Rais Magufuli, watu wanataka kurudi Misri Kanaani mbali sana

Britanicca,
Pole sana ndugu
 
Shida nyingine, huyu Musa wetu amekuwa mbishi wa kutii maelekezo ya muumba (wananchi na wataalam). Alipoambiwa apige jiwe ili maji yatoke wana wa Israel wapate maji, kwa hasira kapiga mara 3. Kwaajili ya kukosa utii, hataiona nchi ya ahadi.

Alitakiwa kurekebisha mfumo wa kodi yeye kaamua kuwaonea wananchi, kuwanyang'anya wananchi kidogo wakipatacho kupitia kodi.

Aliambiwa ajenge mfumo ambao utahakikisha matajiri hawatumii pesa zao kuwanyanyasa au kuwaonea wasio nacho, yeye kaamua kuwafanyia chochote (kuwaonea au kutowatendea haki) matajiri.

Aliambiwa ajenge mfumo utakaowahakikisha wakulima wanazalisha mazao yao na wanakuwa na uhuru wa soko, yeye kaja na kufungia uuzaji mazao nje na kufungua uuzaji mazao nje kwa namna anayoitaka. Leo kasababisha mahindi yauzwe gunia sh 15,000 mikoa ya nyanda za juu. Amewaua wakulima kiuchumi na kutengeneza uwezekano wa njaa miaka ijayo.

Aliambiwa aweke mfumo utakaosaidia kupunguza ajali za barabarani, yeye akaamua kuwafanya matrafiki kuwa idara mpya ya TRA ambayo furaha yao ni makusanyo ya pesa na siyo kupunguza na kuzuia uwezekano wa ajali.

Aliambiwa aendeshe nchi kwa kufuata katiba ili nchi iwe na utulivu na amani, yeye akakimbilia kufuta shughuli za kisiasa kwa vyama vingine vyote isupokuwa chama chake, akaamua kuzuia vyombo vya habari kutangaza shughuli za mihimili mingine na viambatabe naye kila mahali ili hata akikohoa vitangaze kuwa mtukufu leo kakohoa.

Tuliyokuwa nayo yalikuwa mabaya, tukajenga matarajio makubwa kwake, lakini hasira na kiburi cha huyu musa wetu, kinawafanya wana wa Israel wengi kufia jangwani. Ni nani wa kututengenezea nyoka wa shaba ili atakayeumwa na wadudu wauaji, amtazame, apate kupona?
 
Ccm hatimaye tutaongea lugha moja, kikwete alikuwa akitoa ajira kwa mwaka 1.2 M, huyu Mussa Feki wa farao hata ajira laki moja kwa miaka mitatu hajafikisha.
 
Huyu Musa Feki ni mwongo sana, anaamua kuwaibia waña wa Israel 1.5T kwa manufaa ya utawala wa farao.
 
Ila maliasili wana kodi za kiboya.yaani ukitaka kuuza mbao au mirunda.ukate kibali 260,000.kwa mwaka.
Ukitaka kushusha mzigo kibali 600, 000 kwa mwaka.yaani faida yote inakwenda kwao.wao wamekaa tu
Umeona kabisa
 
Hii Tamu angekuja hata Pascal Mayalla Au tindo wakaona
 
Ila maliasili wana kodi za kiboya.yaani ukitaka kuuza mbao au mirunda.ukate kibali 260,000.kwa mwaka.
Ukitaka kushusha mzigo kibali 600, 000 kwa mwaka.yaani faida yote inakwenda kwao.wao wamekaa tu
Turudi misiri
 
kwa miaka mitatu pekee Magufuli kajenga hospitali za wilaya na rufaa 72,kulinganisha na toka uhuru 1961 mpaka 2015,zilijengwa hospitali 60 tu.Kupanga ni kuchagua
 
kwa miaka mitatu pekee Magufuli kajenga hospitali za wilaya na rufaa 72,kulinganisha na toka uhuru 1961 mpaka 2015,zilijengwa hospitali 60 tu.Kupanga ni kuchagua
Nioneshe sentences au comment hata moja uliowahi kutoa kuonesha magufuli kakosea wapi, we kila siku kusifia
 
Jana ilikuwa siku ya MentalHealthAwarenessDay ilikuwa inamuhusu mtoa uzi kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…