Rais Magufuli: Madaktari kukutana na Wagonjwa wa Corona ndiyo wajibu wao

Elitwege

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
5,294
Reaction score
10,970
Rais wa Tanzania John Magufuli wakati akizungumza kule kanisani Chato amesema alishangazwa sana na taarifa za madaktari na wauguzi zaidi ya 60 pale hospitali ya taifa pale Muhimbili kuwekwa karantini kisa siku za mwanzo walikutana na wagonjwa wa Corona!!

Rais Magufuli amesema alipopata taarifa hizo mara moja aliamrisha hao madaktari watolewe karantini na warudi kazini mara moja kuhudumia wananchi. Magufuli alihoji kama mtu kazi yake ni udaktari utamwepushaje asikutane na wagonjwa wa Corona? Magufuli alisema daktari kukutana na wagonjwa wa Corona ndiyo kazi yake na wajibu wake aliousomea hivyo hakuna haja ya kumuweka karantini kwa siku 14 kisa amemhudumia mgonjwa wa Corona.

My take.
Huyu Rais Magufuli tumepewa na Mungu kabisa ,ebu jiulize Mangapi anatusaidia watanzania?
Vipi hiyo tabia ya kuweka karantini madaktari isingeshitukiwa na Magufuli kwa hiyo madaktari wote nchi nzima wangewekwa karantini ? Tungehudumiwa na nani sasa?

Hivi mwanajeshi anaweza kujificha kisa milio ya risasi nchi imevamiwa?

Magufuli hata barakoa amesema yeye kuwa wananchi shoneni barakoa yoyote hata ya shuka sawa tu kuendana na uchumi wako lakini kabla ya tamko la Magufuli aliyekuwa naibu waziri wa afya Dr Ndugulile alisema hakuna kujifukiza na barakoa lazima uvae za N95 ambazo ni bei ghali kweli kweli je wananchi masikini wangezimudu?
Ebu fikiria wakati huu rais angekuwa Mbowe ingekuwaje?

Kwa kweli rais Magufuli unatutetea wanyonge wa nchi hii mchana kweupe hadharani kila mtu anaona na Mungu akulinde sana.
 
.
Screenshot_20200518-215557~2.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmeshindwa kuwapatia vifaa vya kujikinga dhidi ya maambukizi halafu mnataka kulazimisha madaktari wakahatarishe maisha yao kutibia wagonjwa wa Corona huku wakijua ni ugonjwa wa kuambukiza kwa njia ya hewa au hata kugusana. Hata wanajeshi vitani hupewa nyenzo ili wapigane na usitegemee mwananjeshi aingie uwanja wa mapambano akiwa hana silaha yeyote.

Serikali ya Magufuli imefeli kabisa katika kuhakikisha Madaktari na wauguzi wana vifaa vya kujilinda dhidi ya maambukizi ya Corona (PPE). Barakoa ya kitambaa haizuii virusi vya SARS-CoV-2, unahitaji barakoa za N95 au hata zile za kufanyia upasuaji ndio zenye filter sahihi. Nilitegemea kwa Rais aliyesoma sayansi angekuwa na uelewa kuhusiana na athari mbalimbali zinazoweza kuletwa na virusi au hata kemikali bila ya kuwa na vazi sahihi la kujilinda.

Hii serikali imejaa mbumbumbu na goigoi wasio na ubinadamu wala utu, hamthamini wala kujali maisha ya wengine ndio maana hata kuchukua hatua sahihi za kulinda uhai wa raia, madaktari na wauguzi hamuoni umuhimu wake.
 
Mmeshindwa kuwapatia vifaa vya kujikinga dhidi ya maambukizi halafu mnataka kulazimisha madaktari wakahatarishe maisha yao kutibia wagonjwa wa Corona huku wakijua ni ugonjwa wa kuambukiza kwa njia ya hewa au hata kugusana. Hata wanajshi vitani hupewa nyenzo ili wapigane na usitegemee mwananjeshi aingie uwanja wa mapambano akiwa hana silaha yeyote.

Serikali ya Magufuli imefeli kabisa katika kuhakikisha Madaktari na wauguzi wana vifaa vya kujilinda dhidi ya maambukizi (PPE) ya Corona. Barakoa ya kitambaa haizuii virusi vya SARS-CoV-2, unahitaji barakoa za N95 au hata zile za kufanyia upasuaji ndio zenye filter sahihi. Hii serikali imejaa mbumbumbu na goigoi wasio na ubinadamu wala utu, hamthamini maisha ya wengine ndio maana hata hatua sahihi za kulinda uhai wa raia hamuoni umuhimu wake.
Corona ina miezi zaidi ya miwili sasa hapa Tanzania, je umeona madaktari na manesi wangapi wameambukizwa Corona ?

Kama kweli una ushahidi kuwa serikali imefeli kuwakinga na vifaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Corona ina miezi zaidi ya miwili sasa hapa Tanzania, je umeona madaktari na manesi wangapi wameambukizwa Corona ?

Kama kweli una ushahidi kuwa serikali imefeli kuwakinga na vifaa

Sent using Jamii Forums mobile app
nakazia.. hata vifo tunavyosikia ni mitandaoni tu ama!? maana kiuhalisia mitaani tungekua tumeshasikia. nmejaribu kufatilia sana nje ya mtandao ila sisikii kitu!..

ni mawazo yangu tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmeshindwa kuwapatia vifaa vya kujikinga dhidi ya maambukizi halafu mnataka kulazimisha madaktari wakahatarishe maisha yao kutibia wagonjwa wa Corona huku wakijua ni ugonjwa wa kuambukiza kwa njia ya hewa au hata kugusana. Hata wanajeshi vitani hupewa nyenzo ili wapigane na usitegemee mwananjeshi aingie uwanja wa mapambano akiwa hana silaha yeyote.

Serikali ya Magufuli imefeli kabisa katika kuhakikisha Madaktari na wauguzi wana vifaa vya kujilinda dhidi ya maambukizi ya Corona (PPE). Barakoa ya kitambaa haizuii virusi vya SARS-CoV-2, unahitaji barakoa za N95 au hata zile za kufanyia upasuaji ndio zenye filter sahihi. Nilitegemea kwa Rais aliyesoma sayansi angekuwa na uelewa kuhusiana na athari mbalimbali zinazoweza kuletwa na virusi au hata kemikali bila ya kuwa na vazi sahihi la kujilinda.

Hii serikali imejaa mbumbumbu na goigoi wasio na ubinadamu wala utu, hamthamini wala kujali maisha ya wengine ndio maana hata kuchukua hatua sahihi za kulinda uhai wa raia, madaktari na wauguzi hamuoni umuhimu wake.
Ulongo huu!
Umeenda hospital au unahisia?
 
Corona ina miezi zaidi ya miwili sasa hapa Tanzania, je umeona madaktari na manesi wangapi wameambukizwa Corona ?

Kama kweli una ushahidi kuwa serikali imefeli kuwakinga na vifaa

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama takwimu za ukweli tu za maambukizi na vifo vya wagonjwa wa Corona hamtaki kuzitoa, tutegemee mtautangazia uma madaktari na wauguzi walioambukizwa na Corona? Si umejionea madaktari wanavyoogopa hata kutibia wagonjwa wengine kutokana na ukosefu wa PPE mpaka Waziri akaingilia kati. Mamilioni ya pesa kununua wabunge wa upinzani mnayo lakini likija suala la kulinda wataalamu wetu wa afya kwa kuwapatia nyenzo sahihi hakuna.
 
Taja hospitali ambayo imeishiwa na madaktari wake kupata Corona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais Magufuli ni nahodha bora ametuvusha salama kwenye corona

Vibaraka wa mabeberu wanaenda kuaibika vibaya
Nahodha huwa anakaa na chombo chake mpaka watu wote watoke na ikibidi anazama nacho, huyu wa kwetu kakimbia chombo na kwenda kujificha!
 
Na kukiwa na vita amiri jeshi mkuu anatakiwa aongoze mapambano au ajifiche?
Kwa
Rais wa Tanzania John Magufuli wakati akizungumza kule kanisani Chato amesema alishangazwa sana na taarifa za madaktari na wauguzi zaidi ya 60 pale hospitali ya taifa pale Muhimbili kuwekwa karantini kisa siku za mwanzo walikutana na wagonjwa wa Corona!!

Rais Magufuli amesema alipopata taarifa hizo mara moja aliamrisha hao madaktari watolewe karantini na warudi kazini mara moja kuhudumia wananchi. Magufuli alihoji kama mtu kazi yake ni udaktari utamwepushaje asikutane na wagonjwa wa Corona? Magufuli alisema daktari kukutana na wagonjwa wa Corona ndiyo kazi yake na wajibu wake aliousomea hivyo hakuna haja ya kumuweka karantini kwa siku 14 kisa amemhudumia mgonjwa wa Corona.

My take.
Huyu Rais Magufuli tumepewa na Mungu kabisa ,ebu jiulize Mangapi anatusaidia watanzania?
Vipi hiyo tabia ya kuweka karantini madaktari isingeshitukiwa na Magufuli kwa hiyo madaktari wote nchi nzima wangewekwa karantini ? Tungehudumiwa na nani sasa?

Hivi mwanajeshi anaweza kujificha kisa milio ya risasi nchi imevamiwa?

Magufuli hata barakoa amesema yeye kuwa wananchi shoneni barakoa yoyote hata ya shuka sawa tu kuendana na uchumi wako lakini kabla ya tamko la Magufuli aliyekuwa naibu waziri wa afya Dr Ndugulile alisema hakuna kujifukiza na barakoa lazima uvae za N95 ambazo ni bei ghali kweli kweli je wananchi masikini wangezimudu?
Ebu fikiria wakati huu rais angekuwa Mbowe ingekuwaje?

Kwa kweli rais Magufuli unatutetea wanyonge wa nchi hii mchana kweupe hadharani kila mtu anaona na Mungu akulinde sana.
Umenena kweli ndg ! Mungu alijua na ndio maana akatupa Rais bora na sio bora rais...tutaendelea kumuelewa Rais wetu tu ..! Viva Rais Magufuli
 
Back
Top Bottom