamekuwa wanavitegemea kimaisha. Ndiyo nature ya maisha ilivyo. Hakuna mtu anaweza akafanya chochote kuzuia, zaidi ya kutoa pole kwao.
 


Mkuu nianze kwa kukuomba radhi saw your post but couldn’t respond to it, si unajua tena JF chini ya utawala wa ‘Napoleon’ kwenye animal farm “all animals are equal but some are more equal than others”. Ni sawa kwa wengine kumuita Magu kila jina ukifanya ivyo kwa Lissu unakula ban.

Kuhusu hoja zako rasmi will respond appropriately in due time.
 

..Mkuu uliwekwa "selo."?

..kama hilo lilikutokea pole sana.

..wenzako wa CDM kila kukicha wanachezea selo za Polisi au Tume.

..kuna wagombea wa CDM wamefungiwa kufanya kampeni mmoja siku 7, mwingine 14.

..wako wengine rufaa zao hazijaamuliwa mpaka leo hii.
 
Hila humu wamezidi hawana tu uwezo wa kutupeleka selo, vinginevyo ingekuwa uraiani adhabu za mods wa JF zingefanana na ‘draconian laws’, maana kosa dogo tu linaloamkera mod mmoja unakula ban.

Adhabu zao sio standardised kabisa majina anayoitwa Magufuli humu na kuwaachia wachangiaji, ukifanya ivyo kwa Lissu kosa.
 

..kaka unalalamika kuzidi hata waliopigwa risasi 16? 😂

..labda ulikutana na moderator aliyeamka vibaya.

..wakati mwingine wanafuta topic bila sababu za msingi.

..Tuwasamehe.
 
Mkuu Maneno Meier kwanza kabisa nikupongeze kwa bandiko lako hili lakini kuna mengi sana umepotosha au huyajui eidha umeyachukua sehemu bila kuyatafakari mfano swala la Gasi umezungumzia LNG ( Liquid Natural Gas) itumike majumbani.....!! Kupikia....!!!??? Ni Uongo uliopitiliza kivyovyote vile itakua eitha Nitrogen au Oxygen au Carbon dioxide...... sasa kwa hali ya Watanzania watafanyia nini majumbani? Usije kuchanganya na LPG ( Liquid Petroleum Gas).....
 
Umeajiriwa ninikwa kazi hii, maan waraka mrefuuuuu hata hivyo una moyo
 
Umeajiriwa ninikwa kazi hii, maan waraka mrefuuuuu hata hivyo una moyo
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Huu sio waraka kwa watu walio ishia darasa la saba na kwenda kuchukua asta shahada za kuangalia kuta na paa za madarasa, bali ni waraka kwa watu walio yaona madarasa kwa ndani na nje na pia maono.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…