Rais mpya wa TFF, Karia aanza kwa mkwara mzito

Nchi systems ndio zinatuua kuanzia sekta binafsi, serikalini mpaka TFF kama haupo ktk system hata uwe unajua vipi hupewi nafasi na ndicho kilichomkuta Ali mayay tembelea sio kwamba hajui tatizo hayupo ktk system, ila mwenzake karia systems imembeba na yy ana kazi ya kurudisha fadhila kwa walio mbeba, sasa usishangae Ruta akapewa tena mshauri wa maswala ya ufundi wa Rais, wakati hajawahi kucheza mpira hata wa mtaani wala kuhudhuria kozi yoyote (namjua nje ndani Ruta) huku wakiwaacha akina kibadeni wanaojua maswala ya ufundi. Subirini muone hizo kamati zitakazoundwa, hazitozingatia uweledi bali ni za kulipana fadhila. Mpira wa Tanzania ujanja mwingi, jpili ndugu zangu simba wamepelekwa pelekwa na wakaambiwa hamna kuuliza maswala ya mapato na matumizi, huku ajenda kumi na nne zikijadiliwa ndani ya masaa manne si upuuzi huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…