Rais Museveni ajiongezea Jina

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Rais wa Uganda, anayejulikana hadharani kama Yoweri Kaguta Museveni, amebadilisha rasmi majina yake, kujumuisha jina lake la utoto,Tibuhaburwa.

Jina la Tibuhaburwa katika kabila lake la Banyankore, linaweza kutafsiriwa kama "yule ambaye hawezi kuchukua ushauri au kuongozwa / kurekebishwa".

Hatua ya Museveni kubadilisha jina imezua uvumi na utani miongoni mwa Waganda katika mitandao ya kijaii, baadhi yao wakihoji kazi ya washauri wake.

Rais alisaini tamko kama inavyotakiwa na Sheria ya Usajili wa Watu, ili kujulikana rasmi kama Yoweri Tibuhaburwa Kaguta Museveni.

Ingawa jina hilo limetajwa katika katika mazingira tofauti juu ya utawala wake wa miaka 34, hajawahi kulitumia hadharani.
Kulingana na hati ya upeanaji wa hati ya tarehe 6 Oktoba, rais anasema kwamba jina hilo limetumiwa kwenye vyeti vyake vya masomo.

Lakini inaaminika kuwa hatua hiyo inafuata mahitaji kutoka kwa Tume ya Uchaguzi, kwa wagombea wa uchaguzi 2021 kuhakikisha kuwa majina kwenye hati zao za uteuzi zinalingana na zile zilizo kwenye rekodi zao za masomo.

Tume ya uchaguzi hivi karibuni ilitangaza kuwa wagombeaji ambao majina yao kwenye karatasi zilizowasilishwa si sawa na wale walio kwenye karatasi zao za masomo hawatateuliwa.

Mnamo mwaka wa 2017, uamuzi wa mahakama ulibatilisha ushindi wa mbunge kwa misingi kwamba amebadilisha majina yake kwenye hati tofauti rasmi.
 

Attachments

  • 1602507926970.gif
    42 bytes · Views: 2
Ingekuwa nchi hii hapa halafu yupo chama cha upinzani angeenguliwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…