tinkanyarwele
JF-Expert Member
- Dec 30, 2016
- 2,016
- 1,946
Mh, rais wa JMT tunakuomba uingilie kati bei ya Saruji au cement kama ilivyo zoeleka pamoja na vifaa vingine vya ujenzi. Mh Rais huku Missenyi Mkoani Kagera bei ya vifaa vya ujenzi iko juu sana kiasi cha kutisha nikilinganisha na baadhi ya maeneo hapa nchini, mfuko wa kg 50 wa saruji ya ujenzi wa kawaida unauzwa kati ya shilingi elfu 20 hadi elfu 21, huku nondo ya mm 12 ikiuzwa kati ya shilingi elfu 24 hadi elfu 25.
Nadhani tumekosa wa kutusemea juu ya hili lakini hali inatisha maana ni muda mrefu sasa hali ikiwa hivi, kwakuwa najua baadhi ya wahusika wamo humu naomba wasaidie kufikisha kadhia hii kwa mtukufu na wengine wote ambao wanaweza kusaidia kutatua hili.