Rais Museveni aamrisha jeshi kulinda biashara za Wachina Uganda

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameamrisha oparesheni inayoongozwa na jeshi ya kulinda biashara za Wachina.

Hii inafuatia mkutano aliofanya na zaidi ya wawekezaji 120 wa Kichina ambao wanasema kuwa baadhi ya viwanda vyao viliporwa na pesa nyingi kuibwa.

Hatua zilizopendekezwa na Rais Yoweri Museveni ni pamoja na kuongezwa doria maeneo vilipo viwanda na kuweka kamera za CCTV.

Nchi hiyo kwa jumla imeshuhudia kuongezeka visa vya uhalifu na wiki za hivi karibuni, jeshi limekuwa likipiga doria ndani na nje ya mji mkuu huku serikali ikibuni vikosi vya ulinzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…