Hivi ni Rushwa gani na Ufisadi upi ambao Rais anapambana nao? Au awamu hii kuna Rushwa na aina mpya ya Ufisadi ambao haukuwepk hapo nyuma na tunasema anapambana nao?
Tuwe wakweli, sasa hivi anayeweza kuongelea suala la Ufisadi na Rushwa ni mmoja tu na ndio huyo huyo anayesema anapambana nao, hapo awali hata vyombo vya habari vilikuwa vinaweza kuzungumzia kuhusu Rushwa na Ufisadi.
Sasa hivi ukiwa CCM au Mtu wa kanda ya Ziwa wewe sio mla wala mtoa Rushwa na Ufisadi au Mhujumu uchumi. Tunaaminishwa kuwa wala Rishwa au Ufisadi ni wale wote ambao hawako 'upande wa mpinga Rushwa na Ufisadi.'
Angekuwa ana nia njema na sio hii ya kutafuta sifa, angeimarisha Taasisi imara ila hiki anachokifanya ni anatengeneza mazingira ije kuonekana hakuna mtu anaweza kuyafanya ili...
Anawekeza kwenye MTU na sio TAASISI/SHERIA.