Rais Museveni alijisikiaje baada ya kuona video na taarifa za kifo cha huyu mtu?

feyzal

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2016
Posts
7,683
Reaction score
15,128
Raia wa sehemu hiyo ni watu wanaounga mkono harakati za Boby Wine kwa yanayofanywa na Museveni huko Uganda aliyepokea kipigo na kufa baadae baada ya kipigo anajulikana kwa jina la Sweet Pepsi (Ssewankambo Hannington).

================

Ssewankambo Hannington maarufu kama Sweet Pepsi ambaye alipigwa na wanausalama wa Uganda katika maandamano ya ‘’Free Bobi Wine’’ mwaka jana, amefariki dunia.

Taarifa kutoka kwa wanafamilia yake wanasema kijana huyo aliyekuwa mfuasi wa harakati za ‘’People Power’’ alivuta pumzi yake ya mwisho siku ya Jumatano.

Mwanahabari wa BBC Atulinda Allan ambaye alimsaidia Sweet Pepsi kwa kumfunga ‘bandage’ baada ya kupwigwa na wanajeshi amesema kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii kuwa amepata taarifa za kifo hicho kutoka kwa dada wa Sweet Pepsi.


Your browser is not able to display this video.
 
Wanywa damu ulishaona wanasikitika? Nadhani alitaka akailambe kabisa. Samahani kwa maneno haya ila inatia uchungu.
 
Ukiwa chama pinzani lazima upate tabu sana ! I hope Bob wine hatapoteza focus kwenye harakati zake
Rest easy young soul
 
Sidhani kama kuna kiongozi yeyote kwenye tukio kama hilo yakayokea hayo ati atakisikia vibaya hakuna
 
Museveni anajisikia poa tu...hata huku kwetu kuna watu wanakufa(mfano Akwilina, Daniel, Mawazo) lakini kuna mtu anajisikia poa tu yani fresh na Jumapili anaingia Church kama kawa yani
 
Nakumbuka historia kadhaa niliwahi kusoma miaka kadhaa iliyopita, Mapinduzi ya Uingereza, Mapinduzi ya Ufaransa yalianza hivyo hivyo. Iko siku Umma utaingia barabarani na hakuna Askari atakaeweza kudhibiti
 
Wakati naiona hiyo video nilipata uchungu sana utadhani huyo jamaa ndugu yangu
Museveni anajisikia poa tu...hata huku kwetu kuna watu wanakufa(mfano Akwilina, Daniel, Mawazo) lakini kuna mtu anajisikia poa tu yani fresh na Jumapili anaingia Church kama kawa yani
 
Inatia sana uchungu ni unyama wa hali ya juu sana
Wanywa damu ulishaona wanasikitika? Nadhani alitaka akailambe kabisa. Samahani kwa maneno haya ila inatia uchungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…