Mitaa ya Mwembetogwa "maswala" ni vipipi vya mateja, kwa hiyo naweza kuwa naongea Kiswahili cha Mwembetogwa vile vile.
Unaongea Kiswahili cha Mwembetogwa ulipozungumzia hotuba ya Mkapa?
Kweli Mkapa arosto yeye na sera zake
Hiyo ni kasumba, si unaona hata wasanii wa bongo fleva wanaona shida kuimba Kiswahili matokeo yake wanaboronga na kiingereza cha hajabu. Kwa kifupi usishangae Mkapa kujifanya anajua sana kiingereza hii ni tabia yetu watanzania tunapenda sana sifa za kijinga.
Unapoandika "Unaongea Kiswahili cha Mwembetogwa ulipozungumzia hotuba ya Mkapa?"
Unakuwa hujaandika kiswahili chochote kinachojulikana.
Kiingereza pia ni lugha rasmi Tanzania. Swali linakuja, audience ya hiyo hotuba ilikuwa ipi? Ilikuwa ya Wajapani wengi na watu wa diplomatic corps za nchi mbalimbali walio Tanzania? Kama ni hivyo inawezekana Mkapa aliweka nyuma nationalistic pride kwa kutaka kuipa umuhimu practical issue ya kutaka kueleweka kirahisi zaidi na watu wengi.
Kama audience ilikuwa ya waTanzania ambao wengi wao hawajui kiingereza then swala la practicality linatoka, inaonekana labda kapendelea Kiingereza tu.
Tatizo la Mkapa hata akiongea Kiswahili kwa watu wa kawaida ataanza kuwaambia habari za "kuboresha wigo wa hadidu za rejea za asasi za washikadau kwenye mustakabali wa kukarafati miundombinu kama ilivyoainishwa na MKUKUTA", atawapoteza diplomats na Watanzania.
Balozi wa Japan kutoa hotuba Kiswahili ni moja kati ya njia za kidiplomasia kuonyesha heshima kwa Watanzania.
Wadau,
Majuzi hapa wakati wa-Japan wanakumbuka wenzao walipoteza hali, mali na nafsi katika tsunami ya mwaka uliopita Mh Rais Mkapa alikuwa ni katika wageni waalikwa ambao walikaribishwa jukwaani na kutoa hotuba. Balozi wa Japan hapa nchini alikuwa ni mwenyeji katika hafla hiyo pamoja na wageni wengine kadhaa.
Kilichonishangaza ni kuwa Raisi Mkapa alipokaribishwa jukwaani, alitoa hotuba yake kwa ki-ingereza(sijui kama ni english phobia au laa) wakati mwenyeji wa shughuli, balozi wa Japan, alitoa hotuba yake kwa Kiswahili.
Ni kwa mantiki hiyo nauliza swali hili je, mh sana Ben Mkapa ana nini na kiswahili chetu, hakipendi au ni vipi?
Nauliza nikiwa na kumbukumbu kuwa wakati fulani akiwa madarakani, alikwenda Addis Ababa kuhudhuria mkutano wa AU. Wakati huo AU ilikuwa imetoka kupitisha azimio la kuruhusu hotuba za wakulu kutolewa kwa kiswahili, mh Mkapa alichagua kutumia kingereza lakini Joachim Chissano akatumia kiswahili kwa muda wa kutosha na baadae ki-reno.
Hivi kuna aibu gani ya Rais Mmachinga, Mndengereko, Mchaga, n.k. akatumia kiswahili katika kutoa hotuba huko ughaibuni? Hivi pasi na juhudi za makusudi za wakiwemo watawala(usiseme viongozi maana hakuna njia wanayotuongoza kuipita), hiki kiswahili kitakuwa kweli.
Kuna lugha inaitwa Fursi...inaongewa na taifa moja tu duniani, Iran na bado Ahmadinejad anatamba nayo mpaka UN.
Hivi, ni kweli kuwa tumethubutu, tumeweza na tunasonga mbele au ni porojo za alinacha kama kawaida yetu.
Mitaa ya Mwembetogwa "maswala" ni vipipi vya mateja, kwa hiyo naweza kuwa naongea Kiswahili cha Mwembetogwa vile vile.
mkuu hii mwembetogwa ya wapi..Iringa au siyo? maeneo ya kule nyuma ya stendi na highland cinema, dah kweli wakati umekwenda.
Huyu keshakula chumvi nyingi, Mwembetogwa anayoizungumzia yeye ni pale Fire, Dar es Salaam :thinking:
Umezibuka wewe!
Unanikumbusha mbali sana enzi hizo wazee wazee kweli.Chaurembo akishika tama kila mtu shurti kumsikiliza. Chamgui akianza kukuhadithia habari za mtume utafikiri alikuwa naye katika safari zake. Changeda babu mwenyewe alishakuwa mzee sana, lakini akikuhadithia habari za mipambano wa Wajerumani Tanga vita vikuu vya kwanza, utafikiri Jemadari alikuwa yeye.
Tulikuwa tunakula kashata na kunywa kahawa na Juliasi pale, enzi hizo kijana mdogo tu, haongei sana, anavaa kaptura bado ana kasumba za Kiskochi na UFabiani. Tukamwambia "Juliasi, wewe umetoka shamba ukaenda Uskochi moja kwa moja, habari za hapa Mwembetogwa wanaovaa vikaputura ni watoto wadogo tu" basi nusura tugombane pale.
Na kuanzia siku hiyo Juliasi akahama mpaka na kikao, akawa mtu wa kukaa sana New Street na hatimaye Magomeni. Lakini New Street tulijua kuna shughuli za siri zikiendelea, badaye sana ndiyo tukajua mambo ya harakati za uhuru.
Ujumbe aliupata, maana vikao vyote vya bao na kina Abdulwahid kuanzia siku hizo mpaka siku za bao la Baba Wandema Msasani Juliasi hakuvaa vikaputula tena, alipoulizwa akadai Dar-es-salaam mbu wamezidi. Huku akicheka kwa bashasha kuonyesha utani mwingi.
Mwembetogwa ya Iringa nilifika siku zile walipomuua yule mwalimu mkuu pale, lakini ninayoiongelea mie ni hii ya pale panapoiwa "Faya".
I'm just messsing with y'all.
Mjini Magharibi na Mrima wapi na wapi?
Ukitaka hivyo hata "Swali" badilisha ufanye "suali" na maadamu tunaongelea hili, hata jina lenyewe la lugha liwe Ki-suahil.
Mzizi wa swali na swala ni mmoja, habari za "suala" ni kukiarabisha Kiswahili. Na mie kama mtu ninayeamini kiarabu hakina hati pekee ya ugavi wa Kiswahili (au Kisuahil ?) na Kimang'ati nacho kina cha kuchangia, naondokana na hizo habari za kwamba "suala" ni sahihi zaidi ya "swala".
Nakataa kwamba Kiswahili kinatakiwa kukikumbatia kiarabu kuendelea mbele ili kiwe na maana, na kusema kwamba "swala" si sahihi bali "suala" ni sahihi, ni kukinyima Kiswahili sifa yake kubwa ya kuwa lugha ya kisikio (phonetic language).
Kama kamusi yako inasema "swala" siyo sawa na "suala" ndiyo sawa hata yenyewe haiko juu ya darubini ya Kiranga. Kamusi zinakosea nazo, au maneno yanabadilika, ndiyo maana unaona matoleo yanabadilika.
Katika kuendeleza lugha ya Kiswahili, tujitahidi sote kuepuka makosa yanayoonekana kuzoeleka
Swala =Suala
Swali= Suali