Rais mstaafu Dr. Kikwete ajitolea kumsaidia Mzee Majuto matibabu India, pia kumnunulia trekta la kilimo

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
16,515
Reaction score
28,506


LICHA ya kufanyiwa upasuaji wa tezi dume bado hali ya staa wa filamu za Kibongo, Amri Athuman ‘Mzee Majuto’ ni tete ambapo Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK’, amejitosa baada ya kumuona alivyodhoofu kwa sasa.

JK na Mzee Majuto walikutana uso kwa uso wikiendi iliyopita katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar katika Tuzo za Kimataifa za Sinema Zetu ambapo walionekana wakiteta kwa dakika kadhaa kabla ya kila mmoja akaenda kukaa kwenye siti yake.

Hali ya mzee Majuto haikuonekana nzuri na alionekana ukumbini akitembea kwa msaada wa fimbo huku akionekana kutokuwa mchangamfu kama ilivyo kawaida yake, hali iliyowahuzunisha mashabiki wake waliokuwa ukumbini hapo.

Baada ya mazungumzo hayo Mzee Majuto amesema kuwa, kutokana na hali yake kutokuwa nzuri licha ya kufanyiwa upasuaji, Muheshimiwa JK amemuahidi kwamba watajadili na Rais Magufuli na ili wampeleke India kwa matibabu zaidi kwani tiba za hapa hajaridhishwa nazo.

“JK ameniahidi kwamba watanipeleka India kwa ajili ya matibabu ikiwa ni baada ya kwenda na kujadili na rais aliyeko madarakani Dk John Pombe Magufuli ‘JPM’ ili nikapate matibabu zaidi maana tiba nilizopatiwa hapa bado sijakaa sawa.

“Kwanza kwa sasa nimepatwa ugonjwa mpya tena ambapo mkono unaniuma mno, ninashindwa hata kushika chochote ndiyo nataka nirudi tena hospitalini nikawaeleze kuhusu hilo maana hali siyo nzuri kabisa,” alisema Mzee Majuto.

Hata hivyo, Mzee Majuto alisema kuwa, pamoja na hilo, JK amemuahidi kwamba atamnunulia trekta kwa ajili ya kulima kwenye mashamba yake ambako atapanda minazi huko Tanga ili aweze kuendesha maisha.

Source: GPL
 
Hongera Mh kwa msaada maana madhara yake unayajua
 
Majuto hajawah kuwa serious..
Sasa minazi ukipanda leo unataka ulinde mipaka ya shamba?
 
Pole kwake na asante JK.

Sasa hiyo minazi itakuja kumpa faida lini na umri wote huo?

Trekta awe anakodisha apate pesa za kujikimu. Pia alime mashamba ya mazao ya muda mfupi.
Alime mananasi huyu mzee yatamtoa kuliko minazi..... Au anataka kugema Tembo?
 
Jk kasema atajadili na Magu manaa hilo trekta majuto kamwambia anataka kulimia minazi ya kulinda mipaka ya Kenya na tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…