Rais mpya wa TFF, Karia aanza kwa mkwara mzito

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
Muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi wa nafasi ya uraisi katika Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), Wallace Karia alipewa nafasi ya kutoa neno kwa familia ya soka.

Karia ambaye aliibuka na ushindi wa kishindo katika uchaguzi huo, aliapishwa muda mfupi baada ya kutangazwa kwa matokeo ikiwa ni utaratibu mpya, kisha akapata nafasi ya kutoa hotuba kwa ajili ya wanasoka.

Akizungumza huku akionekana kujiamini, Karia alisema huu ni muda wa kupambana na kushikana kuwa wamoja ili kupeleka mbele mchezo wa soka.

Karia ameonyesha kuwa mkali na kutotaka utani katika uongozi wake ambapo amesisitiza umakini na watendaji wake kufuata mipango ambayo watakuwa wkaiipanga kwa faida ya soka la nchi ya Tanzania.

Amesema kuanzia sasa hataki ubabaishaji kwenye soka, ameeleza kuwa anataka watu ambao wapo makini kwenye kazi, hao ndiyo ambao atafanya nao kazi.
Aidha, amemshukuru Waziri Harrison Mwakyembe ambaye alikuwemo kwenye mchakato wa uchaguzi mwanzo hadi mwisho mkoani Dodoma, kwa kusema kuwa TFF itafanya kazi pamoja na serikali kwa kuwa imeonyesha nia ya kuwasaidia na imekuwa na TFF bega kwa bega.

Chanzo: Salehe Jembe
 
biti tu mbona alvokuw na malinzi hakuwa mkal

Sent using Jamii Forums mobile app from my Android phone
 
Katika watu ambao tumelamba garasa ni huyu jamaa yaani TFF alitakiwa kupewa Ally Mayai...

Sio hawa wachumia tumbo wala wasioujua Mpira.....

Sijui ni kwa vile Ally Mayai hana pesa za kuhonga wajumbe .....
Ndo hivyo hivyo mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…