Uchaguzi 2020 Rais Magufuli na mafaniko ya miaka mitano mkoani Geita

Joined
Sep 8, 2020
Posts
67
Reaction score
133
Na Debora C. Kiyuga✍🏽

WhatsApp Image 2020-09-09 at 14.08.21.jpeg

Katika Sekta ya Madini, Serikali imeweza kudhibiti utoroshwaji wa Madini kwa kutunga Sheria ya kuyalinda na kuanzisha Soko kubwa la Madini. Kabla ya hapo Madini mengi yalikuwa yakitoroshwa nje ya nchi, Serikali ilikuwa haipati chochote na wananchi hawakuweza kufaidika na rasilimali hiyo.

Serikali imewezesha wachimbaji wadogo wadogo kwa Kuwatengea maeneo, Kufuta au kupunguza viwango vya Kodi walizokuwa wakilipa, kuwapatia mafunzo na mitambo ya kuendesha shughuli zao za uchimbaji.

Kumekuwa na ongezeko la mapato kwa wachimbaji wadogowadogo kutoka Mwaka 2016 ambapo waliuza dhahabu Kilo 337.482 yenye thamani ya shilingi bilioni 22.5 na kupelekea Serikali kupata Mrabaha wa shilingi bilioni 1.2 hadi kuuza dhahabu kilo 4,656.29 yenye thamani ya Bil 375.5 na kupelekea Serikali kupata Mrabaha wa shilingi bilioni 22.5 kwa mwaka 2019.

Kumekuwa na ongezeko la mapato kwa Wachimbaji wakubwa. Mwaka 2016 waliuza dhahabu kilo 17,587.15 yenye thamani ya Dola za Marekani Mil 607.3 sawa na shilingi tilioni 1.4, Serikali ilipata Mrabaha wa thamani ya Dola za Kimarekani Mil 23.4 sawa na shilingi bilioni 53.81. Hadi mwezi Mei, Mwaka 2020 wameuza Kilo 21,652.77 zenye thamani ya Dola za Kimarekani Mil 949.8 sawa na shilingi tilioni 2.2 na kutoa Mrabaha wenye thamani ya Dola za Kimarekani mil 56.8 sawa na shilingi bilioni 130.64.

Serikali imepanga kuimarisha mipango ya kuwawezesha wachimbaji wadogodogo ili wafanye shughuli zao kwa ufanisi na tija zaidi ikwemo Kuongeza maeneo na kuendelea kuwapatia Leseni, mafunzo, Mitaji na Teknolojia rahisi ili wafanye shughuli zao kwa tija na ufanisi Zaidi (Ilani ya Uchaguzi Uk 108-110).

Katika Sekta ya Utalii, Kwa miaka mingi Mkoa wa Geita ulikuwa na Hifadhi moja tu ya Rubondo, kwa Miaka Mitano iliyopita Serikali imeanzisha hifadhi nyingine ya Kimataifa ya Buligi- Chato ambayo ni ya tatu kwa ukubwa nchini Tanzania.

Katika Sekta ya Kilimo, ufugaji na Uvuvi kwa Miaka mitano iliyopita Serikali imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kufuta Tozo 114 kwa Wakulima, Wafugaji na Wavuvi. Katika kipindi kijacho Serikali imejipanga kutengeneza machinjio ya kisasa, kuendeleza na kujenga Maghala ya kuhifadhi na Vituo vya kuchakata mazao. (Ilani ya Uchaguzi Uk 33-56).

Katika Sekta ya Miundombinu Kwa miaka mitano iliyopita Serikali imejenga barabara zenye viwango vya Lami Km 123.27 zenye thamani ya Shilingi Bil 212.67. Miaka Mitano ijayo Serikali imejipanga kujenga barabara za Lami nyingi zaidi ikiwemo kukamilisha barabara ya kutoka Geita- Bukori- Kahama. (Ilani ya Uchaguzi Uk 61-95).

Katika Sekta ya Afya Miaka Mitano iliyopita Serikali imeendeleza ujenzi wa Hospitali za Rufaa za Kanda na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita. Aidha Serikali imejenga Hospitali nne za Wilaya.

index.jpg

Katika Sekta ya Elimu Serikali imejenga madarasa 1,539 katika Mkoa wa Geita, Shule za Sekondari 27 na nyumba za walimu 162. Aidha imeleta takribani shilingi bilioni 35.3 ya elimu bila malipo.

Serikali imefanikisha kupeleka umeme kwenye Vijiji 282 na kubakiza vijiji 116 tu. Kwa nchi nzima Serikali imepeleka umeme kwenye vijiji 9,570 na kubakiza takribani vijiji 2600. Kadhalika bei ya kuvuta umeme imeshuka hadi kufikia elfu 27 tu.

Katika sekta ya maji Serikali imetekeleza miradi mbalimbali ya maji na mji wa Geita umepangwa katika miradi mikubwa ya miji 28 itakayopatiwa maji ambapo mji wa Geita umetengewa shilingi bilioni 130.

Katika kupambana na umaskini Serikali imeleta Shilingi bilioni 29 kwa ajili ya kunusuru kaya maskini kupitia mradi wa TASSAF na imetenga bil 73.3 katika miaka inayokuja.

Katika Masuala ya jumla na ya kimataifa Tanzania imeweza kuongeza mapato, kutoka wastani wa shilingi bilioni 850 hadi shilingi Tilioni 1.5, Kuongeza makusanyo ya madini kutoka shilingi bililioni 160 hadi shilingi bilioni 528 mwaka 2019/2020. Kadhalika kuongeza makusanyo ya Halmashauri kutoka takribani shilingi bilioni 379 mwaka 2015 hadi shilingi bilioni 713.3 mwaka 2019/20.

Aidha Serikali imeongeza makusanyo ya Gawio kutoka Taasisi ambazo Serikali inazimiliki au ina hisa kutoka shilingi bilioni 161 mwaka 2014/2015 hadi shilingi tilioni 1.528 mwaka 2019/2020 kwa mwaka.

Kutokana na ongezeko la Mapato Bajeti ya Maendeleo ilipanda kutoka asilimia 26, mwaka 2015 hadi asilimia 40 mwaka 2020. Hivyo Serikali imewezesha kutekeleza miradi nchi nzima yenye thamani ya takribani shilingi tilioni 37.8. Miradi kama vile Stiglires Gauge, Reli ya Standard Gauge, Ununuzi wa ndege na kufufua reli ya Tanga, Arusha.

Serikali imetengeneza barabaraza zenye ukubwa wa zaidi ya KM 3,500 za barabara za Lami, Madaraja Zaidi ya 10 na inapanga kutengeneza madaraja takribani 8 likiwepo la Busisi na Sarenda na upanuzi wa bandari ya Tanga, Dar es salaam na Mtwara.

#MagufuliMitanotena
 
Baadhi ya Nukuu za Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika maeneo tofauti mkoani Geita

WhatsApp Image 2020-09-09 at 12.25.44(2).jpeg

WhatsApp Image 2020-09-09 at 12.25.44(1).jpeg

WhatsApp Image 2020-09-09 at 12.25.44.jpeg

WhatsApp Image 2020-09-09 at 12.25.45.jpeg

WhatsApp Image 2020-09-09 at 12.25.46.jpeg

WhatsApp Image 2020-09-09 at 12.25.47.jpeg

WhatsApp Image 2020-09-09 at 12.25.48.jpeg
 
Hakyamungu tukiendelea hivi kwa miaka kumi tutaomba kujiunga G8,
 
Hivi Chato si ipo Geita? Kama ndio basi Geita imepata mafanikio makubwa ie mbuga, uwanja wa ndege na mataa ya barabarani.
 
Magufuli anatupa somo Kali Sana Watanzania wote!

Kuohoji matumizi ya rasilimali pesa zetu endapo tukipata kiuongozi mkwapuaji!

Kuhoji pia kwamba, kabla yake, hizo pesa zoote zilizofanya yote haya leo, zilikuwa zinakwenda wapi?
 
Watwambie kwanza zile Trillion 450 ziliishia wapi .... badala ya kuhangaika na change za dollar million 300!!
 
Urais ni mtamu sana mpaka watu wazima kujitoa fahamu kisa....
 
Na Debora C. Kiyuga✍🏽

View attachment 1564210

Katika Sekta ya Madini, Serikali imeweza kudhibiti utoroshwaji wa Madini kwa kutunga Sheria ya kuyalinda na kuanzisha Soko kubwa la Madini. Kabla ya hapo Madini mengi yalikuwa yakitoroshwa nje ya nchi, Serikali ilikuwa haipati chochote na wananchi hawakuweza kufaidika na rasilimali hiyo.

Serikali imewezesha wachimbaji wadogo wadogo kwa Kuwatengea maeneo, Kufuta au kupunguza viwango vya Kodi walizokuwa wakilipa, kuwapatia mafunzo na mitambo ya kuendesha shughuli zao za uchimbaji.

Kumekuwa na ongezeko la mapato kwa wachimbaji wadogowadogo kutoka Mwaka 2016 ambapo waliuza dhahabu Kilo 337.482 yenye thamani ya shilingi bilioni 22.5 na kupelekea Serikali kupata Mrabaha wa shilingi bilioni 1.2 hadi kuuza dhahabu kilo 4,656.29 yenye thamani ya Bil 375.5 na kupelekea Serikali kupata Mrabaha wa shilingi bilioni 22.5 kwa mwaka 2019.

Kumekuwa na ongezeko la mapato kwa Wachimbaji wakubwa. Mwaka 2016 waliuza dhahabu kilo 17,587.15 yenye thamani ya Dola za Marekani Mil 607.3 sawa na shilingi tilioni 1.4, Serikali ilipata Mrabaha wa thamani ya Dola za Kimarekani Mil 23.4 sawa na shilingi bilioni 53.81. Hadi mwezi Mei, Mwaka 2020 wameuza Kilo 21,652.77 zenye thamani ya Dola za Kimarekani Mil 949.8 sawa na shilingi tilioni 2.2 na kutoa Mrabaha wenye thamani ya Dola za Kimarekani mil 56.8 sawa na shilingi bilioni 130.64.

Serikali imepanga kuimarisha mipango ya kuwawezesha wachimbaji wadogodogo ili wafanye shughuli zao kwa ufanisi na tija zaidi ikwemo Kuongeza maeneo na kuendelea kuwapatia Leseni, mafunzo, Mitaji na Teknolojia rahisi ili wafanye shughuli zao kwa tija na ufanisi Zaidi (Ilani ya Uchaguzi Uk 108-110).

Katika Sekta ya Utalii, Kwa miaka mingi Mkoa wa Geita ulikuwa na Hifadhi moja tu ya Rubondo, kwa Miaka Mitano iliyopita Serikali imeanzisha hifadhi nyingine ya Kimataifa ya Buligi- Chato ambayo ni ya tatu kwa ukubwa nchini Tanzania.

Katika Sekta ya Kilimo, ufugaji na Uvuvi kwa Miaka mitano iliyopita Serikali imechukua hatua mbalimbali ikiwemo kufuta Tozo 114 kwa Wakulima, Wafugaji na Wavuvi. Katika kipindi kijacho Serikali imejipanga kutengeneza machinjio ya kisasa, kuendeleza na kujenga Maghala ya kuhifadhi na Vituo vya kuchakata mazao. (Ilani ya Uchaguzi Uk 33-56).

Katika Sekta ya Miundombinu Kwa miaka mitano iliyopita Serikali imejenga barabara zenye viwango vya Lami Km 123.27 zenye thamani ya Shilingi Bil 212.67. Miaka Mitano ijayo Serikali imejipanga kujenga barabara za Lami nyingi zaidi ikiwemo kukamilisha barabara ya kutoka Geita- Bukori- Kahama. (Ilani ya Uchaguzi Uk 61-95).

Katika Sekta ya Afya Miaka Mitano iliyopita Serikali imeendeleza ujenzi wa Hospitali za Rufaa za Kanda na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita. Aidha Serikali imejenga Hospitali nne za Wilaya.

View attachment 1564211

Katika Sekta ya Elimu Serikali imejenga madarasa 1,539 katika Mkoa wa Geita, Shule za Sekondari 27 na nyumba za walimu 162. Aidha imeleta takribani shilingi bilioni 35.3 ya elimu bila malipo.

Serikali imefanikisha kupeleka umeme kwenye Vijiji 282 na kubakiza vijiji 116 tu. Kwa nchi nzima Serikali imepeleka umeme kwenye vijiji 9,570 na kubakiza takribani vijiji 2600. Kadhalika bei ya kuvuta umeme imeshuka hadi kufikia elfu 27 tu.

Katika sekta ya maji Serikali imetekeleza miradi mbalimbali ya maji na mji wa Geita umepangwa katika miradi mikubwa ya miji 28 itakayopatiwa maji ambapo mji wa Geita umetengewa shilingi bilioni 130.

Katika kupambana na umaskini Serikali imeleta Shilingi bilioni 29 kwa ajili ya kunusuru kaya maskini kupitia mradi wa TASSAF na imetenga bil 73.3 katika miaka inayokuja.

Katika Masuala ya jumla na ya kimataifa Tanzania imeweza kuongeza mapato, kutoka wastani wa shilingi bilioni 850 hadi shilingi Tilioni 1.5, Kuongeza makusanyo ya madini kutoka shilingi bililioni 160 hadi shilingi bilioni 528 mwaka 2019/2020. Kadhalika kuongeza makusanyo ya Halmashauri kutoka takribani shilingi bilioni 379 mwaka 2015 hadi shilingi bilioni 713.3 mwaka 2019/20.

Aidha Serikali imeongeza makusanyo ya Gawio kutoka Taasisi ambazo Serikali inazimiliki au ina hisa kutoka shilingi bilioni 161 mwaka 2014/2015 hadi shilingi tilioni 1.528 mwaka 2019/2020 kwa mwaka.

Kutokana na ongezeko la Mapato Bajeti ya Maendeleo ilipanda kutoka asilimia 26, mwaka 2015 hadi asilimia 40 mwaka 2020. Hivyo Serikali imewezesha kutekeleza miradi nchi nzima yenye thamani ya takribani shilingi tilioni 37.8. Miradi kama vile Stiglires Gauge, Reli ya Standard Gauge, Ununuzi wa ndege na kufufua reli ya Tanga, Arusha.

Serikali imetengeneza barabaraza zenye ukubwa wa zaidi ya KM 3,500 za barabara za Lami, Madaraja Zaidi ya 10 na inapanga kutengeneza madaraja takribani 8 likiwepo la Busisi na Sarenda na upanuzi wa bandari ya Tanga, Dar es salaam na Mtwara.

#MagufuliMitanotena

Yote ni ukhanithi kama hakuna demokrasia na Uhuru wa kweli. Udikteta haujawahi kushinda duniani.
 
Back
Top Bottom