Kenya 2022 Rais Mteule wa Kenya kuapishwa Agosti 30

Kenya 2022 Rais Mteule wa Kenya kuapishwa Agosti 30

Kenya 2022 General Election

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Kwa mujibu wa Katiba ya Kenya, Iwapo mshindi atatangazwa leo, na asipate zuio la kupinga ushindi wake, Rais Mteule ataapishwa Agosti 30 ambayo ni siku 14 baada kutangazwa kwa Matokeo ya Urais

Kifungu cha 141 cha Katiba ya Kenya kuhusu Rais kuchukua Madaraka kinasema:

(1) Kuapishwa kwa Rais Mteule kutakuwa hadharani mbele ya Jaji Mkuu, au, iwapo Jaji Mkuu hayupo, Naibu Jaji Mkuu.

(2) Rais mteule ataapishwa siku ya Jumanne ya kwanza ifuatayo:
(a) siku ya 14 baada ya tarehe ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Rais, ikiwa hakuna malalamiko yaliyowasilishwa chini ya Kifungu cha 140; au
(b) siku ya 7 kufuatia tarehe ambayo Mahakama itatoa uamuzi wa kutangaza Uchaguzi kuwa halali, ikiwa ombi lolote limewasilishwa chini ya Kifungu cha 140.

(3) Rais Mteule anashika Madaraka kwa kula kiapo au uthibitisho wa uaminifu, kiapo au uthibitisho wa utekelezaji wa majukumu ya ofisi kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Tatu.

(4) Bunge kwa sheria litaweka utaratibu na sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule.
 
#Tanzania tuna jambo kubwa sana la kujifunza toka Kenya.
 
Yaani wakenya wametushinda hata sie kwa kupindua matokeo,
Haya kazi munayo,,msije mkasema ni mtz yupo huko, sio kweli mzee yupo hapa dar na leo ameshiriki marathon
 
Back
Top Bottom