Hebu tuangalie kidogo hoja zilizotolewa na niweza kuona uzito wake:
a. Watu wanamshabikia Obama kwa sababu ya chuki yao dhidi ya sera za Rais Bush.
Hili linashangaza. Sera za Bush kuhusu nchi gani? Hakuna Rais wa Marekani aliyefanya mengi kwa Tanzania na Afrika kuliko Rais Bush. Kwa kila hali. Siyo Carter wala siyo Clinton ambao wameipa Afrika nafasi ya kufanikiwa kuliko alivyofanya Rais Bush.
Tukiwauliza mashabiki wa Obama wa Tanzania kwamba ni kitu gani ambacho Bush amekifanya kwa Tanzania ambacho kinawafanya wamchukie Bush na wampende Obama?
Ndio maana kati ya majibu mazuri ambayo JK amewahi kutoa ni pale alipoulizwa na media wakati Bush amekuja nyumbani kuwa ni mgombea gani Tanzania ingempendelea ashinde huko Marekani. Yeye alijibu na kusema "yeyote yule kwa kadiri ya kwamba atakuwa kwetu Afrika kama alivyokuwa Rais Bush". Huu ni ukweli.
Hatujauliza hivi Obama ana sera gani kuhusu Afrika? Mwenye jibu aseme lakini sera ya Bush inajulikana na imeonekana. Sioni dalili yoyote kuwa Obama atakuwa zaidi ya Bush kwa Afrika. So hii chuki ya Bush ni wazi haihusiani na sera za Bush kwa bara letu kwani sera zake zimetupa nafasi ya kufanikiwa, nafasi ya kupiga hatua katika mambo mbalimbali. Leo hii Tanzania inapokewa watalii wengi zaidi kutoka Marekani kuliko wakati mwingine wowote, vijana wetu wengi wamepata nafasi ya kuja Marekani kwa urahisi zaidi kuliko wakati mwingine wowote wa mahusiano ya Tanzania na Marekani. Leo hii kuna miradi kadhaa ya hali ya juu ambayo imefadhiliwa na USAID.
Nina bahati ya kupata daily press releases kutoka Ubalozi wa Marekani Dar na ninajua kwa hakika ni mambo mangapi yanafanywa na Marekani kuipa Tanzania nafasi. Hii haikuwa hivyo wakati wa Clinton (a Democrat) na nathubutu kusema haitakuwa hivyo chini ya Obama.
b. Angalia mataifa mengine yanavyomshabikia Obama, haiwezekani kuwa ni kwa sababu ya rangi, uliona umati wa watu kule Ujerumani?
Hii inashangaza. Haitakuwa mara ya kwanza kwa watu weupe kujitokeza kumshangaa mtu mweusi ambaye anaonekana kutofit "the stereotype". Lakini hapa kuna kitu kingine pia. Ni kweli kuna wale ambao wanamshabikia Obama kwa sababu ya mlengo wake wa kushoto wa kiliberali. Obama anaendana na mwelekeo huo wa kiliberali ambao leo hii unaonekana katika misingi ifuatayo:
a. Kupunguza nguvu ya Jeshi la Marekani duniani
b. Kusababisha redistribution of wealth to the so called middle class (a.k.a the workers)
c. Mwelekeo wa kisoshalist mambo leo (neo-socialism) ambapo hawafuati ukomunisti wa kina Max, Juche au Lenin bali wanafuata ile "njia ya kati" kama ilivyo katika nchi za Uskandinavia, Hispania, na Australia. Hii wenyewe wanaiita "social capitalism".
d. Kueneza wazo la "haki" za mtu mmoja mmoja katika masuala ya ndoa za ushoga, utoaji mimba, n.k
e. Kuongeza nguvu za mamlaka ya serikali katika sekta binafsi na hivyo kutaka kutoza kodi kubwa kwa matajiri na kodi ndogo au kutotoza kodi kwa watu wa kipato cha chini na hivyo kuadhibu matajiri na watu waliofanya kazi kujenga maisha yao.
f. Kupunguza clout (ujiko) wa Marekani katika nguvu za uchumi na hivyo kuufanya ulimwengu uwe sawa. Kimsingi kujaribu (kama alivyosema bi. Albright) kupunguza the Super Power status of America. Kwamba kuwa na Super Power mmoja duniani si vizuri.
n.k n.k
Sasa baadhi ya hawa wanaomshabikia Obama ni kwa sababu ya mwelekeo huo.
c. Obama atabadilisha sera za Bush hususan katika nchi za mapigano za Iraq na Afghanistan na hivyo kufanya America ipendwe.
Mojawapo ya vitu ambavyo yawezekana watu wengi hawajavipata vizuri ni kuwa historia haiwatendei haki watu walio so liberal kama Obama. Bahati nzuri tuna mfano mzuri wa dovish president wa Marekani Bw. Jimmy Carter ambaye chini ya uongozi wake na nia yake ya kuifanya Marekani kuwa "kama nchi nyingine tu" na kushinda kuchukuua maamuzi magumu wakati wa Mgogoro wa Irani (1979) kumefanya watu waone ulinganifu kati yake na Obama.
Lakini itakuwa makosa makubwa kwa watu kudhania kuwa Obama akiwa Rais basi mwangaza mpya wa amani utatokea duniani. Obama atakula kiapo kile kile alichokula Bush na jukumu lake la kwanza na la pekee ni kwa nchi ya Marekani.
Rais Obama hatosita kutumia nguvu zote za Taifa hili kukabiliana na tishio lolote lile. Kama Iran, Syria, North Korea au nchi yeyote inafikiri itaweza kumpiga mkwara Obama na kuwa Obama atakaa chini na maghaidi kuzungumza nchi hiyo itafanya makosa. Obama hatosita kutumia the fully military mighty of the States na sitakuwa wa kwanza kushangaa nikiona na yeye picha yake na mfano wake (effigy) ikichomwa moto na kumuita yeye "Shetani Mkuu"!
Anayefikiri kuwa utawala wa Marekani chini ya Obama linapokuja suala la kimataifa itakuwa ni tofauti sana na ya Bush mtu huyo haelewi sentiments za Wamarekani kuhusu Taifa lao.
Hivyo, kudhania kuwa Obama akiwa Rais vita Iraq na Afghanistan zitakoma na ya kuwa Marekani itasita kutumia majeshi au vikosi vyake sehemu yoyote duniani ni naivette of the first class.
d. Huu ni uchaguzi wa kihistoria na ndio maana watu wengi wanafuatilia.
Hili ni kweli kabisa na binafsi sisemi ni vibaya kwani nami ni shabiki wa historia. Ninaona fahari kuishi wakati huu kuweza kuona tunachokiona. Macho yetu bila ya shaka hayatakaa kuona nafasi kama hii tena (hasa kama Obama atashinda) kwani kutokuangalia rangi kwenye uchaguzi huu ni kutokuwa wa kweli.
Obama angekuwa mtu mweupe wala asingefika hapa alipofikia. Kama angekuwa mtu mweupe mahusiano yake na kina Ayers, Rev. Wright yasingempa hata nafasi. Ile siku ambapo video ya Wright ilipotoka na kuoneshwa kuwa huyo ndiye alikuwa mchungaji wake na ya kuwa alionekana naye kwa hakika siyo tu angejitenga naye angetakiwa kudrop. Lakini kwa vile ni mweusi na yule mchungaji ni mweusi watu waliliweka pembeni maana kulipigia kelele ingeonekana kuwa ni "racist".
Obama angekuwa mweupe kauli zake kadhaa huko nyuma na kutokuwa na rekodi ya kuonesha utendaji zisingempa nafasi yoyote ile. Hata Sen. Clinton alisema kwa haki kuwa "McCain bring experience, but Obama speech". Ndiyo watu wanachoshangilia kuhusu Obama ni maneno matamu kama ya kiongozi mwingine tunayemjua.
Watu wanachofurahia ni jinsi gani anaweza kuungurama kama mkombozi akiahidi kuleta mabadiliko katika maisha ya wanadamu. Ndio anasimama katika maelfu ya watu akiahidi mbingu hapa hapa duniani na ninakumbuka wakati ule wa kampeni hadi watu wanazimia na anaharakisha kama malaika "hebu msaidieni huyo, kuna glasi ya maji karibu".. ?
Ndio tufurahie kuwa kwa Taifa lenye watu wengi weupe, taifa ambalo limewanyanyasa watu weusi, Taifa lililonufaika na utumwa na ambalo lina alama za kitumwa hadi leo hii, kwa taifa hilo hata kumpa nafasi ya kugombea tu ni jambo ambalo lazima litutie moyo.
Lakini pia tukumbuke jambo moja, kuna uwezekano mkubwa kuwa kama Obama angekuwa ni mtu mweusi ambaye wazazi wake wote ni weusi waliozaliwa kutoka katika uzao wa watumwa, yawezekana kabisa asingepewa nafasi hiyo kwani kabla yake wapo viongozi wengi weusi wenye uwezo wa lugha (Alan Keyes mmojawapo) na maneno (Revs. Jackson, Sharpton n.k) ambao kwa hakika wanajisikia resentment ya aina fulani kwa kuona kijana huyo ambaye hakulipa gharama ya haki za watu weusi. Lakini wote leo wanakubaliana bila ya shaka (na mimi naungana nao) kuwa Obama amekuja wakati muafaka, na ujumbe muafaka, katika kipindi na wakati kama huu kwa Marekani. Na hicho ndicho naamini kinaweza kumpatia ushindi.
Na hakuna kitu kingine kinachompa ujiko huo kama siku hii ya leo ambapo Bibi yake (mtu mweupe) amefariki dunia on the eve of such an historic moment. Tukumbuke kuwa nao weupe wanamclaim Obama kuwa ni wa kwao, and rightly so, kwa sababu ya rangi yake.