Rais Mstaafu Kikwete aongoza harambee kuchangia gharama za matibabu ya Moyo kwa Watoto wanaotoka Familia Maskini. Zaidi ya billion 2.7 zapatikana

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ametoa wito kwa taasisi na watu binafsi wenye nia njema kujitokeza na kuchangia matibabu ya watoto wenye matatizo ya moyo kutoka familia zisizo na uwezo ili kuwaondolea au kupunguza mateso yanayosababishwa na maradhi hayo.

Dkt. Kikwete alitoa wito huo Jumamosi usiku wakati wa harambee aliyoongoza kuchangia gharama za matibabu ya watoto hao, iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Heart Team Africa Foundation (HTAF) katika hoteli ya Joihari Rotana, jijini Dar es Salaam.

Rais Mstaafu, ambaye ni mlezi wa watoto wanaohitaji matibabu ya moyo, alieleza kuwa lengo kuu la harambee hiyo ni kuchangisha asilimia 30 ya gharama zilizobaki za matibabu, kwani asilimia 70 ya gharama hizo huchangiwa kila mwaka na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

"Naishukuru serikali kwa kuchangia asilimia 70 ya gharama zote za matibabu ya wagonjwa hao. Hata hivyo, asilimia 30 iliyobaki, ambayo familia ya mgonjwa inapaswa kuchangia, bado ni mzigo mzito kwa familia nyingi. Wanahitaji kusaidiwa," alisema.

Alieleza kuwa kuna watoto 1,500 kutoka familia zisizo na uwezo ambao wamesajiliwa JKCI wakisubiri matibabu ya haraka ili kuokoa maisha yao. Bila matibabu hayo, watoto hawa wanakabiliwa na hatari kubwa ya kupoteza maisha.

"Nawashukuru sana wadau wote waliochangia katika harambee hii ambapo hadi sasa kiasi cha shilingi 2,718,525,000/= kimepatikana. Kiasi hiki kitawezesha kugharamia matibabu ya watoto 500 ambao wanahitaji huduma ya haraka," aliongeza Rais Mstaafu.

Akitoa shukurani za pekee kwa Benki ya NMB kwa mchango wake wa shilingi bilioni moja, aliomba taasisi zingine ziige mfano huu si tu kwa kuwasaidia wagonjwa, bali pia kwa kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita katika kupunguza au kutatua tatizo hilo.

Pia aliipongeza na kuishukuru taasisi ya kimataifa ya BAPS Charities tawi la Tanzania kwa mchango wake wa dola za Kimarekani laki nne (takriban shilingi 1,078,674,800), pamoja na Benki ya CRDB kwa kuchangia zaidi ya shilingi milioni 700 katika vipindi tofauti huku ikiahidi kuendelea na zoezi hilo kila mwaka.

Rais Mstaafu aliwashukuru pia wadau wote waliojitokeza kwenye hafla hiyo kwa kuchangia pesa na wengine kutoa ahadi, akiwaomba kila mmoja wao kuheshimu ahadi aliyotoa ili kufanikisha zoezi zima la kuwaokoa watoto hao wenye matatizo ya moyo.

Dkt. Kikwete pia aliishukuru Serikali ya Awamu ya Tano na ya Sita kwa kuendelea kuwekeza kwenye vifaa vya kisasa katika JKCI na kuleta madaktari bingwa, jambo ambalo limeiongezea uwezo JKCI wa kuhudumia Watanzania wenye maradhi ya moyo.

Alitumia hafla hiyo pia kumtambulisha Prof. David Mwakyusa, ambaye alisema akiwa Waziri wa Afya, yeye na timu yake ya wataalamu aliyoiongoza walitoa mchango mkubwa katika kuanzishwa kwa Taasisi ya JKCI mwaka 2015.

Mwenyekiti wa HTAF, Mhe. Mussa Hassan Zungu, ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amemshukuru Rais Mstaafu kwa kubuni na hatimaye kuanzisha Taasisi ya JKCI, ambayo kwa sasa ni ya tatu kwa ubora barani Afrika, ikifuatia kwa karibu taasisi kama hizo za Misri na Afrika Kusini.

Mhe. Zungu alieleza kuwa uwepo wa JKCI umepunguza kwa kiwango kikubwa gharama za matibabu ya wagonjwa wa moyo, kwani uwepo wa taasisi hiyo umewezesha matibabu yaliyokuwa yakipatikana India na nchi zingine kwa gharama kubwa, sasa kupatikana hapa nchini na kwa ubora uleule wa huduma za nje.

Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI katika risala yake alisema hivi sasa taasisi hiyo imefikisha uwezo wake wa kutoa huduma kwa kiwango cha asilimia 90, na kwamba ina madaktari bingwa wazawa 50 na wa kawaida zaidi ya 40 wanaotoa huduma za kisasa.

Chanzo cha habari hii ni :Issa Michuzi
Screenshot_20241103-184248_1.jpg
 
Alikuwa na uwezo wakuweka mazingira ya vyanzo vya kupatikana hela kama hizo bila kutembeza bakuli.

Yes, leo kapata kiasi hicho, itakuwaje siku akiwa hayupo duniani ?
 
Nimeona JK amewasifia sana Wanyakyusa wenye Mbeya yao na kusema Prof Mwakyusa alikuwa na Msaada mkubwa kwenye Serikali yake

Ikumbukwe kwenye Serikali ya Kikwete Mawaziri wa Mbeya Walikuwa Prof Mwakyusa, Prof Mwandosya na Dr Mwakyembe

Mbeya mjini mlitisha sana 😂😂😂
 
Ingekua rahisi hivy, nyerere angejenga sgr, hospital kama muhimbili nchi nzima,lami nchi nzima,stiglers gorge, irrigation schemes nchi nzima...punguzeni ujinga
 
Alikuwa na uwezo wakuweka mazingira ya vyanzo vya kupatikana hela kama hizo bila kutembeza bakuli.

Yes, leo kapata kiasi hicho, itakuwaje siku akiwa hayupo duniani ?
Wataendeleza wengine mahali alipoishia yeye. Yeye ameanzisha na wengine watafuata na wala yeye peke yake hawezi kufanikisha na ndio Maana anawashirikisha watu na taasisi mbalimbali.
 
Nimeona JK amewasifia sana Wanyakyusa wenye Mbeya yao na kusema Prof Mwakyusa alikuwa na Msaada mkubwa kwenye Serikali yake

Ikumbukwe kwenye Serikali ya Kikwete Mawaziri wa Mbeya Walikuwa Prof Mwakyusa, Prof Mwandosya na Dr Mwakyembe

Mbeya mjini mlitisha sana 😂😂😂
Kwamba Tulia.....
 
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ametoa wito kwa taasisi na watu binafsi wenye nia njema kujitokeza na kuchangia matibabu ya watoto wenye matatizo ya moyo kutoka familia zisizo na uwezo ili kuwaondolea au kupunguza mateso yanayosababishwa na maradhi hayo.

Dkt. Kikwete alitoa wito huo Jumamosi usiku wakati wa harambee aliyoongoza kuchangia gharama za matibabu ya watoto hao, iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Heart Team Africa Foundation (HTAF) katika hoteli ya Joihari Rotana, jijini Dar es Salaam.

Rais Mstaafu, ambaye ni mlezi wa watoto wanaohitaji matibabu ya moyo, alieleza kuwa lengo kuu la harambee hiyo ni kuchangisha asilimia 30 ya gharama zilizobaki za matibabu, kwani asilimia 70 ya gharama hizo huchangiwa kila mwaka na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

"Naishukuru serikali kwa kuchangia asilimia 70 ya gharama zote za matibabu ya wagonjwa hao. Hata hivyo, asilimia 30 iliyobaki, ambayo familia ya mgonjwa inapaswa kuchangia, bado ni mzigo mzito kwa familia nyingi. Wanahitaji kusaidiwa," alisema.

Alieleza kuwa kuna watoto 1,500 kutoka familia zisizo na uwezo ambao wamesajiliwa JKCI wakisubiri matibabu ya haraka ili kuokoa maisha yao. Bila matibabu hayo, watoto hawa wanakabiliwa na hatari kubwa ya kupoteza maisha.

"Nawashukuru sana wadau wote waliochangia katika harambee hii ambapo hadi sasa kiasi cha shilingi 2,718,525,000/= kimepatikana. Kiasi hiki kitawezesha kugharamia matibabu ya watoto 500 ambao wanahitaji huduma ya haraka," aliongeza Rais Mstaafu.

Akitoa shukurani za pekee kwa Benki ya NMB kwa mchango wake wa shilingi bilioni moja, aliomba taasisi zingine ziige mfano huu si tu kwa kuwasaidia wagonjwa, bali pia kwa kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita katika kupunguza au kutatua tatizo hilo.

Pia aliipongeza na kuishukuru taasisi ya kimataifa ya BAPS Charities tawi la Tanzania kwa mchango wake wa dola za Kimarekani laki nne (takriban shilingi 1,078,674,800), pamoja na Benki ya CRDB kwa kuchangia zaidi ya shilingi milioni 700 katika vipindi tofauti huku ikiahidi kuendelea na zoezi hilo kila mwaka.

Rais Mstaafu aliwashukuru pia wadau wote waliojitokeza kwenye hafla hiyo kwa kuchangia pesa na wengine kutoa ahadi, akiwaomba kila mmoja wao kuheshimu ahadi aliyotoa ili kufanikisha zoezi zima la kuwaokoa watoto hao wenye matatizo ya moyo.

Dkt. Kikwete pia aliishukuru Serikali ya Awamu ya Tano na ya Sita kwa kuendelea kuwekeza kwenye vifaa vya kisasa katika JKCI na kuleta madaktari bingwa, jambo ambalo limeiongezea uwezo JKCI wa kuhudumia Watanzania wenye maradhi ya moyo.

Alitumia hafla hiyo pia kumtambulisha Prof. David Mwakyusa, ambaye alisema akiwa Waziri wa Afya, yeye na timu yake ya wataalamu aliyoiongoza walitoa mchango mkubwa katika kuanzishwa kwa Taasisi ya JKCI mwaka 2015.

Mwenyekiti wa HTAF, Mhe. Mussa Hassan Zungu, ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amemshukuru Rais Mstaafu kwa kubuni na hatimaye kuanzisha Taasisi ya JKCI, ambayo kwa sasa ni ya tatu kwa ubora barani Afrika, ikifuatia kwa karibu taasisi kama hizo za Misri na Afrika Kusini.

Mhe. Zungu alieleza kuwa uwepo wa JKCI umepunguza kwa kiwango kikubwa gharama za matibabu ya wagonjwa wa moyo, kwani uwepo wa taasisi hiyo umewezesha matibabu yaliyokuwa yakipatikana India na nchi zingine kwa gharama kubwa, sasa kupatikana hapa nchini na kwa ubora uleule wa huduma za nje.

Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI katika risala yake alisema hivi sasa taasisi hiyo imefikisha uwezo wake wa kutoa huduma kwa kiwango cha asilimia 90, na kwamba ina madaktari bingwa wazawa 50 na wa kawaida zaidi ya 40 wanaotoa huduma za kisasa.

Chanzo cha habari hii ni :Issa MichuziView attachment 3142754
Naona kama ni upuuzi tupu.

Je, suala la Bima ya Afya kwa wote limeishia wapi mpaka huyo JK anaamua kuendesha harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya matibabu ya hao watoto?
 
Back
Top Bottom