Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kuhudhuria harusi ya Alikiba jijini Nairobi Kenya

Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kuhudhuria harusi ya Alikiba jijini Nairobi Kenya

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,587
Ndoa ya mwanamuziki Alikiba na mchumba wake Amina inatarajiwa kufungwa kesho alfajiri katika msikiti wa Ummul Kulthum ulioko eneo la Kizingo jijini Mombasa.


Mama wa bibi harusi mtarajiwa, Bi Asma Said anasema ndoa hiyo itafungwa katika msikiti huo uliojengwa na Gavana wa Mombasa, Hassan Joho.
Anasema baada ya ndoa kufungwa itafuatiwa na sherehe ya kupambwa bibi harusi ambayo itafanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini humo.


Miongoni mwa watu mashuhuri wanaotarajiwa kuhudhuria harusi hiyo ni Rais wa Awamu ya nne, Jakaya Kikwete na Ommy Dimpoz.



Akizungumza na Mwananchi Bi Asma anasema maandalizi yanaendelea vizuri na nyumbani
kwa bibi harusi mwandishi alishuhudia wanawake wakiwa wanajipamba huku wengine wakijipaka henna.



Alibainisha kuwa tayari bwana harusi ameingia nchini Kenya huku wadokezi wakisema kuwa Alikiba alikuwa katika hoteli ya English Point Marina ambapo ni karibu na nyumba ya bibi harusi iliopo eneo la Kongowea.



“Kijana ametoka Tanzania na kuja kuoa Kenya mimi sikujua kama mtoto wangu ataolewa na Alikiba lakini Mungu ndio aliyepanga,” akasema Bi Asma.
 
Kwa hiyo hawa wadada wa kibongo ni kwa matumizi ya kutafunwa tu! Hata hivyo sio mbaya kwa kuwa ndio maisha waliyo yachagua.....
 
Sijawahi kufikiria kuoa mwanamke wa nchi nyingine, bora nioe mtoto wa mama tukinao Kule kwa Mtogole tugawane umaskini
 
Huyu mzee kupenda kwake bata nakuwekeza rasilimal ktk mambo yakijingajinga ndiko kulikotufikisha hapa kama Taifa
 
Mfano mimi nanufaika na nini kwenye harusi hiyo?


Nafikiri hilo jambo no binafsi sana sio habari kubwa kama unavyotaka kutufanya tuamini.
 
Huu ujinga ni news? Kweli? Ujinga ni mzigo wa kinyesi.
 
Back
Top Bottom