Uchaguzi 2020 Rais Magufuli kama Mbeya na Kanda ya Nyasa na Arusha mjini wanamshabikia Tundu Lissu na CHADEMA kiasi hiki, wapi utakuwa umefanya makosa?


Sijasoma sana ila naona ni hadithi zile zile. Mbeya toka enzi ni pro chadema. JPM ameyakuta, na yanabadilika.

Kanda ya kaskazini, Moshi mjini inarudi CCM. Labda Arusha sijui sana. Kwahiyo tusichukulie wingi wa watu ndio kura za eneo hilo
 
Nimesoma yote lakini wewe ni mshenzi mwenye mawazo mazuri (inventive and innovative ideas)
 
You can’t win them all Gaddafi aliwafanyia kila kitu wananchi wake lakini bado kuna waliokosa shukran.
 
Makala yako ni nzuri kinadharia lakini mimi nadiriki kusema kwamba Awamu hii imejaribu kujibu matatizo ya nchi yetu ingawa ninakiri kuwa maendeleo ni mchakato na uzingatiaji wa vipaumbele vya kuchochea uchumi. So far so good kwa kuanzia na kuweka msingi. Niseme uchambuzi wako unatia hamasa ya kudadavua kwa kina na kwa maoni yangu hatua zifuatazo ni ni za kupongzwa na ni mwanzo mzuri huwezi kupuuza:
1. Mkazo kwenye miundo mbinu ya uzalishaji na usambazaji wa umeme wa uhakika na rahisi usio katikakatika ni hatua muhimu katika mapinduzi ya viwanda, kilimo,teknolojia unayoizungumzia, utafuti, ubunifu,ustawi wa jamii na hata uzalishaji wa chuma madini na ajira unaoizungumzia nk. Umeme ni uchumi na ni maisha.Mwelekeo wa Rais Magufuri kwa hili yuko sahihi kabisa. Hakuna nchi duniani iliyopiga maendeleo bila ya kupitia hatua hii muhimu ya umeme wa uhakika. Ujenzi wa uchumi wa nchi za ulaya, China, Malaysia,Marekani, Asian Tigers umefanikiwa baada ya kuwa na vyanzo vingi vya umeme. Hivyo kama nchi kwa maoni yangu tuanzie hapo kama kipaumbele ingawaje hukulipa uzito unaostahili kwenye mada.
2. Maji
Kitu kingine muhimu katika kusukuma maendeleo ni upatikanaji wa maji. Hili hukulizungumza sana lakini ni hitaji muhimu sana kwa maendeleo ya nchi. Maji ya uhakika ni muhimu kwa ustawi wa jamii, viwanda, tafiti na afya ya watu. Kutopatikana kwa maji safi na salama ni kielezo cha umasikini. Nchi zote zilizoendelea zimekwisha ondokana na changamoto ya maji. Hatua ya sasa ya Rais Magufuli kupigania miradi ya maji naipongeza
3.Suala lingine muhimu ni miundo mbinu vya usafirishaji km.barabara, meli, viwanja vya ndege,ni muhmu sana nchi kuwa na miundo mbinu hii ili uunganishe uchumi wa kilimo, viwanda,utalii, uvuvi, ajira- vyote hivi vinahitaji uwekezaji wa ndani na nje ya nchi ili mradi miundo mbinu wezeshi iwepo la sivyo utakuwa umeufunga uchumi.Maendeleo ya ustawi wa watu yamejifunganisha kwa kina na maendeleo ya vitu tajwa. Mjadala wa kuhoji uwepo wa hivi vitu ni kutoelewa kanuni za kiuchumi na maendeleo. Kimsingi uchumi unaongozwa na kanuni ya mduara wenye muunganisho. Huwezi kuzungumzia maendeleo ya watu bila kuzungumzia vitu vinavyowezesha uzalishaji(capital+labour+ land) vitu vinasimama upande wa capital na watu upande wa labour. Katika Afrika Mashariki na kati nchi ambazo ni economic powerhouse kama Afrika kusini angalia miundo mbinu yake ndipo utajua umuhimu wake.unapozungumzia chuma, madini, utalii,kilimo, kwa hakika Ujenzi wa miundo mbinu unajibu mahitaji hasa kwa uwekezaji mkubwa, vivutio vya utalii na ajira. Hivi vitu vinategemeana sana ili mradi tahadhari ichukuliwe kwa kujenga miundo mbinu kimkakati kwa maeneo na vipaumbele na teknlojia na ujuzi sahihi.Hatua na mwelekeo wa sasa wa kuimarisha miundombinu ni muhimu kwa kuzingatia uchumi shindani Regional competitive economy) na hususani kwa jiografia ya nchi yetu na majirani zetu ni fursa muhimu kwetu. Hata hivyo miundo mbinu hainabudi kuchochea uchumi wa kilimo hususani usafirishaji mazao, kuchochea uchumi wa bandari,utalii, na viwanda ambavyo kwa baadaye utafainya Tanzania kuwa kitovu cha uchumi mkubwa Afrika Mashariki( hub) ni suala la muda tu.
4.Teknolojia na elimu
Kwa uchumi wa kisasa hapa ninaungana na mtoa mada kuhusu umuhimu wa teknlojia, ubunifu na elimu sahihi kwa ajili ya mazingira yetu. Hili ni eneo muhimu linalohitaji msukumo wa pekee kwa uchumi wa kisasa hizi ni (software economic inputs)hazikwepeki ili uchumi uende mbele Miundo mbinu niliyoitaja hapo juu ni (Hardware) ambayo pekee haiwezi kufanya kazi vinategemeana.Hili nalo sioni kama serikali imelipuuza sana ingawaje jitihada za kuzamisha teknolojia ya digitali na elektroniki kwenye maisha ya kila siku ya mtanzania km mashule, afya,manunuzi, mawasiliano ni muhimu. Hapa kuhamasisha na kurahisisha masharti ya watanzania walio nje (dispora) kurejea na kushiriki kwenye uwekezaji wa teknolojia na ujuzi ni muhimu sana.

Maoni ya kimkakati
1.Kuna umuhimu sasa kuangalia kwa kina maeneo ya sera na sheria za kodi ili ziwe rafiki na ziendane na dhima nzima ya uwekezaji kupitia sekta binafsi.
2.Iko changamoto kubwa ya serikali kuweka mazingira rafiki na endelevu ya kuimarisha na kustawisha sekta binafsi ili iweze kujibu matatizo ya ajira na kuweza kuongeza pato la taifa. Kwa sasa yapo malalamiko ya wafanya hiashara kuhusu sheria ya kodi kuwa ni gandamizi na isiyo yenye kuhamasisha mfanyabiashara kulipa kodi kwa hiari.Sheria za kodi zinaangaliwa kwa jicho la ugandamizaji na kuua biashara. Zifanike tafiti za kina eneo hili ili kupata tiba sahihi.
4. Mifumo ya ukusanyaji kodi kwa kutumia digitali na elektroniki iendelezwe kwa vile inaleta uwazi na kupunguza urasimu na rushwa
5. Serikali ihuishe sera na sheria za kodi ili watanzania at least 90% walipe kodi ya moja kwa moja (direct tax ) hata kama ni kiasi kidogo cha fedha mf hapa nchini yapo magari ya biashara ya taxi bubu hayalipi kodi kabisa yangewekewa kiwango cha shs 10000 kwa mwezi serikali ingeingiza mapato. Yako maeneo mengi sana kama haya.Serikali ijayo itayopata ridhaa iweke kipaumbele cha kupanua wigo wa kodi na itoke kwenye kodi iliyozoeleka(traditional tax systems)ili mzigo ubebwe na wananchi wengi na pesa nyingi itapatikane. Ninakumbuka Rais alikwishalitolea maelekezo hili. TRA waanze nalo kwa ubunifu na kupitia sheria zetu na kujifunza kwa wenzetu nje ya nchi (best practices) ili kunusuru sekta binafsi, ajira na ukamilishaji wa miradi ya taifa inayoendela bila maumivu makubwa na kwa makusanyo ya kodi endelevu(sustainable)
 
Brilliant.. nimeelimika zaidi mkuu. shukrani sana kwa kutenga muda wako kutoa chakula ya ubongo.
 
Nimeufurahia mchango wako wa mada. Nitarudi kukupa mawazo yangu juu ya hoja yako. Asante sana.
 
You can’t win them all Gaddafi aliwafanyia kila kitu wananchi wake lakini bado kuna waliokosa shukran.
Sawa kabisa. Tofauti kati ya Gadafi na Magufuli ni kwamba watanzania wana njaa na hawana perspective. Walibya walikuwa hawana njaa wala shida ya maisha

Sio wamachinga wote wana kipato cha uhakika kama Rais Magufuli anavyo dhani. Watu wengi wanaishi maisha ya kubaisha na hawajui kesho yake itakuwaje.
 
Sijasoma sana ila naona ni hadithi zile zile. Mbeya toka enzi ni pro chadema. JPM ameyakuta, na yanabadilika.

Kanda ya kaskazini, Moshi mjini inarudi CCM. Labda Arusha sijui sana. Kwahiyo tusichukulie wingi wa watu ndio kura za eneo hilo
Sawa. Umejikita sana kwenye uchaguzi na sio sana kimada. Hiyo ilikuwa kama Pretext. Malengo ni mambo ambayo Rais Magufuli kwa mtazamo wangu alitakiwa ayafanye kwenye awamu yake ya kwanza.
 
Unadhani serikali yetu inauwezo wa kuajiri watu wote wenye umri wa kufanya kazi? Zingatia kati ya trillion 1.3 inayokusanywa sasa, billion 600 ni mshahara kila mwezi achilia mbali matumizi mengine.

Kama unadhani inawezekana toa mwangaza wako makosa yalipo na nini kifanyike watu wapate ajira.

Magufuli yeye anadhani hilo swala ni impossible anafikiria long term solution kutengeneza miundombinu itakayotoa access ya kufikia sehemu mbali mbali na umeme wa uhakika kwa bei nafuu ili kuvutia uwekezaji wa private sector na kutoa ajira.

Sasa wewe kama una mbinu mbadala ya haraka ebu tuelezee utawasaidia vipi hao watu wenye kipato cha chini.
 
Ni sawa vile vile hakuna shida na hakuna mtu ana kulazimisha.

Wewe sio binadam peke yako na wala sio mtanzania peke yako na vile vile sio mswahili peke yako.

Sisi tumetapakaa ulimwemgu mzima kwa taarifa yako na sio walioko Tanzania tu. Na Jamii Forum inamfikia kila mtu mwenye interest kwenye kila pembe ya dunia.

Kuwa na amani tu!

So wichtig bist du auch nicht!
 
Nimesoma hoja zako zote, ninaloweza kusema ni kukushauri utafute Ilani ya CCM 2015/20 na ya sasa 2020/25 uichambue ukizingatia ushauri wako na Dira ya Maendeleo 20205 (Development Vision 2025). Hakika utangundua kuwa ushauri wako umenzigatiwa kwa umakini kuliko ulivyofanya kwa ukurasa mmoja humu JF.

Sina uhakika kama Ilani ya vyama vingine zinakisi "Development Vision 2025" au watatengeneza Dira Mpya ya maendeleo maana bila Dira ni ubabaishaji tu.
 
Nimependa sana mada yako. Kasoro yako ni kuonyesha mapenzi yako makubwa kwa CCM na rasi Magufuri na kuamini kuwa nchi hii haiwezi kuongozwa na mtu zaidi ya Magufuri. Ushauri wako ungeuelekeza kwa mgombea yeyote atakayepewa ridhaa na wapiga kura. Unafikia kutukatana mgombea uraisi na kumuita pimbi. kwa hili nakushauri uombe samahani! wasomaji wengi ni wapenzi wa Lissu. Kumuita pimbi ni kushusha hadhi ya mada yako. Unajua watu wengi wameishia hapo kusoma.

Kwangu mimi naona kasoro kubwa aliyonayo raisi wetu mpendwa wa sasa hivi, kubwa ni kutopenda kupokea ushauri (nahisi hata huu hataupokea). Anapenda kujiamini kuliko kuamini washauri wake. Nchi hii ni kubwa yenye watu na mali asili nyingi, haiwezi kuongozwa na kichwa kimoja kama tunavyoaminishwa. Anapashwa asikilize watalaamu mbali mbali wa uchumi, kilimo, afya, (to mention few). Watu wanomzunguka wanaangalia upepo wake unaelekea wapi na ndivyo wanavyomshauri. Imagime profesa mzima anajidhalilisha na kusema ameokotwa kutoka jalalani!
Tatizo la pili ambalo anapaswa arekebishe ni kutopenda upinzani! Alisema wazi kuwa anataka kufuta upinzani, Lo! Kwa sasa mambo mengi anayosema anarekebisha, ni kelele zilizokuwa zinapigwa na wapinzani. Kwa kiasi kikubwa anatekeleza sela za upinzani. Watu wake wanaomzunguka hakuna wenye uthubutu wa kukosoa anayofanya. Kama siyo wapinzani, nani basi atakubali kumfunga paka kengere. Wapinzani wafanye kazi, aache vyombo vya habari viwe huru kukosoa, aache magazeti yawe huru kusema wapoona panakwenda tenge, aache wanaharakati wakosoe wanapoona pana dosari. Hii ndiyo namna pekee ya kujua dosari zake. Kwa hulka yake kamwe asitegemee kukosolewa na watu wanaomzunguka.
Mwisho kabisa ambacho huwa sipendi ni imani kuwa nchi hii daima itaongozwa na CCM. Ni kutetea kwa nguvu zote either kwa kutumia vyombo vya dora ( kama alivyosema katibu mkuu wa CCM - wanatumia jeshi la polisi kubaki madarakani) au rafu nyingine ilimradi washike dora. Acha watanzania wajiamulie kwa uhuru nani wanataka awatawale. Wakipenda CCM sawa, wakipenda CDM sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…