BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema baada ya kifo cha Oulanya ametoa amri kwa Polisi kufuatilia wanaondika kwenye mitandao ya kijamii kuwa Jacob Oulanya alifariki baada ya kupewa sumu, wakamatwe ili watoe ufafanuzi na kueleza Polisi kile wanachokijua.
Pamoja na hivyo, bado familia ya Oulanya, inasisitiza kwamba alipewa sumu. Oulanyah aliaga dunia Machi 19, 2022 alipokuwa akipokea matibabu Nchini Marekani baada ya kutibiwa katika hospitali tofauti nchini Uganda na Kenya.
Wakati wa mazishi yake, baba wa Oulanya, Nathan L’Okori kupitia kwa mkalimani alisema kwa lugha ya Luo kwamba “Nataka walio hapa wote kujua kwamba Oulanyah alipewa sumu. Aliniambia mwenyewe kwamba alipewa sumu. Alifanyiwa upasuaji. Madaktari walijaribu kukabiliana na sumu hiyo lakini tayari ilikuwa imesambaa mwilini. Wakati alisafirishwa kwa ndege kupata matibabu Marekani, alikuwa katika hali mbaya ambayo hasingepona.”
Ripoti ya kwanza kuhusu Spika kupewa sumu
Mnamo mwezi Agosti, 2021, Gazeti la Observor la Uganda liliripoti kwamba “Rais Yoweri Museveni alikuwa ameagiza timu maalum ya usalama kuchunguza sababu zilizokuwa zikipelekea afya ya Spika Jcaob Oulanyah, ikiwemo madai ya kupewa sumu.”
Wakati wa mazishi ya Oulanya, Jumamosi AprilI 8 2022, Waziri wa Afya wa Uganda, Dr. Jane Ruth Aceng alisema kwamba “Oulanya alifariki baada ya viungo muhimu mwilini kukosa kufanya kazi. Moyo ulishindwa kufanya kazi, mapafu, ini na kulikuwa na maambukizi katika sehemu kadhaa za mwili.”
Licha ya Polisi kushikilia kwamba itawakamata na kuwazuia wanaosema kwamba aliyekuwa Spika Oulanya alipewa sumu, madai bado yanaenea Uganda.
Naibu wa chama kinachotawala asema alijua kuhusu ‘Oulanya kupewa sumu’
Naibu Mwenyekiti wa chama kinachotawala cha National Resistance Movement (NRM), Godfrey Kiwanda ameambia radio ya Capital FM katika mjadala maalum, Jumapili asubuhi AprilI 9, kwamba Jacob Oulanya alimwambia alikuwa amepewa sumu na kwamba tukio hilo lilifanyika mUda mfupi baada ya kushinda uchaguzi wa kiti cha spika, mwezi Mei, 2021.
Kiwanda, ambaye alikuwa Waziri wa Utalii katika Serikali ya Museveni, amesema kwamba anaamini kwamba haoni kama kuna ripoti zinazokinzana kati ya madai ya Oulanya kupewa sumu na ripoti ya madaktari katika hospitali ya Marekani, ambayo haikusema kwamba Oulanya alikufa kutokana na viungo muhimu mwilini kukosa kufanya kazi kutokana na ugonjwa wa saratani inavyosema serikali.
Video ya NTV Uganda, iliyowekwa kwenye mitandao ya kijamii, inaonyesha Godfrey Kiwanda, akisisitiza: “Oulanya mwenyewe aliniambia kwamba alipewa sumu. Hakujua ni wapi alipewa sumu hiyo wala hakuniambia aliyempa sumu. Sasa haya madai ya aliyekuwa spika kupewa sumu hayakuanza kwa familia yake. Yalianza na Oulanya mwenyewe akiwa hai. Na siwezi kunyamaza kusema ninachokijua. Hata niliambia baadhi ya watu wakati Oulanya alikuwa bado hai.”
Chanzo: VOA