Kenyan
JF-Expert Member
- Jun 7, 2012
- 414
- 314
Familia ya Kenyatta inakadiria hasara ya bilioni 1.2 pesa za Tanzania (sawa na milioni 70 za Kenya) kufuatia uvamizi wa shamba lake na watu wasiojulikana hapo Jana.
Wavamizi waliiba kondoo zaidi ya 1,400 aina ya Dorper mchana peupe, ambapo kondoo mmoja aina ya Dorper huuzwa kwa takriban tsh 800,000 nchini Kenya.
Kondoo hao wenye asili ya Afrika Kusini, hukua kwa haraka hata katika maeneo kame, na wanafaa zaidi kwa nyama yao ambayo ina sifa ya kuwa nyororo.
Kwa sasa shamba hilo lililoko eneo la Ruiru barabara ya kwenda Thika lipo chini ya ulinzi mkali wa maafisa wa polisi.