Rais mstaafu wa Pakistani ahukumiwa kifo katika kesi ya uhaini mkubwa na kukiuka Katiba

Musharraf hawezi kunyongwa,Jeshi limefuatilia kwa makini hii kesi sababu ni mtu wao. Na ijulikane kuwa Pakistan inaendeshwa kwa Jeshi indirectly kama ilivyo Misri. Na Jeshi lao washatoa tamko kuwa haiwezekani mtu alietumikia Jeshi la Pakistan miaka 40 akawa Mkuu wa Majeshi na Rais wa Nchi akawa Msaliti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toka Maktaba :

Kiongozi wa kijeshi wa Pakistani 1999-2013 Jenerali Musharraf. Video ya majumuishi ya matukio wakati Jenerali Musharraf akiwa madarakani na baada ya kutoka mamlakani

Source : VOA news
 
December 16, 2019
Rawalpindi, Pakistan

Jenerali Pervez Musharraf akiwa Dubai anaendelea na matibabu katika hospitali iliyoko katika Falme za Kiarabu, huku Mahakama Kuu ya Pakistani ikitibitisha hatia na kutoa hukumu ya juu kabisa kutokana na makosa yake Jen. Musharraf wakati alipokuwa kiongozi wa Pakistani.

Source: WION
 
very interesting,nimeisoma yote.
 
Habarini Wadau,

Leo nimeshangazwa na hii habari inayosambaa Twitter kuwa aliyekuwa Rais wa Pakistan PERVEZ MUSHARRAF amehukumiwa kifo kutoka katika mahakama kuu ya nchi hiyo.

Hiyo ni kutokana na kubadilisha katiba na kuingiza vifungu vya dharura vitakavyoongeza muda wake madarakani.

Binafsi nilifikiri Marais wote wakifanya udikteta na kunyanyasa watu, kupiga watu, kunyang'anya mali za watu, kufilisi watu na hata kutapanya pesa za serikali hawawezi kuchukuliwa hatua yoyote.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama kuna siku itathibitika Ben Sanane na Azory waliuawa, waliohusika wote, kuanzia waliotoa maelekezo mpaka watekelezaji, waionje adhabu hiyo.

Uhai wa binadamu yeyote una thamani sawa, bila ya kujali ni mwananchi wa kawaida, RC, TISS, Polisi, Waziri au Rais.

Kuna siku Dunia itakuwa ni mahali pema. Ni wakati ambapo mifumo ya Dunia itazuia udikteta, uonevu na ubaguzi kutendeka mahali popote Duniani, na kinga zote zitaondolewa na maamuzi ya Dunia pale ambapo watawala watakuwa waliamrisha mauaji, mateso, ugandamizaji haki au ubaguzi.
 
Huyo Court Chief Justice ni kiboko
Anasema anyongwe kwa kila kosa na maiti itundikwe mbele ya jengo la bunge kwa siku tatu
Huyo ndio Chief Justice wa huko



Sent from my iPhone using Tapatalk
Kwa ninavyozijua siasa za Pakistan,sitashangaa nikisikia huyo Court Chief Justice akipigwa shaba au bomu la kujitoa Muhanga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…