Rais Magufuli kutamka hadharani kuwa Prof. Kabudi na Lukuvi hawawezi kuwa miongoni ya Rais ajaye mwaka 2025; Je, amevunja Katiba ya nchi?

Rais Magufuli kutamka hadharani kuwa Prof. Kabudi na Lukuvi hawawezi kuwa miongoni ya Rais ajaye mwaka 2025; Je, amevunja Katiba ya nchi?

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,843
Reaction score
31,057
Tulimsikia Rais Magufuli wakati akimwapisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akisema kuwa Profesa Kabudi na William Lukuvi hawawezi kuwa miongoni ya wagombea wa Urais wa CCM kwa mwaka 2025, kwa kuwa tu umri wao hauwaruhusu, kwa kuwa watakuwa na umri mkubwa, kwa kuwa ameeleza kuwa Rais ajaye atakuwa kijana na hataruhusu yeyote atakayekuwa na umri unaomzidi yeye Rais Magufuli, agombee Urais kwa mwaka huo wa 2025, je kwa kuyatamka hayo amevunja Katiba ya nchi?

Nimesoma Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzani,1977 ambayo imetaja sifa za mtu anayetakiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na inasema kama ifuatavyo katika ibara ya 39, kama ifuatavyo:-

39(1) Mtu hatastahili kuchaguliwa kushika kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, isipokuwa kama:-

(a) Ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa sheria ya Urais

(b) Ametimiza umri wa miaka arobaini

(c) Ni mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa

(d) Anazo sifa za kumwezesha kuwa mbunge au Baraza la Wawalikishi

(e) Katika kipindi cha miaka mitano kabla ya uchaguzi Mkuu, hajawahi kutiwa hatiani katika Mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote ya Serikali


Katika masharti hayo naliona sharti la umri wa chini kabisa wa miaka 40 (minimum age) na sijaona kipengele chochote kinachomzuia mgombea yeyote kutokana na umri wa juu (maximum age)

Sasa nimuulize Rais Magufuli amepata wapi mamlaka nje ya Katiba ya nchi ya kuwatamkia akina Profesa Kabudi na William Lukuvi kuwa watakuwa disqualified kutokana na umri wao kuwa mkubwa?

Kwa kuwa kutokana na Maelezo yake hataruhusu mtu yeyote atakayekuwa na umri wa zaidi ya miaka 65, ifikapo mwaka 2025, kugombea Urais!

Hivi sisi wananchi tunaposema kuwa yeye Rais matamshi yake ndiyo yanakuwa sheria tutakuwa tunakosea kweli?

Hivi inawezekanaje yeye Rais Magufuli atoe matamshi, ambayo anajua wazi kuwa yanavunja Katiba ya nchi?
 
Jamaa kaanza kuwaandaa watu kisaikolojia! Kwamba no one like him.. Lazima niseme na huo ndo ukweli wenyewee.
Hivi hata mgombea atakuwa na umri kama Museveni au Joe Baden, atakuwa amevunja ibara ipi ndani ya Katiba ya nchi?

Sasa yeye Rais Magufuli anaposema kuwa Rais ajaye ni lazima awe kijana, je anatuandalia mtu wake wa mfukoni?

Tutakapokuwa tunahisi kuwa anatuandalia mtu wake wa dizaini ya Bashite, tutakuwa tunakosea kweli?
 
Hivi hata mgombea atakuwa na umri kama Museveni au Joe Baden, atakuwa amevunja ibara ipi ndani ya Katiba ya nchi?

Sasa yeye Rais Magufuli anaposema kuwa Rais ajaye ni lazima awe kijana, je anatuandalia mtu wake wa mfukoni?
Mkuu huyo mwamba ashatuona vilaza ndiyo maana anaongea anachojisikia. We huoni licha ya kuongea huo utopolo bado wabunge walimpigia makofi.
 
Mkuu huyo mwamba ashatuona vilaza ndiyo maana anaongea anachojisikia. We huoni licha ya kuongea huo utopolo bado wabunge walimpigia makofi.
Ninachojua Mimi ni kuwa kwa mujibu wa Katiba ya nchi, hao kina Profesa Kabudi na William Lukuvi wana haki ya kujaza form za urais mwaka 2025.

Na kama "kukatwa" majina hayo yatakatwa na wajumbe wa chama chao cha CCM, katika kura za maoni.

Yeye kama Rais wa nchi hana mamlaka yoyote ya kutuchagulia Rais ajaye.
 
Magufuli huwa hapimi maneno yake.

Huwa yanamtoka tu utadhani mtoto.
Ukweli ni kuwa ni lazima mtu unapokuwa na nafasi kubwa kama hiyo ya Urais upime kila unachokitamka, mbele ya hadhara.

Cha kushangaza ni kuwa kwa Rais tuliye naye hapimi kabisa madhara ya maneno yanayomtoka.

Kwanza ni lazima ajue kuwa nchi yetu ina mfumo wa vyama Vingi, kwa hiyo hapaswi kuwa na uhakika wa asilimia 100 kuwa ni lazima mshindi wa kiti cha urais ni lazima atoke kwenye chama chake cha CCM!
 
Tafsiri yake atoki leo Wala kesho na hata akitoka hao watakuwa washazeeka sana
 
Jamaa kaanza kuwaandaa watu kisaikolojia! Kwamba no one like him.. Lazima niseme na huo ndo ukweli wenyewee.

Mark my words majitu yalivyo mapuuz yatakuja kushtuka mwishoni huyu dingi anatuharibia hii nchi tutakuja kuparangana vibaya sana
 
Magufuli huwa hapimi maneno yake.

Huwa yanamtoka tu utadhani mtoto.
Haa😁😂😀😅😄😄😃😁😂🤣😅😄😄
Usimseme Mwenyekiti Vibaya 🤨😑😏😐
Wanachama Hatujapenda Kabisa 😁😂😅
Kiongozi Wetu Huwa Hakosei


Jamiiforums.com Ina Thread Nyingi Nzuri Sana
Katiba Imevunjwa Na Itaendelea Kuvunjwa
Mtake Msitake (Atake Asitake, Tutamuongezea Muda)😶🤨😑😎😐😏😏


Kosea Kuoa Lakini Siyo Kuchagua Ukikosea Kuchagua Ni Mpaka Baada Ya Miaka Mitano
Ila Tumeibiwa Uchaguzi Mkuu Huu
 
Back
Top Bottom