Rais mteule Donald Trump ameendelea kutoa vitisho vya kudai kumiliki Greenland na rasi ya Panama

Rais mteule Donald Trump ameendelea kutoa vitisho vya kudai kumiliki Greenland na rasi ya Panama

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
1736316376609.jpeg

Rais mteule Donald Trump ameendelea kutoa vitisho vya kudai kumiliki Greenland na rasi ya Panama, akisema maeneo haya ni muhimu kwa usalama wa taifa la Marekani.

Alisisitiza kuwa Marekani inayahitaji kwa usalama wa kiuchumi na kijeshi, akisema Greenland ni muhimu katika kufuatilia meli za China na Urusi.

Trump pia alikosoa Canada, akisema kuwa inapaswa kuwa jimbo la Marekani kutokana na uhusiano wao mpakani.

Hata hivyo, Waziri Mkuu wa Canada anayeondoka, Justin Trudeau, alipinga wazo hilo, akisema hakuna uwezekano wa kuungana kwa mataifa haya mawili.

Katika mkutano wa waandishi wa habari, Trump alijadili masuala mbalimbali, akipinga nguvu za upepo na kutaka Ghuba ya Mexico iitwe “Ghuba ya Amerika”.

Alidai pia kuwa rasi ya Panama inasimamiwa na China, madai ambayo yalikataliwa na Rais wa Panama.

Trump alisisitiza kuwa Marekani inapaswa kuongeza udhibiti juu ya maeneo haya muhimu kwa usalama wake.
 
Ufaransa yenyewe ina mayotte, mshangao ni kwamba inakuwaje ufaransa ikamiliki kisiwa kilicho mbali na ilipo? Greenland nayo inatakwa na marekani iwe sehemu yake, wengine nao wataitaka iceland iwe eneo lao
 
Kwani tunataka kurudi maisha ya kuvamia eneo kwa kupiga na kuliteka? Naona Trump anaitaja na Canada pia kuwa jimbo.
 
Denmark ndio kama inajifanya mmiliki wa Greenland sio fully but partially, tokea 1917 USA ilisema inamiliki Greenland but haikuweka serious attempt kuichukua, kama Trump kasema hivyo, tayari Greenland yenye population kama 56,000 tu itaenda Marekani.

Nuuk ndio mji mkuu wa Greeland na ni nchi kubwa mara 3 ya jimbo la Texas, inautajiri wa natural resources za kutosha mafuta na gas, uranium, samaki wa kutosha..!! etc
 
Trump anajua kusukuma kete zake muhimu mpaka anamaliza muhula wake vita ya Ukraine imeisha na Panama canal na Greenland imeenda
 
Wale wa kumsema Urusi kujinyakulia majimbo toka kwa Ukraine wasome na hapa
 
Ufaransa yenyewe ina mayotte, mshangao ni kwamba inakuwaje ufaransa ikamiliki kisiwa kilicho mbali na ilipo? Greenland nayo inatakwa na marekani iwe sehemu yake, wengine nao wataitaka iceland iwe eneo lao
Urusi nayo itaitaka Alaska,
Mexico nao wadai majimbo ya Texas na New Mexico.
Poland nayo iitake Kaliningrad.
 
Bila shaka ni zama za kila nchi kuanza kutengeneza silaha za maangamizi ili kujilinda na ubabe unaoanza kuchipukia.

Hebu fikiria kama wakiamua kuanza tena ukoloni tutaweza kuwazuia silaha hatuna, tunachapwa na kutawaliwa na hakuna wa kututetea
 
Back
Top Bottom