Rais Magufuli kutamka hadharani kuwa Prof. Kabudi na Lukuvi hawawezi kuwa miongoni ya Rais ajaye mwaka 2025; Je, amevunja Katiba ya nchi?

Tofauti ni kwamba angalau kwa Trump kuna sauti toka ndani ya Republicans wenzake za kutokukubaliana nae. Huku kwetu hakuna hata sauti moja ndani ya chama chake iliyo na itakayothubu kusema lolote dhidi ya Mwenyekiti na Rais wa nchi
Mbona Membe alikuwa akimkosoa!
 
Swali la msingi zaidi tujiulize kwa kusema hivyo ana mtu wake kishamweka akilini nwake na sasa anatutayarisha kisaikologia? Anajuaje kama raisi ajae atatoka CCM ambako ana madaraka katika uteuzi wake au ndo haya yaliyotokea mwaka huu?
Tunaposema hawa jamaa wa CCM wamepora uchaguzi wa mwaka huu, basi ushahidi mmojawapo ndiyo huo wa mtu kujiongelea kuwa atamteua mtu wake ili awe Rais wa nchi hii, utadhani hakuna uchaguzi wa vyama vingi ndani ya nchi hii!
 
Rais Samia aliwaambia hao hao wakongwe wa CCM kwamba kwa sasa wafanye kazi za uwaziri na masuala ya kampeni yataanza wakati ukifika.

Na hayati JPM hakukosea kuwataja hao wakongwe kwamba wasahau juu ya urais, wanao tabia zile zile za kuutaka urais kwa chini chini, ni wapenda makundi.

Rais bora kwa uzoefu wa nchi hii ni yule ambaye hazungumzwi sana midomoni. Wenye kuwa maarufu sana siku zote wapo tayari kufanya hata mambo machafu ili waingie ikulu.

Ndio maneno ya RIP Nyerere yanapokuwa na ujumbe hai kwa taifa...ikulu kuna biashara gani mpaka mtu atumie pesa kuingia!!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…